DR Congo: Mgombea wa upinzani, Felix Tshisekedi ashinda Urais. Mgombea mwenza apinga matokeo hayo


Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
81,995
Likes
49,147
Points
280
Age
28
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
81,995 49,147 280
Opposition named winner in DR Congo poll

Mgombea urais wa upande wa upinzani huko Congo-Kinshasa, Bw. Felix Tshisekedi ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais na tume ya uchaguzi ya nchini humo, CENI.

Hii ni habari mpya kabisa kwa hiyo taarifa zaidi zitafuatia.

Ila nahisi kama chama tawala hakitokubali matokeo. Nahisi tu.

Tusubiri tuone........
=======

Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia wa Congo uliokuwa una ushindani mkubwa, tume ya uchaguzi imesema Alhamisi.

Matokeo ya awali yameonyesha kuwa yeye anaongoza katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya mgombea wa upinzani Martin Fayulu, na yule wa muungano wa chama tawala Emmanuel Shadary.

Atakapo thibitishwa, Tshisekedi atakuwa mshindani mpinzani wa kwanza kushinda tangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupata uhuru.

Rais Joseph Kabila anaachia madaraka baada ya miaka 18 ya uongozi wake.

Alikuwa ameahidi kuwepo kubadilishana madaraka kwa njia ya utulivu DRC tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Ubelgiji 1960.

Chanzo: VOA Swahili

=============

Martin Fayulu, mgombea urais wa upinzani DRC aliyeibuka wa pili, ameyakataa matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) yanaonesha Felix Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi mteule wa urais."

Bw Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye Bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akimaliza wa tatu akiwa na takriban kura 4.4 milioni.

Bw Fayulu ameambia Idhaa ya Kifaransa ya BBC kuwa: "Hii ni kashfa mbaya sana. Matokeo haya hayana uhusiano hata kidogo na ukweli halisi. Raia wa Congo hawataukubali utapeli kama huu daima. Felix Tshisekedi hakupata kura 7 milioni, haiwezekani. Alizitoa wapi?"

Awali, alikuwa ameambia kituo cha redio ya Radio France International (RFI) kwamba matokeo hayo ni "mapinduzi halisi kupitia uchaguzi" na akatoa wito kwa waangalizi wa uchaguzi kuchapisha matokeo waliyo nayo aliyosema ni ya kweli.

Nchini DRC hata hivyo, ni kinyume cha sheria kwa mtu mwingine kando na CENI kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mji mkuu Kinshasa, Tshisekedi amesema atakuwa "rais wa raia wote wa Congo.

Kumekuwa na tetesi kwamba kucheleweshwa kwa shughuli ya kutangaza matokeo, ambayo awali yalitarajiwa kutangazwa Jumapili, kulitoa muda kwa Rais Kabila na Bw Tshisekedi kuafikiana.

Kanisa Katoliki limesema matokeo rasmi yaliyotangazwa na tume hiyo yanakinzana na matokeo ambayo yameandaliwa na waangalizi wake.

Wamedokeza kwamba Bw Fayulu alipata kura nyingi, kwa mujibu wa takwimu walizo nazo. Baadhi ya kura za maoni zilikuwa zinamuonesha Bw Fayulu akiwa mbele ya wagombea wengine.

Msemaji wa Bw Tshisekedi Claude Lbalanky ambaye amesema siku ya leo ni "siku njema kwa taifa" ameambia BBC kwamba hakuna makubaliano yoyote kati ya Rais Kabila na Bw Tshisekedi.

Kwa taarifa zaidi, soma:
Uchaguzi DRC: Martin Fayulu apinga matokeo ya urais DRC, Felix Tshisekedi afurahia na kumtaja Kabila kuwa 'mshirika muhimu'
 
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Messages
2,618
Likes
4,321
Points
280
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2018
2,618 4,321 280
Aisee,angalia CCM kwa nafasi hizo ulizotaja,wamepongeza???Kumbe walitaka mtawala aendelee kutawala!!!!!!!
 
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Messages
2,618
Likes
4,321
Points
280
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2018
2,618 4,321 280
Sijaona tamko lolote toka kwa Zito wa ACT wala Mashinji katibu mkuu wa Chadema wakimpongoza mpinzani kushinda urais Congo!

Kumbe mlitaka chama tawala kiendelee kutawala Congo?Sent using Jamii Forums mobile app
Usiwe unaandika bila uhakika sana sana utaonekana mwendawazimu!Kaangalie tweet ya Zitto!
Lumumba full mihemko!

Tweet ya Zitto!

My heartly and comradely congratulations to UDPS ( and UNC of @VitalKamerhe1 ) and @fatshvit for their victory in DRC #DRCElections It is my appeal to the Congolese people to remain calm in this first ever peaceful transfer of power since independence of Congo.
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,181
Likes
13,178
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,181 13,178 280
Mimi nimezianza Balimi asubuhi tu!..Walinza Zambia wakaja Malawi Kenya nao ikafuatia DRC nayo hiyo sasa ni Zamu yetu.
 
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Messages
2,618
Likes
4,321
Points
280
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2018
2,618 4,321 280
Mimi nimezianza Balimi asubuhi tu!..Walinza Zambia wakaja Malawi Kenya nao ikafuatia DRC nayo hiyo sasa ni Zamu yetu.
Hahahahaaaa,ndoto zako na zitimie!Gonga balimi 4,nikipandishwa daraja la mshahara nitakutoa!
 
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
5,548
Likes
4,395
Points
280
Age
29
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
5,548 4,395 280
Usiwe unaandika bila uhakika sana sana utaonekana mwendawazimu!Kaangalie tweet ya Zitto!
Lumumba full mihemko!

Tweet ya Zitto!

My heartly and comradely congratulations to UDPS ( and UNC of @VitalKamerhe1 ) and @fatshvit for their victory in DRC #DRCElections It is my appeal to the Congolese people to remain calm in this first ever peaceful transfer of power since independence of Congo.
Mbona mnapongezana kiunyonge sana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,181
Likes
13,178
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,181 13,178 280
Hahahahaaaa,ndoto zako na zitimie!Gonga balimi 4,nikipandishwa daraja la mshahara nitakutoa!
Siku ya Kuapishwa Lissu lazima ninywe kwa utulivu..halafu niwaige Less Wanyika:Sina makosawee bwanaa Ikulu si yaaako wala si yaangu risasi za nini kati yangu wewe na mimi×2

Halafu naongeza Balimi nyingine hahahahaha!!
 
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Messages
2,618
Likes
4,321
Points
280
T

Tigershark

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2018
2,618 4,321 280
Siku ya Kuapishwa Lissu lazima ninywe kwa utulivu..halafu niwaige Less Wanyika:Sina makosawee bwanaa Ikulu si yaaako wala si yaangu risasi za nini kati yangu wewe na mimi×2

Halafu naongeza Balimi nyingine hahahahaha!!
Umetisha kwa mistari murua kabisa,WCB hawaoni kipaji hiki?
 
L

lee van cliff

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Messages
1,675
Likes
1,471
Points
280
L

lee van cliff

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2013
1,675 1,471 280
Mimi nimezianza Balimi asubuhi tu!..Walinza Zambia wakaja Malawi Kenya nao ikafuatia DRC nayo hiyo sasa ni Zamu yetu.
Hapa kwetu UWT bado wanaipenda CCM siku wakiichukia NI kama kumsukuma mlevi
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
15,181
Likes
13,178
Points
280
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
15,181 13,178 280
Hapa kwetu UWT bado wanaipenda CCM siku wakiichukia NI kama kumsukuma mlevi
UWT wanatakiwa waamke wasingojee kitu kutoka kwenye A5 katiba inasokotewa tumbaku laa sivyo watakuwa wanasikia miungurumo ya Ndege zinazopita juu yao huku zikiwa tupu.
 
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
14,930
Likes
5,125
Points
280
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
14,930 5,125 280
Miafrika ndivyo ilivyo mkuu Nyani Ngabu. Yaani Kabila ameona kuwa kibaraka wake hakubaliki ameamua kuingia makubaliano na Tiseshekedi ili atawale kupitia kwake. Hii mijitu ya rangi nyeusi haiwezi kujitawala kamwe. Bora tu wazungu warudi kuja kututawala, hakuna namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
binti kiziwi

binti kiziwi

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2014
Messages
2,896
Likes
2,412
Points
280
binti kiziwi

binti kiziwi

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2014
2,896 2,412 280
Wamegombea CCM, CDM, ACT, CUF etc. Ameshinda CUF halafu CDM wanapinga matokeo! Hehehe kabila! kabila!
 
Alphonce Kagezi

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2015
Messages
261
Likes
98
Points
45
Alphonce Kagezi

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2015
261 98 45
Raia na Wana Siasa mjizuie kuichafua DRC ni yenu wote ,Kumbukeni mlikopitia Hadi uchaguzi huu ,Msipojizuia Kilio na Maombolezi na Majuto ya Maumivu ni yenu wenyewe kwa Nchi zingine nj hadithi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
William Ntantalila senior

William Ntantalila senior

Member
Joined
Jan 12, 2019
Messages
14
Likes
5
Points
5
William Ntantalila senior

William Ntantalila senior

Member
Joined Jan 12, 2019
14 5 5
daaah mung awasaidie watu Wa Kongo upnzan ukubali matokeo
 

Forum statistics

Threads 1,250,889
Members 481,523
Posts 29,749,700