Siku 9 tu baada ya UKAWA kutoka bungeni,CCM walibadilisha baadhi ya kanuni muhumu:

masanjasb

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
2,364
864
Wana body nimatumaini yangu nyote mko salama?

Kuna jambo moja la muhimu sana ambalo viongozi wetu hasa wa Tanzania One(ccm) hawaliongelee kabisa nalo ni;

Mnamo tarehe 16/04/2014 Umoja wa katiba ya wananchi walitoka bungeni na tarehe 25/04/2014 yani siku 9 tu baada ya ukawa kutoka njebya bunge la katiba ccm walibadilisha kanuni za bunge la katiba ili kuhalalisha uvunjaji wa moyo wa katiba ambao ni serikali 3

Kanuni moja wapo mpya iliyoingizwa baada ya ukawa kutoka ndani ya bunge la katiba ni kanuni ya 32,6

Kifungu hiki Kinasema hivi: "bila yakuadhiri utaratibu wa majadiliano ya sura ya kwanza naya sita,mjumbe yoyote au kundi lolote la wajumbe lilotajwa chini ya kufungu cha 22,1 cha sheria ya mabadiliko ya katiba linaweza kupendekeza sura mpya kwenye rasimu ya katiba"

Ndugu zangu hiki kifungu ni kipya na sasa ccm wanauwezo wa kuondoa sura ya 6 inayohusu muundo wa muungano wa serikali 3 na kuweka wa serikali 2 na haya yote yamefanyika kimya kimya na bila ukawa kuwepo ndani,sasa nia ya dhati ya hawa jamaa iko wapi?

Na kama wanawataka Ukawa warejee bungeni wakajadili nini? Wakati UTI au MOYO wa katiba hauna uhai tena

Wanawataka ukawa wakabariki hayo mabadiliko ya kanuni ya 32,6?

Tukiwa tunafakali uchakachuaji wa kanuni hizi pia leo tujitahidi kuweka macho na masikio yetu katika luninga yetu ya ITV ambapo kutakuwa na mjadala mkali utakaowashirikisha wajumbe wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba chini ya gwiji wa sheria na mwanasiasa wa enzi na enzi, jaji sinde warioba ili tujifunze mengi zaidi kuhusiana na mchakato huu mkubwa na muhimu kwa Taifa letu
 
CCM inaelekea either wameamua kujivua ufahamu au hawaelewi kinachoendelea. Wanaiangalia nchi ya 2015 wakati TZ itakuwepo zaidi ya miaka elfu.
 
ccm wahuni sana hawa ni hukumu yao ni kwenye kura tuu

Kwenye kura nako watatumia uhuni wao ule ule wa miaka nenda rudi.....swala la muhimu kama hili bado wanapenyeza rupia ili wapewe support?

swala la katiba wanasomba watoto wa buguruni ili kumzomea mtu yoyote akayesema neno serikali3 kwenye mdaharo wa jana Nkuruma hall?

Ni issue ipi ccm wakayoiona kama ya Kitaifa zaidi ya maonyesho ya nanenane?
 
CCM inaelekea either wameamua kujivua ufahamu au hawaelewi kinachoendelea. Wanaiangalia nchi ya 2015 wakati TZ itakuwepo zaidi ya miaka elfu.

Binadamu huwa tunajifunza kutokana na makosa ila kwa upande wa ccm wa roho ya paka,fikiria mtu aliesaidia kuandika katiba yao ya 1977 na bado ikawa na makosa leo anapochukua jukumu la kerekebisha makosa hayo anaoneka ni mwandawazimu,cjui wanataka mzee wa watu afe ndiyo waje waanza kumlaumu kama ilivyotokea kwa baba wa Taifa?

Ngoja tuone wanakolipeleka Taifa hili
 
Wao walisusa. CCM wamekula. Wewe inakuuma nini?

Nchi hii c ya maccm peke yanu,ni nchi ya watu wote ila kwa vile mnatengeneza katiba ya ccm mie wala hainiumi at all ni haki yenu ya msingi kabisa

Kwanza katiba ya chama mnayo, style yenu ya kuvaa koti la muungano ndiyo hyo hyo mliyokuwa mkiitumia kwenye katiba ya 1977 kwani katiba hyo ilikuwa ya mfumo wa chama kimoja na leo tunataka tengeneza katiba ya Tanzania nyie bado mwataka tundelee na katiba ya ccm,hakuna anaekubali kubariki ujinga huo,nendeni mkapitishe katiba yenu wenyewe
 
wenzetu kama kuna mnachopata toka plaza tujulisheni pls huku kwetu radio one na itv vimekatwa!
 
wenzetu kama kuna mnachopata toka plaza tujulisheni pls huku kwetu radio one na itv vimekatwa!

Mkuu mbona radio one wako hewani,jiachie upate elimu nzr toka kwa wataalamu wa rasimu ya katiba mpya,na kama ulimiss zile hotuba za mwalimu bs leo zinapatikana live
 
Back
Top Bottom