Dr. Dorothy Gwajima na makeke kama Kangi Lugola

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Binafsi Siamini kama Wizara ya Afya, ambayo kwa maoni yangu ni Wizara nyeti kabisa inahitaji kuwa na Waziri, ama viongozi wenye makeke, ama makelele yasiyo na tija.

Kwanza uzoefu unatuonesha viongozi wenye makeke/ makelele wala hawadumu katika nafasi zao maana huwa hawana Ufanisi wowote zaidi ya kuzurura huku na huko wakipiga makelele na kutofanikisha lolote... mfano, Paul Makonda, Kigwangallah, Humphrey Polepole, Kangi Lugola na juzi Magu amemtaja Jafo kuwa Anazunguka tu lkn hakuna Ufanisi wowote katika mizunguko yake hiyo na makelele yake.

Sasa ametoka Lugola kaingia Mmama mmoja ana makeke kweli, Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya na Mnyiramba wa Shelui, Singida. Naye anatembea na Ilani ya CCM na scarf ya bendera ya Tanzania kama Lugola na kama Mwigulu...makelele yaleyale, makeke yaleyale, mikogo ileile.

Namwona hafiki Mbali, kama wapo wa Karibu yake wamwambie atulize wenge afanye kazi kwa Utulivu na Maarifa

Asije kusema hatukusema, ana mdomo sana yan chaaa🤧
 
Bila ya kujali mapungufu yake, tumuombee atekeleze yale wizara na jamii yake inayohitajia toka kwake
 
Dr Gwajima anajitahidi kuboresha mfumo wa afya ili wapate wateja wengi kwenye Universal Health Carea Insurance. (Moja ya manifesto za Lissu na Chadema).

Tatizo lililopo ni mfumo mbovu wa utawala. Kama katiba inapindishwa, daktari anaefanya makosa akiwa ni ndugu wa rais atawajibishwa?
 
Back
Top Bottom