Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 25,251
- 18,630
Ndugu zangu Watanzania,
Ninayo furaha kubwa sana Moyoni Mwangu kumtakia heri ya kuzaliwa mzee wetu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya Nne,Mwanajeshi mstaafu,mwanadiplomasia Nguli,Mwana Demokrasia aliyekomaa,Kipenzi cha watanzania na waafrika na DUNIA nzima kwa ujumla wake aliyezaliwa siku kama ya leo yaani Tarehe 7 -10-1950.
Nitaendelea kumkumbuka kwa Mengi sana huyu mzee wakati wa utawala na uongozi wake. Ni yeye aliyenishawishi kujiunga CCM mwaka 2005 alipokuja kwenye kampeni za Urais mkoani Rukwa ,wilaya ya Sumbawanga vijijini ,mji mdogo wa Laela, Jimbo la Kwela lililoongozwa kwa muda mrefu na Marehemu mzee Chrisant Maji ya Tanga Mzindakaya. Ni yeye na serikali yake aliyenipatia mkopo wa Elimu ya juu ambapo kama siyo kupata mkopo huo basi nisingeweza kupata Elimu hiyo ndani ya chuo kikuu cha Dar es salaam.
Watanzania na hususani vijana wataendelea kumkumbuka mzee huyu asiye na makuu wala majivuno.ni kiongozi ambaye alifikika na makundi yote ,alimfariji kila mtu,alimpatia matumaini kila mtu,aligusa maisha ya wengi sana ,alitoa misaada kwa wengi sana.na kwa hakika watu waliguswa vyema sana.Alikuwa mtu wa watu,mtu wa Msaada na hakuona uvivu kuinuka na kutoka ofisini kwenda kumpa faraja mtu au mtanzania mmoja tu mwenye shida na tatizo iwe ni hospitalini au nyumbani.
Alitoa ajira kwa vijana mpaka watu wakawa wanachagua mahali pa kufanyia kazi kati ya mijini na vijijini. Ukimaliza tu chuo hasa ualimu na udaktari ilikuwa ni lazima upate ajira tu .ilikuwa ni raha sana kiukweli kwa waliobahatika au waliomaliza vyuo wakati wake maana walipata bahati sana tena kubwa ya ajira..
Alitukanwa sana huyu Mzee ,alidhalilishwa sana lakini alibakia mtulivu mwenye tabasamu ya uso na moyo na kumsamehe kila mtu ,na kuwafanya watu waliomtukana kujutia baadaye alipoondoka madarakani. Alijuwa kuwalea na kuwakuza viongozi na kuibua vipaji vya uongozi .hakuwa na chuki na mtu wala baya na mtu.alikuwa mvumilivu sana huyu Mzee na aliwapenda sana Watanzania.hakuwa na visasi wala chuki na mtu.ni Mwenyewe alisema za kuambiwa changanya na zako maana hakupenda kurithishwa adui au maadui au kumezeshwa chuki au uongo au uchonganishi na mtu fulani.
Alileta tabasamu kwa kila mtu.yeyote aliweza kuwa kiongozi wakati wake bila kujali hali yake au ukoo alipotokea mtu.alichoangalia ni uwezo wa mtu kiuongozi.mikono yake imekuwa daraja na imewabeba watu wengi sana kiuongozi, Mabega yake na mgongo wake umewabeba wengi sana kuwainua na kuwasogeza mbele. Hata sasa ukiangalia viongozi wakubwa na ngazi ya juu kabisa serikalini na hata katika Baraza la Mawaziri utaona wamepita mikononi mwake .
Mungu aendelee kumjalia maisha marefu yenye heri ,amani ,furaha na baraka tele.aishi maisha marefu zaidi ya karne moja hapa Duniani.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.