Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020

Sawa tu ,nimeshasema nimeota hakuna uchaguzi mwaka huu .Tuiombee Tz sana yajayo sio mazuri ila Mungu ni mwema.
 
Uchaguzi Mkuu uheshimiwe, Vyama vya siasa vifanye chaguzi zao na wananchi waachwe waamue wenyewe viongozi wanao wataka, Watanzania wanaakili timamu na hii nchi ni ya watanzania wote. Waliopewa dhamana watimize majukumu yao tusileteane mbwembwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu muhaya kwisha habari yake.mbinu za kuamrisha watendaji kata kutopokea fomu za wapinzani
 
Watu hawana aibu. Hata remorse hawana.
Unafanya upuuzi wa kishamba kama ule halafu unasema kwenye uchaguzi mkuu utatumia mbinu zilezile. Kwa hiyo uchaguzi mkuu hautakuwepo!
Yaani unawambia watendaji wakimbie ofisi mpaka wengine walianguka na kuteguka miguu, fomu kukataliwa na nyingine kutupwa kupitia madirishani. Mwisho wa siku unajivunia 'ushindi' wa 99.9%
Aibu sana.
 
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 CCM itatumia mbinu, mikakati na ubunifu ule ule uliotumika kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dr Bashiru amesisitiza kuwa yeyote atakayejipendekeza kugombea udiwani, uwakilishi, ubunge au urais kupitia Upinzani atakuwa ni halali ya CCM kwani KUSHINDWA ni demokrasia pia.

Dr Bashiru amesema hayo akiwa ziarani wilayani Korogwe mkoani Tanga

Source: Star Tv Habari

My take: Mnyika na Chadema watapata wakati mgumu sana mwaka huu. Chadema bila mbunge itaandikwa historia mpya.

Maendeleo hayana vyama!
He can't be serious. Yaani mbinu za kihuni zilezile zitumike tena ktk uchafuzi mwingine. Historia itamweka ktk rekodi zake, yaani yule mhadhiri maarufu ktk masuala ya taaluma aliyekuwa amejaa hoja na tafakuri za kina kupitia "theoretical critical thinking" ila sasa ktk vitendo kageuka kuwa kioja na muflisi wa hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom