Wanaomdharau Dr. Bilal inawezekana hawamfahamu vizuri huyu mzee, au inawezekana wameanza kumfuatilia kipindi hiki cha Umakamu wa Rais! Wanaotaka kufahamu ujuzi wa sarakasi za siasa za Dr. Bilal, basi wakamuulize Karume ambae kama si CCM Dodoma, Urais wa Zanzibar msimu wa Karume ungekuwa ni wa Bilal.....in short, alikuwa hamuwezi hata chembe kimikakati!! Na hata suala la kumfanya agombee Umakamu wa Rais, zilikuwa ni busara za CCM kwani isingeleta sense Dr. Shein aendelee kusimama kama makamu wa Rais; kwahiyo ilikuwa ni ama atupwe nje ya ulingo wa siasa au akashindane na Bilal Zanzibar! CCM wajanja, walifahamu wazi kwamba Dr. Shein asingekuwa na ubavu wa kushindana na mtandao wa Dr. Bilal; so CCM wakaona busara ni kumpa nafasi ya Umakamu wa Rais wa jamhuri ili Shein asipate ushidani wa nguvu ZNZ! Tatizo kubwa la Dr. Bilal ni umri manake by 2015, atakuwa seventy!