Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020

Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 CCM itatumia mbinu, mikakati na ubunifu ule ule uliotumika kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dr Bashiru amesisitiza kuwa yeyote atakayejipendekeza kugombea udiwani, uwakilishi, ubunge au urais kupitia Upinzani atakuwa ni halali ya CCM kwani KUSHINDWA ni demokrasia pia.

Dr Bashiru amesema hayo akiwa ziarani wilayani Korogwe mkoani Tanga

Source: Star Tv Habari

My take: Mnyika na Chadema watapata wakati mgumu sana mwaka huu. Chadema bila mbunge itaandikwa historia mpya.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani tatizo liko wapi Chadema wakose au wapate wabunge. Maadamu MABADILIKO yapo ndani ya mioyo ya watanzania yatafanyika tu. Uwizi wa kura kwa kutumia polisi jeshi wala haitasaidia ila tunasubiri hiyo siku kwasababu nyie ndio wale wale bendera fuata upepo
 
nashauri viongozi wasome alama za nyakati. watanzania sio wajinga kiasi hicho. hakuna mtu mbaya kwenye maamuzi kama mtu mkimya! time will tell!
 
Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kuwa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 2020 CCM itatumia mbinu, mikakati na ubunifu ule ule uliotumika kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dr Bashiru amesisitiza kuwa yeyote atakayejipendekeza kugombea udiwani, uwakilishi, ubunge au urais kupitia Upinzani atakuwa ni halali ya CCM kwani KUSHINDWA ni demokrasia pia.

Dr Bashiru amesema hayo akiwa ziarani wilayani Korogwe mkoani Tanga

Source: Star Tv Habari

My take: Mnyika na Chadema watapata wakati mgumu sana mwaka huu. Chadema bila mbunge itaandikwa historia mpya.

Maendeleo hayana vyama!
Na kweli mkuu kuwakimbia wagombea wa upinzani,kuedit fomu zao na kujipitisha bila kupingwa sawa kabisa ccm oyeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
johnthebaptist,
Huyo Katibu Mkuu Dkt Bashiru anaongea hayo hata aibu hana?

Hivi atawezaje kujivunia huo ushindi wa asilimia 99 wa uchaguzi wa serikali za mitaa, wakati hata mtoto mdogo anayesoma chekechea anajua kuwa nyinyi masisiem mlifanya wizi mkubwa sana katika huo mnaouita uchaguzi wa serkali za mitaa?

Anaitumbukiza nchi katika machafuko aache kabisa ujinga huo
 
Hata wapate 100%, mafuriko ya Dar yako palepale,barabara za Korogwe zitabaki vilevile,na umaskini utabaki palepale
 
Back
Top Bottom