Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

Dr. Kafumu (CCM) avuliwa ubunge Igunga!

rostam aziz yupo kwenye siasa za kenya,siasa za bongo ni uchwara
 
Ubunge Igunga: Dr Kafumu, "fuuuumuuuu"!
 
Hii ni failure kubwa kwa Mwigulu Nchemba. Igunga ndiye alikuwa kinara wa kampeni sasa chali, Arumeru Mashariki alikuwa kinara wa kampeni nako alipigwa mweleka. Sasa CCM waangalie sana huyu jamaa, atazidi kuwapeleka kaburini mapema.

Hivi unafikiri mtu kama Mchemba anavalisha mbwa bendera ya Chadema unafikiri kichwani pana kitu kweli?,au umeuasahau Yale matusi ya Arumeru Mashariki namna ccm ilivuna laaana!?
 


tutakata rufaa haki itapatikana..
Kwanini msimshukie Magufuli? yeye ndie alikacha kwenda kupangua ushahidi! sasa hata mkikata rufaa Magufuli atakwenda kukanusha tuhuma za kauri zake za rushwa ya kujenga daraja la Ndutu?
 
nakumbuka sana mh. Nape nnauye ndo alikuwa wa kwanza kuja kuzomea chadema hapa jf, tunataka aje atoe msimamo wake hapa tena baada ya hukumu hii. Kwa kweli siku ile alitumia maneno ambayo hakustahili kuyatumia kwa nafasi yake. Ningefurahi akija tena leo tumsikie mh sana.

amegoma kuongelea hukumu hii kule itv na redio one jamvini ndio hawezi kutia mguu aelekeze shingo yake kimbla kashindye akate shingo yake.
 
.WANA BODI MNAMKUMBUKA HUYU KIJANA AMBAYE MWIGULU ALIMWAGIA TINDIKALI NA KUSINGIZIA CHADEMA?
MWIGULU ALIPATA LAANA KUANZIA HAPA HADI SASA ANAENDELEA KUUWA VIJANA KWA KUTUMIA PROPAGANDA KUWA CHADEMA NI CHAMA CHA VURUGU... AIBU KUUWA, KUUMIZA KISA MADARAKA YA KISIASA... SASA KAFIKA WAPI HUYO KAMFUMU?

1.jpg

MKAZI wa Igunga, Kada wa CCM, Mussa Tesha aliyekuwa nchini India kwa matibabu baada ya kumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADAEMA), wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo (Igunga) mwaka jana, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, baada ya kurejea nchini. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni za CCM jimboni humo.

images


Angalia leo alivyo na huzuni utadhani ni kweli,kumbe magumashi ya mnyilamba
 
chadema yashinda rufaa igunga.....dr kafumu kukata rufaa mahakama kuu....chanzo habari leo
 
Sidhani kama Rostam ana hamu na CCM tena...na sidhani kama atakuabli kula matapishi yake. Kumbuka kauli yake, nimejitoa CCM kwasababu ya siasa uchwara zinazoendeshwa na baadhi ya viongozi na makada wa chama hiki.
 
Dah, nina furaha ya ajabu sana.
Nmebahatika kusikia sehemu ya mahojiano ya Bw. Dr. Dalali Kafumu na Itv.
Amechanganyikiwa aisee, anaaga mara mia mia anamualika mwandishi Igunga, anadai anarudi kwenye fani yake ya madini.
Nmecheka sana.

Kazi ilikuwa pevu mwandishi alipojiroga kumuhoji Nape.....
 
HUKUMU ya IGUNGA Leo..Kashinje Vs Kafumu,


....Kwakweli mpaka sasa hivi Mbunge wa CCM ameshindwa kumleta shahidi ambaye angetoa taswira njema kwa Ushindi wa Kafumu.
Kwani Bwana Magufuli, ambaye yeye ametajwa kwenye Kesi mara kadhaa; kwamba alikuwa akitoa Ahadi ambazo alikuwa akitoa
mbele ya Jukwaa..kwa hali hiyo Mgombea Wa Chadema anasema alikuwa anatoa Kama Nani? Waziri au mpiga Debe wa CCM?

Kwakweli Kesi imekaa patamu sana...kama Haki ikitendeka ...Basi Jimbo tutalajie kuwa Wazi katika Hukumu ya Leo..!!!

=======
UPDATES
=======

Magari ya polisi, gari la maji washa, naona ndo yanawasili hapa mahakamani, ila bado hatujaingia ndani ya ukumbi wa mahakama, pia watu bado si wengi sana.



Hii inaweza kuwa ni kwa sababu ya Nondo ya Tundu Lissu aliowapiga majaji, kwani sasa naona wanafanya kazi yao kiitaaluma na kimaadili!!
 
Taarifa kuwa Dk Peter Kafumu amevuliwa ubunge ni za kufurahisha kutokana na rafu aliyocheza yeye na chama chake kushinda ubunge. Sasa si siri kuwa CCM imo njia panda kuhusiana jinsi ya kurejesha kiti hicho hasa ikizingatiwa kilichotokea Arumeru Mashariki. Je kudondoka kwa Kafumu ni haki kutendeka au maandalizi ya kumrejesha ugani Rostam Aziz?

Hivi unavuta bangi?
 
Mahakama imetenda haki kabisa!!!!! MUNGU ibariki Tanzania MUNGU ibariki CDM
 
first eleven aliomfumua Kamfum na kumponza Kamfumu ni-:
1. Mwigulu
2.Lusinde
3. Nape
4. Magufuli
5. Mkapa
6.DC Hawa
7. Bakwata Igunga
8.Wassira
9. Ester Bulaya
10. aliekuwa mbunge wa Sumbawanga...
11......
 
Nina kila sababu ya kupata Konyagi leo! Remmy, tafadhali sn leo nitakuwa pale YENU BAR kuanzia saa 2.30 za usiku, nikukabidhi kabisa haya mananihii aisee!, usikose. sweetlady, nyie huko Arusha mnisubiri tu, nina zawadi zenu wote, najua lile kinywaji lako unalotumia ambalo lina Historia ya kumsababishia mtu fulani Brain Concussion!


Sitakosa maana furaha niliyo nayo si haba. Hivi nakaribia.
 
Last edited by a moderator:
Nina kila sababu ya kupata Konyagi leo! Remmy, tafadhali sn leo nitakuwa pale YENU BAR kuanzia saa 2.30 za usiku, nikukabidhi kabisa haya mananihii aisee!, usikose. sweetlady, nyie huko Arusha mnisubiri tu, nina zawadi zenu wote, najua lile kinywaji lako unalotumia ambalo lina Historia ya kumsababishia mtu fulani Brain Concussion!

Hahahahaha......mie nimetulia tu kwa furaha nasubiria hizo zawadi zetu lol.......Raha sana PakaJimmy ila usilewe sana eeh???? .....tusijekuokota mabwepande huna meno!........bado tunakutegemea sana katika ujenzi wa Taifa !
 
Last edited by a moderator:
tatizo la mwigulu nchenba anajiona kwamba ameshafika na kujiona ni kati ya MASTAA WA CCM kimbelembele chake, kiburi, jazba na kujifanya anajua kila kitu kinawapa hasira watu ya kumng'oa na yeye mwaka 2015, kwa dalili zote za watu wa Iramba na Singida kwa ujumla ameshachokwa
 
Back
Top Bottom