Dr. Shein: Sitoteua Makamu wa Kwanza wa Rais toka Upinzani, hawakukidhi vigezo

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau amani iwe kwenu.

Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la 9 la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ifipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

HUU NDIO MSIMAMO WA RAIS WA ZANZIBAR, DR ALI MOHAMED SHEIN KUHUSU SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR.

Sote tunafahamu kwamba tarehe 20 Machi, 2016, tulikuwa na Uchaguzi Mkuu wa marudio ulioendeshwa na kusimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Sheria ya Uchaguzi Nambari 11 ya mwaka 1984. Madhumuni ya uchaguzi huo yalikuwa ni kuchaguliwa kwa viongozi wa vyama vya siasa wakataoingoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika Uchaguzi Mkuu huo wa Marudio wa tarehe 20 Machi, 2016 nafasi ya Rais iligombewa na vyama 14 vya siasa na hakukuwa na Chama chochote zaidi ya Chama cha Mapinduzi, kilichopata matokeo ya kura za Uchaguzi wa Rais kwa zaidi ya asilimia 10. Mimi nikiwa Mgombea wa Urais wa CCM, nilipata asilimia 91.4. Kadhalika, hakukuwa na Chama cha siasa zaidi ya CCM chenye wingi wa Viti vya Majimbo katika Baraza la Wawakilishi. Kwa kuzingatia msingi huo, na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, hakuna Chama cha siasa ambacho kinakidhi masharti ya kustahiki kutoa Makamo wa Kwanza wa Rais ili kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Huo ni uamuzi wa wananchi wa kukipa ushindi mkubwa Chama cha Mapinduzi na hawakutoa nafasi ya kumchagua Makamu wa Kwanza wa Rais. Huo ni uamuzi wao wa kidemokrasia. Kadhalika, uteuzi wa nafasi ya Makamo wa Pili wa Rais umewekewa masharti na kifungu cha 39(6), kuwa:-
(i) Atateuliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
(ii) Atoke katika chama anachotoka Rais. Uteuzi nilioufanya wa kumteua Makamu wa Pili wa Rais umekidhi matakwa ya kifungu cha 39(6) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984.

Nimelazimika nilieleze jambo hili la kikatiba, kwa sababu wapo waliodhani kuwa yupo Mgombea anayestahiki kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, lakini Rais amekataa kumteua na hivyo Katiba imekiukwa. Nililolifanya, la kumteua Balozi Seif Ali Iddi kuwa Makamo wa Pili wa Rais ni sahihi na ni kwa mujibu wa Katiba na nimechukua hatua ya kuunda Serikali kwa kuzingatia Katiba ya Zanzibar ya 1984.
 
Wadau amani iwe kwenu.

Akihutubia Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichooata wabunge wengi isipokuwa CCM.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kitakachopewa ridhaa ya kuwa sehemu ya serikali ya Umoja wa Kitaifa ifipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua wengine nje ya CCM. Amesema hayo ni maamuzi ya CCM. Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

CCM HOYEEEEEE.
ama kweli hayo ni maamuzi ya CCM kama ulivyoandika mstari wa nne kutoka chini, naona sasa unafikiria kuedit uandike hayo ni maamuzi ya wananchi teh! teh! ingawa tayari ushasema ukweli kwamba hayo ni maamuzi ya CCM
 
Wadau amani iwe kwenu.

Akihutubia Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichooata wabunge wengi isipokuwa CCM.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kitakachopewa ridhaa ya kuwa sehemu ya serikali ya Umoja wa Kitaifa ifipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua wengine nje ya CCM. Amesema hayo ni maamuzi ya CCM. Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.
 
Wadau amani iwe kwenu.

Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ifipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.

Maamuzi ya CCM
 
Majuto ni Mjukuu, mimi nafikiri Dkt Sheni labda Ameshauriwa vibaya, kwa Zanzibari ninayoijua! Nivyema Angeomba ushauri kwa mtangulizi wake. Mzee karume, maana Anajua Kwanini ilipelekea Zanzibar iwe na Vyama Mseto. Majuto ni Mjukuu.
 
ama kweli hayo ni maamuzi ya ccm kama ulivyoandika mstari wa nne kutoka chini, naona sasa unafikiria kuedit uandike hayo ni maamuzi ya wananchi teh! teh! ingawa tayari ushasema ukweli kwamba hayo ni maamuzi ya ccm

Mkuu umemuwah vizur huyu kijana wa lumumba ata edit sasa
 
Wadau amani iwe kwenu.

Akihutubia Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichooata wabunge wengi isipokuwa CCM.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kitakachopewa ridhaa ya kuwa sehemu ya serikali ya Umoja wa Kitaifa ifipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua wengine nje ya CCM. Amesema hayo ni maamuzi ya CCM. Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi.
Safi sana,ndo walichokitaka CUF....wamekwisha na kuzikwa rasmi.
 
Back
Top Bottom