Dr Hussein Mwinyi awe rais wa Tanzania 2015

Status
Not open for further replies.
Si bora Pombe Magufuri?

Wanamtandao, ambao imegundulika kuwa wengi wao ndio mafisadi, wanamwogopa huyu JPM mpambanaji wa ukweli.

Kama vp muungano ufe, tutengane kabla ya 2015, iwepo Tanganyika na Zanzibar kama nchi mbili jirani tu. Huyo Mwinyi arudi kwao Znz akatafute mafuta ya kufikirika, yajaa kwenye kinibu.
 
Si bora Pombe Magufuri?

Huyu akiwa rais twaweza ona kasi ya maendeleo ya kweli. Jamaa ni mzalendo kwelikweli na mchapakazi. Huponzwa tu na wakubwa wake wakati mwingine kama vile BWM alivyomponza kwenye dili la kuuza nyumba za serikali.
 
Tanzania si nchi ya kifalme. Nafikiri mtoa mada ni mmoja wa watu wale waliotayari kuuza utu wao kwa bei ya chee. Bila shaka ametoa maoni yake baada ya kupewa Tsh.10,000 au kidogo juu ya hapo. Hana tofauti na wale wauzao kura kwa kupewa pilau,kanga na kofia za CCM. Mimi pia nautaka uraisi mwaka 2015,sasa kusema Hussein ndo awe mgombea ni kunikatisha tamaa na wengine wenye nia kama yangu.
 
Hussein N.O

Labda Makufuli, Pinda, Mwandosya, Yambesi, George Waitara...... and the list goes on
 
hata marekani kwenyewe wameshindwa na kina kenedy, bush, clinton na wenzao wanarithishana madaraka. Au hujasikia kuwa Chelsea Clinton anataka useneta pia baadaye agombee uraisi?

hiyo haihalalishi na sisi tuanze kuiga
 
ah

angekuwa huyo hussein m ndo magufuli, masaka ningekuunga mkono.
lakin ajabu sijui kwanin hujampendekeza magufuli. au kwasababu babake hakuwa rais siku za nyuma

mtu wa kawaida kama mie kazi za magufuli naziona na nazisikia. hussein mwinyi namsikia bungeni tu. au labda anapewa wizara zinazomficha

kwangu ni rahis kuimagine magufuli anaweza kuwakuwaje akiwa rais. kwa hussein sipat picha
 
Kwa vile Zitto ameonekana kuwa ana nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 baada ya muda wa maendeleo ya uhakika yanayoletwa na Kikwete kuisha. Ni vyema sasa ikaangaliwa kwa upande wa ccm ni kina nani wenye uwezo wa kugalagaza wapinzani kwenye uchaguzi. Ni ukweli kuwa ccm itashinda tena kwa kishindo 2010 na kwa kishindo zaidi 2015, 2020, 2025, 2030, 2035 nk, mimi naanza na huu uchaguzi wa 2015 na kumpendekeza Dr Mwinyi kwa hii nafasi muhimu kabisa.

Ni msomi na mchapakazi mzuri. Ni mchamungu na msafi. Mwenzetu huyu ni mpole na mkarimu kama baba yake. Ruhusa na maendeleo ya watanzania wote kama aliyoleta baba yake. Ataendeleza sera za maendeleo za ccm na kuwanyima wahafidhina nafasi ya kuvuruga nchi.

Dr Hussein Mwinyi for president of Tanzania - 2015

Mbona Dr Shein ana sifa zaidi ya hizo,na cha muhimu zaidi,amekuwa VP kwa muda mrefu sasa!

Come Mwinyi Jr,or even Mwinyi Sr,CCM MUST GO,NOW!
 
Hayo maendeleo anayosema Mkuu Masaka kuletwa na Mh. Mwinyi sijui ni yapi. Watu wanahitaji REKODI na si LONGOLONGO. Taja hayo maendeleo na watu watajadili ukweli na si kuleta triki za Uhuru na Mzalendo hapa.

Labda kwa vile alituletea daladala za chai maharage,ndo maendeleo anayoyaona.
 
Huyu kijana safi hana ufisadi hata kidogo, kama umemsikia kwenye kashifa yoyote ile useme.

2015 - Hussein Mwinyi
2025 - Ridhiwani Kikwete
2035 - Kama kuna mjukuu wa Karume atapewa nafasi hapa

Mbona kwa Che Nkapa hamsemi????????? anyway porojo za kijiweni hizi
 
Kwa vile Zitto ameonekana kuwa ana nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 baada ya muda wa maendeleo ya uhakika yanayoletwa na Kikwete kuisha. Ni vyema sasa ikaangaliwa kwa upande wa ccm ni kina nani wenye uwezo wa kugalagaza wapinzani kwenye uchaguzi. Ni ukweli kuwa ccm itashinda tena kwa kishindo 2010 na kwa kishindo zaidi 2015, 2020, 2025, 2030, 2035 nk, mimi naanza na huu uchaguzi wa 2015 na kumpendekeza Dr Mwinyi kwa hii nafasi muhimu kabisa.

Ni msomi na mchapakazi mzuri. Ni mchamungu na msafi. Mwenzetu huyu ni mpole na mkarimu kama baba yake. Ruhusa na maendeleo ya watanzania wote kama aliyoleta baba yake. Ataendeleza sera za maendeleo za ccm na kuwanyima wahafidhina nafasi ya kuvuruga nchi.

Dr Hussein Mwinyi for president of Tanzania - 2015

sina tatizo na maoni yako, eleza tu kwa kifupi kafanya nini (with evidence) mpaka sasa , itakuwa indicator ya nzuri, isije kuwa kama JK
 
Masaka,
Nadhani umefanikiwa sana katika hii thread yako, wengi wa wachangiaji wameonesha kuingiwa na woga zaidi pale wanaposhindwa kutoa sababu za msingi kwani asiwe Dr.Mwinyi kwenye uchaguzi wa 2015. Baadhi wameishia kusema kuwa hii si nchi ya kisultan bila ya kujua kuwa kwa maneno ndiyo wanakubaliana na mawazo yako kuwa Dr Mwinyi ana nafasi ya kuchaguliwa kama wanavyochaguliwa viongozi wengine kwa vile nchi hii kiongozi anapatikana kwa uchaguzi wa kidemokrasia. Wengi wanadhani 2015 ni mbali kwa maana ya kutayarisha kiongozi ajaye, hasha ni kama kufumba na kufumbua.
 
Bado sijaona hoja za kumsupport wala kumpinga huyo Hussein. Ila siyo vibaya huyo aliye leta hoja angeorodhesha sifa na mafanikio ya bwana Mwinyi Jr. Maana sijamuelewa kuwa ana msupport kwa mafanikio aliyo nayo sasa hivi au kwa mafanikio ambayo ana tarajia atakuwa nayo ifikapo 2015. Hoja pekee ninazo ziona kwa sana ni Hussein awe au asiwe raisi kwa sababu ya baba yake. Hiyo baba ake kuwa raisi hakumfanyi awe au asiwe mtu mwenye kigezo cha kuwa raisi. Kuna baadhi ya wachangiaji wametoa hoja nzuri kutetea hoja zao otherwise zingine ni ze komedi tu. Cha msingi ni zitolewe sifa zake na aliye weka thread zijadiliwe sifa zake siyo jina.
 
hivi tunavyojadili Rais wa 2015 ina maana tumeshakubali JK anaendelea bila kupingwa?hii si itajenga utumwa kwamba kila rais akichaguliwa lazima afike miaka 10 hata kama ni ZERO?kwa nini JF isianze na mikakati ya CV za rais wa 2015 ili kama Dr HAM anafikikia kiwango basi ruksa.
 
huu mjadala unaelekea patamu...ila aliyesema Dr.Mwinyi awe rais rais 2015 hajabainisha yale aliyoona kwa bwana huyu...ni kweli nakubali kabisa Dr. Mwinyi ni mtaratibu si mtu wa kujikweza ni vigumu kujua hasa anawaza nini maana ni mkwimya sana...he is so honest...hata serikali ilipotoa medali za wale walienda kukomboa kile kisiwa cha anjwani yeye hakupata medali badala yake alipata waziri wa mambo ya nje...suala la mabomu mbagala lilitakiwa liwe big issue lakini angalia linavyochukuliwa..raisi yupo safarini, kazi za mwinyi anafanya mkuu wa mkoa...kwenye suala la ufisadi ni kweli Dr.Mwinyi ni very clean...aliwahi kuwa offered 35% ya HITS (kampuni mpya ya simu) (awe kama rostam kwa vodacom) lakini alichomoa na kumuachia mdogo wake Abdulah Mwinyi (ambaye ni mbunge wa EA) na mwenye ASYLA ATTRNEY pale Moroko, mwanasheria, na ndio mweyekiti wa board ya HITS, kwa Taarifa tu HITS sasa imekwama kiuchumi na wamestuck kidogo...
Dr.Mwinyi sio kiongozi mzuri kwa kumpa nchi, hana historia ya uongozi, anabebwa na historia ya mzee wake ambaye alinaswa kibao siku chache zilizopita katika shughuli ya kidini...huyu ni mtu ambaye anafaa kutumwa yaani awe chini ya mtu japo anaoneka na yeye kuwa anania ya kuwa raisi wa zenji...ifike hatua tuchague viongozi ambao wanahistoria ya uongozi mzuri isije ikawa kama JK..big mistake...Dr.mwinyi labda kwa zenji sio bara...

sasa mimi nimeona nimpendekeze mtu ambaye kweli anaonekana anafaa kuongoza hii nchi kwa miaka ijayo..huyu ni MIZENGO KAYANZA PETER PINDA...huyu bwana ni kiongozi mzuri sana na hajawa corrupted so far na anamsimamo mzuri saa nyingine hata unaopingana na serikali na kweli anafanya kazi hana longolongo...na ccm kama kweli wanaona mbali this is their last man...wasiwasi wangu ni kwamba anaonekana kupata upinzani mkubwa sana ndani ya chama na serikali kwa misimamo yake...angalia hata anavyojibu maswali ya moja kwa moja pale bungeni...this is the leader na anatakiwa mtu kama huyu apewe madaraka zaidi ili kusimamia maendeleo..kwani anaweza, kwa sasa JK anamfunga speed gorvenor...
 
Huyo Dr. Mwinyi ana tofauti gani na JK? JK naye tuliambiwa tu kwamba anatufaa sana, tena na viongozi wa dini wakatuambia kwamba ni chaguo la Mungu...Wachache wakahoji anatufaa kivipi na katika rekodi yake ya kiutendaji amefanya nini kikubwa, hakukuwa na majibu zaidi ya Prince Bagenda kutuambia kwamba ...JK ni Tumaini lililorejea!

Baada ya hapo akashinda uchaguzi, na sasa watu wanalalamika kwamba hakuna la maana analofanya zaidi ya kusafiri kila siku. Maisha yamezidi kuwa magumu, serikali inafanya kazi kwa mtindo wa zimamoto....Hali ya uchumi haieleweki, ili mradi kunakucha tu basi!

Kwa hiyo sitashangaa hata huyo Dr. Mwinyi kama wajanja wakifanikiwa "kumtengeneza" na kuwafanya Watanzania waamini yeye ndiye "Mesia" na ataifanya nchi hii iwe ya kumiminika maziwa na asali. Na pengine wanaweza wakafanikiwa. Kwa umbumbumbu wa Watanzania walio wengi, lolote kwenye uchaguzi linawezekana!

Ni nani hapa ndani anaweza kuniambia kwanini Dar es Salaam ambako tuko tunaamini watu wengi wamepuvuka angalau kidogo kisiasa, hakuna jimbo hata moja lililoko mikononi mwa wapinzani????

Fikiria, chukua hatua !
 
Kwa vile Zitto ameonekana kuwa ana nia ya kugombea uraisi mwaka 2015 baada ya muda wa maendeleo ya uhakika yanayoletwa na Kikwete kuisha. Ni vyema sasa ikaangaliwa kwa upande wa ccm ni kina nani wenye uwezo wa kugalagaza wapinzani kwenye uchaguzi. Ni ukweli kuwa ccm itashinda tena kwa kishindo 2010 na kwa kishindo zaidi 2015, 2020, 2025, 2030, 2035 nk, mimi naanza na huu uchaguzi wa 2015 na kumpendekeza Dr Mwinyi kwa hii nafasi muhimu kabisa.

Ni msomi na mchapakazi mzuri. Ni mchamungu na msafi. Mwenzetu huyu ni mpole na mkarimu kama baba yake. Ruhusa na maendeleo ya watanzania wote kama aliyoleta baba yake. Ataendeleza sera za maendeleo za ccm na kuwanyima wahafidhina nafasi ya kuvuruga nchi.

Dr Hussein Mwinyi for president of Tanzania - 2015

Na ni baba yake huyo huyo ndie aliyefuta Azimio La Arusha na kuleta Azimio la ZANZIBAR na matokeo yake leo wanyoge wapiga kura wanakiona kilichomfanya kuku kunywa maji shingo juu, sasa hatujuwi mtoto ataleta azimio gani,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom