Mwenyekiti wa NLD na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Dr. Emmanuel Makaidi azikwa makaburi ya Sinza

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mwenyekiti wa NLD na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Dr. Emmanuel Makaidi azikwa kwenye makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam leo. Viongozi mbalimbali wa Serikali na vyama vya siasa wamehudhuria mazishi yake.
makaidi.jpg
5.jpg
1.jpg
mk1.jpg mk.jpg
3.jpg
Mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa taifa wa chama cha siasa cha National League for Democrasy-NLD- na mwenyekiti mwenza wa umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- Daktari Emmanuel Makaidi umeagwa leo katika viwanja vya Karimjee na kuzikwa katika makaburi ya Sinza jiji Dar es Salaam.

Katika ibada fupi ya kuuga mwili wa marehemu Daktari Emmanuel Makaidi iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.Bw. Edward Lowassa, wazii mkuu mstaafu Fredrick Sumaye na makamu mwenyekiti wa CCM Bwana Philip Mangula, mchungaji wa kanisa TAG makumbusho Bwaba Davd Mwakwenda amewataka wanasiasa kuhacha kuombeana mabaya na kutakiana amani ili kuwa na taifa lenye baraka.

Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi ameiomba jamii kuhacha kuhusisha matukio ya vifo yanayoendele kujitokeza na harakati za kisiasa na kuwataka wanasiasa kutambua swala la amani ni la msingi hivyo taifa likiingia katika uchaguzi mkuu kwa amani litakuwa limemuenzi marehemu Daktari Emmanuel Makaidi.

Akiongea kwa niaba ya umoja wa katiba ya wananchi Bwana James Mbatia amesema umoja huo umepata pengo kubwa kutokana na kifo cha mwenyekiti mwenza marehemu Dkt Makaidi kwa kuwa imekuwa ikituma taaluma yake ya sayansi ya siasa katika mipango yao, huku mwenyekiti wa Chadema Bwana Freeman Mbowe akivita vyombo kisheria na mamlaka za kiserikali kutotumia nguvu ili kwezesha uchaguzi kuwa huru na amani kama njia ya kumuenzi marehemu Dkt Emmanuel Makaidi.
 

Attachments

  • 4.jpg
    4.jpg
    17.9 KB · Views: 3,216
Last edited by a moderator:
Mwili wa mpambanaji shujaa na mwenyekiti wa Ukawa na NLD hayati Dr Emmanuel Makaidi wapumzishwa leo jijini Dsm. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi wote wa Ukawa akiwemo mgombea mwenye mvuto kuliko wote Edward Ngoyai Lowassa na mgombea mwenza Babu Duni
 

Attachments

  • 1445356556245.jpg
    1445356556245.jpg
    16.5 KB · Views: 854
  • 1445356564995.jpg
    1445356564995.jpg
    25.4 KB · Views: 791
  • 1445356577581.jpg
    1445356577581.jpg
    23.6 KB · Views: 794
  • 1445356587331.jpg
    1445356587331.jpg
    24.7 KB · Views: 779
  • 1445356606642.jpg
    1445356606642.jpg
    20.6 KB · Views: 778
Msanii huwazika wasanii wenzake.
R.I.P Mzee wetu tulikupenda na hatutakuangusha tar. 25 kwa kile ulichokuwa unakiamini.
 
Back
Top Bottom