Dr. Hassan Mshinda, DG wa COSTECH...


Inategemea alisoma nchi gani hiyo Masters, kwa kuwa miaka ya nyuma kwenye nchi nyingi za Ulaya mashariki na magharibi hawakuwa na Bsc wala MA, bali ulikuwa na unasoma unagraduate na Masters (Miaka mitano ya kusoma). Nchi kama ujerumani, Bulgaria, Polanda Scheck,). Hata leo ujerumani kuna vyo bado vina mfumo huo wa Masters unasoma miaka mitano kwa kuwa inajumuisha masomo yote ya awali na yale ya ngazi ya juu.
 



Background ya Mshinda ni Lab Technician alieanza na Advanced Diploma. Wakati curriculum ya universities zetu tofauti na sasa ilikuwa hairuhusu mweny Adv Dipl kusoma BSc. Uingereza, tangu zamani mwenye ADv Diploma alikuwa anawekwe kwenye equivqalence ya First degree hivyo anaruhusiwa kusoma MSc. Nadhani Mshinda ni mmoja kati ya waTZ wengi tunaowafahamu waliofuata mkondo huo. Just for our information.
 
Sasa wewe Mchungaji Masa kama ungelikuwa Muislaam, sasa hivi ungelikuwa boss wa Costech 🙂 Wewe ukaenda kuwa Mchungaji.

Hili shirika lilikuwa kubwa na linatisha enzi za Prof. Kayumbo.

Sasa hivi bora liende.... RIP COSTECH.
 

Kaka umeanzisha mada mpya
 
Sasa wewe Mchungaji Masa kama ungelikuwa Muislaam, sasa hivi ungelikuwa boss wa Costech 🙂 Wewe ukaenda kuwa Mchungaji.

Hili shirika lilikuwa kubwa na linatisha enzi za Prof. Kayumbo.

Sasa hivi bora liende.... RIP COSTECH.

Sikonge,
Sikutegemea kauli kama hii kutoka kwako.
Btw maoni yako ni yepi katika uteuzi na utendaji wa Daktari Mshinda? Hasa hili la elimu una lolote la kusema?
 

Nimekubali umesema toka moyoni
 
Simfahamu huyu jamaa na hivyo siwezi kusema lolote.

Nalifahamu hili shirika tangu wapo Wizara ya Elimu. Baadaye wakahamia kwenye majengo ya Tanzania Film na mwisho ndiyo kuja kwenye jengo lao hapo Kijitonyama.

Miaka ya 80 kulikuwa na shughuli nyingi wanafanya na mie mwenyewe nakumbuka kupewa project ya mabomba ya mianzi niangalie huo utafiti na kutoa maoni ila wakati ule uwezo wangu ulikuwa chini sana na nikashindwa kutoa majibu.
Miaka hiyo hawa jamaa walikuwa wanasomesha sana watu wao na kufanya tafiti nyingi sana. Baadhi ya Project zao nakumbuka kuona picha hadi Nyerere alikuwa akizitembelea sehemu mbali mbali walipokuwa wanafanya.

Nafikiri miaka ya 90 mwishoni, likaanza kushuka chini na kama sikosei ndiyo enzi za Koch sijui? Wengi walilikimbia na ukichanganya na huu ukata wa sasa wa Kikwete, sijui wana hali gani. Kuja kwa huyu jamaa hakutasaidia kitu sana kwani Samaki ameshaanza kuozea kichwani (Serikali).

Hayo mengine huwezi kuyafahamu vizuri labda uwe na kumbukumbu ya mengi sana yanayoandikwa kuhusu Medicine in Tanzania. Ni UTANI ulio na ukweli na haswa kwa walengwa. Huo u-Islaam au Ukristo usikutishe sana maana ukitaka kunielewa mie ni kuwa, nikiwa Rais wa Tanzania, ntapiga marufuku DINI ZOTE kwa miaka 10-15.

Sikonge,
Sikutegemea kauli kama hii kutoka kwako.
Btw maoni yako ni yepi katika uteuzi na utendaji wa Daktari Mshinda? Hasa hili la elimu una lolote la kusema?
 
Nitaandika baadaye nikiongea na mmoja wa waathirika yeye aliletwa hapa UDSM. Lakini kiufupi ukristo ulimwondoa.
 
Mimi sina shaka na uwezo na qualification za Dr. Mshinda japo aliruka from Ad Dipl na kufanya MSc kwa kukingiwa kifua na Waswiss hasa Prof. Marcel Tanner wa Basel University.

Hayo machapisho yote kwenye peer review journals mengi amekuwa co-author sio kwamba kwasababu ame-contribute scientifically kwenye hizo papers lakini tu kwasababu alikuwa head wa IHI. It is WRONG lakini ndivyo Taasisi za Utafiti Tanzania zinavyoendeshwa. Wazungu wanatufahamu na wanafanya hivyo.

Mtu ambaye pamoja na sasa hivi kuwa head wa IHI lakini anafanya sayansi (utafiti) bila kubebwa na cheo chake ni Dr. Abdullah Salim. Huyu Mzanzibari ni kichwa, hata Mshinda anamfahamu na anamuheshimu sana kwasabbu ya uwezo wake. Ni Wanasayansi wacahache sana Tanzania wanaoweza kuchapisha tafiti zao kwenye majarida kama NATURE, LANCET etc as first author lakini Dr. Salim amefanya hivyo hata kabla hajawa head wa IHI.

Let a SPADE CALL A SPADE Weakness kubwa ya Dr. Mshinda ni UDINI. Mshinda ni MDINI wa kutupwa, uliza jamaa wote waliofanya kazi naye IHI. Hutakiwi kuwa a rocket scientist kujua kwamba huo UDINI ndiyo pia utakaotokea hapo COSTECH. Sio kwamba haya ni majungu because alishaambiwa in BLACK and WHITE mbele ya Prof Marcel Tanner, Mzungu in a soft laguage akamwambia afanyie kazi hizo tuhuma.

Ugonjwa wa UDINI wa Dr. Mshinda ni miaka nenda miaka rudi, ameshindwa kujirekebisha.
 

Kwa mara nyingine umeshindwa kuthibitisha tuhuma hizo, pia rudi ukaangalie ni vigezo gani mtu anakuwa co-author katika published article, sio kweli kwamba kwa kuwa director mtu automatically anakuwa co-author, kila journal inaainisha contribution y mtu katika chapisho lolote. niambie ni journal gani ambayo mtu anakuwa automatically co-aothored kwa kuwa director, sio kweli hata kidogo watu wengine wanakuwa acknowledged to incase hawakucontribute effectively.
Acha ubabaishaji na chuki binafsi katika hili.
Nasubiri majibu yako, na ukitaka nitakupa giidelines za hayo majournal yote kuwa co-aothored.
Kama hujui sema sijui sio kudanganya watu
 
Anafaa kugombea ubunge, tatizo jimbo lake lipo Shelisheli
 

Hivi wewe umeshawahi kuchapisha hata ka-paper kamoja kwenye peer review journal? Maana unaongea as if umeshuka leo kutoka Mars.

Thing are not BLACK and WHITE as you see dude. Yes guidelines zipo zinazoeleza sifa gani mtu anatakiwa awe nazo ili a-qualify kuwa co-author. Lakini ninasisitiza hapa Tanzania kwenye Taasisi za Utafiti sometimes guideline hizo hazifuati, na mara nyingine ni kwa watafiti wenyewe na donors kujipendekeza kwa wakubwa (DGs) au wakubwa (DGs) wenyewe kushinikiza lazima majina yao ya-apper kila paper inayotoka kwenye Taasisi/kituo chake.

Unataka uthibitisho wa aina gani? Kama uko kwenye Utafiti ninakupatia home work kidogo.
1. Angalia papers zote zilizokuwa published na IHI wakati Dr. Kitua ni DG kila paper utakuta ina Jina la Kitua
2. Angalia almost all papers zilizokuwa published na IHI wakati Dr. Mshinda ni DG wa IHI kila reputable paper ina jina la Mshinda
3. Angalia hata sasa hivi kila reputable paper yeyote inayo kuwa published na IHI ina Jina la Dr. Salim Abdullah (current DG)

Kwa kukusaidia tumia PUbMed kufanya haka ka-utafiti kadogo.

Watu hatujaja hapa JF kuchoma mahindi, tuaandika mambo tuliyo na weledi nayo!
 
Kati ya COSTECH na IHI kwangu mimi naona IHI ingawaje ni NGO iko vizuri kimaslahi binafsi kwa kuwa kuna kazi nyingi na zinatambulika duniani kuliko ilivyo COSTECH. Uamuzi wa JK kumleta hapo nafikiri ame sacrifice sana kuacha masilahi yake mazuri pale IHI na kukubali kuja kulitumikia taifa lake kwa kuwa nako kule alikuwa CEO.
 

Sorry! This is a long time direction, can you get this CV anywhere? Nimetafuta CV ya huyu boss haipo kabisaaa! Wapi ntapata? Siyo kawaida ya mtu msifiwa, CV kujificha kiasi hiki!
 
Huu sio uwanja wa MAJUNGU Ndugu :drama::drama::drama::drama::drama:

 
This is what I got from everywhere you google the name. Take care of the initial education. Kila unapoangalia ananzia Masters... hutaona Bachelor wala shule ya nyuma ya bachelor. Uliza halafu utafunika uso kwa aibu.
READ

Dr. Hassan Mshinda is the Director General of Tanzania Commission for Science and Technology in Tanzania. He completed his Master’s of Science in Applied Parasitology and Medical Technology with University of Liverpool and PhD in Epidemiology with University of Basel in Switzerland. Dr. Mshinda has led several research projects funded by Multilateral Initiative of Malaria in Africa, Tropical Diseases Research Program, World Health Organisation, Bill and Melinda Gates Foundation, Comic Relief, Swiss Agency for Development and Cooperation, International Atomic Energy Agency, International Development Research Centre in Canada, European Union, Ireland Aid and Novartis Foundation for Sustainable Development. He has published several papers in communicable diseases and health system.
Source: http://www.novartisfoundation.org/_file/272/h-mshinda-biography.pdf
 
Hivi faizafox baada ya JK kung' atuka na yeye kang'atuka haonekani kabisa!
 
Ndg Mlaki si ameshastaafu halafu huyu ni mtaalamu wa records management tu au librarian iweje ajiongeze abuni miradi yote ya jengo la costech kweli wachaga wanatisha.

Mama nae alijiongeza kivingine kwemye awamu ya mzee mkapa
 
Seriously? Ule usemi wa patriotism kwamba 'Najivunia kuwa mtanzania' sasa unanipa tabu. Watu wanazungumzia ukabila bila aibu, wanajivuna kwa udini fulani, wanajikweza kwa kuwa karibu/rafiki na kiongozi fulani, wanaleta ushabiki wa siasa za vyama katika mambo ya msingi ya kitaifa!! Man, as a nation we're doomed to fail, we are in a deep hole.
My take: Kama Dr. Mshinda ame-accomplish hayo yaliyo semwa, nashangaa Mh. JPM amechagua na kuwapa uwaziri (as leaders for change) majitu mengine ya ovyo na kumwacha mtu ka Dr. Mshinda. Watanzania wanaotaka kuendeleza ukabila subiri nyakati zenu za matambiko, na wale wa udini mambo yaishie huko huko kwenye misikiti na congregations zenu. Pleeeaase.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…