Dr. Bilal awaangukia UKAWA akiwa ughaibuni

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,394
2,000
Katika hali ya kushangaza Dr Bilali amewaangukia wana diaspora akiwaomba wawashawishi ukawa warejee katika bunge la katiba litakaporejea Mwezi wa nane.

Source: Mwananchi news allert

Huku chama kinasema hawatawabembeleza ukawa kurudi huku viongozi wa serikali ambao pia ni wa chama wakitafuta suluhu! Sasa ni wazi kwamba bila ukawa hakuna katiba mpya. la sivyo kungekuwa na sababu gani ya hawa viongozi kuhangaika na ukawa kiasi hicho? Cha ajabu hawasemi kwamba warudi ili wakajadili rasimu ipi: ya ccm au ya wananchi?

Ukawa kazeni buti hawa mainterahamwe karibia wananza kupata ufahamu! Go Go Mbowe, Lipumba, Mbatia. Ongezeni speed tupo nyuma yenu. Ama maoni ya wananchi yaheshimiwe au hakuna katiba. Ama zao ama zetu.

Msimamo thabiti ni muhimu katika swala hili nyeti kwa taifa letu! Na hii iwe fimbo ya kuwachapia uchaguzi mkuu wa mwakani!
 
samaki2011

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
1,776
0
hivi bilal ni yupi, au ni yule anayeongea huku anasinzia kama ndio yule inawezekana amepitiwa tu
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,501
2,000
Hawa ccm ni wanafiki tu, kwani hawawezi kukimbia kimvuli chao, madai ya UKAWA ni rahisi tu kuwa rasimu iliyoandaliwa na tume ya warioba ndio ijadiliwe bungeni.Mbona hao hawalisemi hili kuwa tulikosea basi tujadili hiyo rasimu na ukawa watarudi, maji yamewafika shingoni! Kwani zamu hii hata viongozi wa dini wamewakimbia, wameungana na hao wanaowaita wahuni!! Na hizo nyomi huko mikoani ndio zinawamaliza kabisa japo kuna wanaojifanya wagumu kuona ila moyoni wanaumia.
 
MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,277
2,000
Katika hali ya kushangaza Dr Bilali amewaangukia wana diaspora akiwaomba wawashawishi ukawa warejee katika bunge la katiba litakaporejea Mwezi wa nane.

Source: Mwananchi news allert

Huku chama kinasema hawatawabembeleza ukawa kurudi huku viongozi wa serikali ambao pia ni wa chama wakitafuta suluhu! Sasa ni wazi kwamba bila ukawa hakuna katiba mpya. la sivyo kungekuwa na sababu gani ya hawa viongozi kuhangaika na ukawa kiasi hicho? Cha ajabu hawasemi kwamba warudi ili wakajadili rasimu ipi: ya ccm au ya wananchi?

Ukawa kazeni buti hawa mainterahamwe karibia wananza kupata ufahamu! Go Go Mbowe, Lipumba, Mbatia. Ongezeni speed tupo nyuma yenu. Ama maoni ya wananchi yaheshimiwe au hakuna katiba. Ama zao ama zetu.

Msimamo thabiti ni muhimu katika swala hili nyeti kwa taifa letu! Na hii iwe fimbo ya kuwachapia uchaguzi mkuu wa mwakani!

Ni ajabu na kweli kusikia baadhi ya viongozi wa juu kama JK, Dr Bilal na PM wanajaribu kuwashawishi UKAWA kurudi bungeni lakini utamsikia Nape mpayukaji akipayuka hakuna kuwabembeleza; jino kwa jino na mambo kama hayo. hivi Who is who katika CCM; hakuna mtu wa kushape maoni na mwelekeo kila mtu asema lwake!? Ma CCM bana! majanga
 
Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
225
Hata jk hayuko serious kwani amekuwa akitia kejeli jama viongozi wengine wa juu wa cc. Vinginevyo angefanya formal plea kama vile kukaa nao ili wapeane dos and don'ts. Vinginevyo wanafanya jokes.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,841
2,000
Msimamo ni ule ule harudi mtu BMK hadi maoni ya Watanzania kuhusu katiba mpya yaheshimiwe bila kuguswa kwa namna yoyote ile na #Maintarahamwe na pia kejeli, kashfa na matusi dhidi ya UKAWA yapigwe marufuku.

makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,048
1,195
Ooyooo hee huyu wa kisongwe yupo kwa waarabu hawa ndo wale waliompindua mwarabu sasa huko wanatafuta nini huko au washakuwa omba omba na kuna nahahu baniani mbaya lakini kiatu chake ni dawa
 
Larry king

Member
May 23, 2014
39
0
Huyo Bilali ni Mnafiki tu, mbona ameshindwa kusema hayo alipokuwepo Tz? Huko JP anamlilia nani? Si wanasema hawatowaomba radhi UKAWA.
Na huko CCM msemaji wao ni nani? Kila mmoja anakuja na kauli yake!
 
Skype

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
7,278
1,195
Ni ajabu na kweli kusikia baadhi ya viongozi wa juu kama JK, Dr Bilal na PM wanajaribu kuwashawishi UKAWA kurudi bungeni lakini utamsikia Nape mpayukaji akipayuka hakuna kuwabembeleza; jino kwa jino na mambo kama hayo. hivi Who is who katika CCM; hakuna mtu wa kushape maoni na mwelekeo kila mtu asema lwake!? Ma CCM bana! majanga

Mkuu pitia msamiati unaitwa "mbugi", ukipata maana yake utakua umepata majibu ya bandiko lako hili, asante.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
CCM ni sawa na wale WAJENZI WA MNARA WA BABEL, kila kiongozi wa CCM sasa hivi anasema lake kuhusu UKAWA!
 
mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,394
2,000
CCM ni sawa na wale WAJENZI WA MNARA WA BABEL, kila kiongozi wa CCM sasa hivi anasema lake kuhusu UKAWA!

Sasa hivi CCM hawajui wanataka nini! Swali moja ambalo linasumbua sana kichwa changu ni: Kwa nini kama Kikwete aliona mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu hayafai na si maoni ya wananchi wengi yet akasaini kumaanisha kuipa uhalali kwamba hatua nyingine ifuate yaani bunge la katiba? Au alikubali kusaini rasimu shingo upande akijua kwambe wenzake CCM wataenda kuibadilisha tu kirahisi? Ndio maana alijaza makada kwenye lile kundi la 201? hivi hakuona kwamba rsimu yote imejengwa kwenye muundo wa serikali tatu na haiwezekani kuondoa msingi huo na rsimu ikabaki?

kwa mfano rasimu inapendekeza kila mkoa utoe mbunge mwanamke na mwanamme. je ukiweka muundo wa serikali mbili hili si litakuwa limeyeyuka kiaina? Je hawaoni hiyo katiba itakuwa kichekesho na mvurugano?

Kwa nini kikwete hakuishauri tume ya warioba iibadilishe rasimu iwe ya serikali mbili kabla ya kuisign? Au aliweka signature yake kwenye rasimu kabla ya kuisoma? Je haya maoni mapya ya serikali mbili yanatolewa kwa tume ipi ili iweze kuyatengeneza na kuyaingiza kwenye rasimu mpya? Kwa nini mheshimiwa rais umeamua kutuingiza kwenye mkorogano usiokuwa na sababu yoyote just kwa kukosa umakini na busara?

Je Bunge la katiba lina uwezo wa kubadilisha rasimu na kuja narasimu nyingine mpya? Bila kujali sheria inasemaje kuhusu hili ni kwamba swali hili linabaki kuwa la msingi na mpaka sasa halijajibiwa kikamilifu. Na kabla ya BMK kurejea august hili swali linatakiwa lijibiwe! mahakamani au popote kwa sababu litakata mzizi wa fitina.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom