Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Jun 14, 2012.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Na Mwandishi Maalumu

  NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro amemaliza jukumu lake rasmi katika Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.Kwa hatua hiyo, mashirika ya UN yanayohusika na masuala ya Idadi ya Watu (UNFPA), Ukimwi (Unaids) na Mpango wa Kupambana na Malaria (RBM) Jumanne yaliandaa tafrija ya kumshukuru na kumuaga.Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, akifuatana na mkewe na wadau mbalimbali akiwamo Ofisa Mtendaji Mkuu wa UNDP, Helen Clark, mabalozi wanaowakilisha nchi zao UN, sekta binafsi na taasisi za kiraia, ilifanyika makao makuu ya UN.

  Akizungumza kwenye tafrija hiyo, Ban alielezea baadhi ya sababu zilizomsukuma kumteua Dk Migiro kuwa msaidizi wake wa karibu."Nilimfahamu Migiro wakati huo sote tukiwa mawaziri wa mambo ya nje katika nchi zetu."Uwezo wake na uelewa wake wa mambo ulinivutia sana, lakini nilivutiwa zaidi pale nilipofahamu kwamba alipata kuwa waziri wa masuala ya wanawake na watoto. Nikajiridhisha kwamba huyu ndiye atafaa kuwa msaidizi wangu wa karibu," alisema Ban na kushangiliwa.Kama haitoshi, Ban alimwelezea Dk Migiro kama msaidizi wake wa karibu ambaye licha ya kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, ni mtu asiye na makuu na hata siku moja hakujikweza."Katika kipindi chote ambacho Migiro amekuwa msaidizi wangu wa karibu, amenisaidia katika mambo mengi, ni mtu mwadilifu sana, ni mtu aliye karibu sana na watu, aliyeamsha matumaini na kuwapa tabasamu waliokuwa katika mazingira magumu. Daima amekuwa mstari wa mbele kunisaidia na hakuna hata siku moja alipojikweza.Na kwa sababu hii, anastahili tafrija hii," alisisitiza Ban. Aidha, Ban alimwelezea Migiro kama kiongozi ambaye daima alitoa kipaumbele cha aina yake katika masuala ya afya ya jamii, eneo alilotumia uwezo wake wote, maarifa yake yote kama Naibu Katibu Mkuu kupigania afya ya wanawake na watoto na watu wote walio katika mazingira magumu.

  Kwa upande wao, waandaaji wa tafrija hiyo na wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemwelezea Naibu Katibu Mkuu, kama kiongozi ambaye mchango wake umesaidia kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kuweka mkazo wa aina yake katika kushughulikia afya ya jamii. Michel Sidibe, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS alimwelezea Migiro kama dada yake ambaye sifa zake zinaanzia mbali."Migiro ni dada yangu, ni dada ambaye ana sifa za kipekee, ni mwanamke wa kwanza aliyefaulu daraja la kwanza katika Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania na mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN," alisema kauli iliyoamsha tena makofi kutoka kwa wageni waalikwa.

  Sidibe alimwelezea Migiro kama kiongozi aliyefanya kazi kwa karibu na shirika lake katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Ukimwi yanapungua, ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa tiba ya uhakika kwa waathirika."Tuna kila sababu leo hii kumshukuru kwa namna alivyoshirikiana nasi, na ingawa unaondoka, lakini tambua kwamba mchango wako utaendelea kukumbukwa na kuenziwa," alisisitiza Sidibe.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, Dk Babatunde Osotimehin alisema juhudi kubwa zilizooneshwa na Naibu Katibu Mkuu katika kushughulikia masuala ya afya ya jamii, zilipunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi, hali kadhalika vya watoto wachanga wa chini ya umri wa miaka mitano."Katika kipindi cha uongozi wako, umefanikisha kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada na kutoa kupaumbele katika afya ya mama na mtoto, tunakushukuru sana kwa hili na Mungu aendelee kukubariki," alisema Dk Osotimehin.

  Herve Verhoosel, Mwakilishi wa Mpango wa Kupunguza Malaria, alimwelezea Dk Migiro kwamba chini ya uongozi wa Ban, alijenga misingi bora ya ushirikiano na mwamko miongoni mwa wadau katika kuhakikisha unakuwapo uhusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kutimiza malengo ya afya ya jamii, ikiwa ni pamoja na kasi ya kupunguza malaria.

  Akishukuru waandaaji wa tafrija hiyo, Dk Migiro alimshukuru Ban kwa kumwamini kuwa msaidizi wake wa karibu kwa miaka mitano na nusu. Alisema ingawa alijituma kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, alifanya hivyo kwa kuwa Ban alimwamini kwamba anaweza. Na kwamba daima ataendelea kuienzi heshima hiyo.Alitumia fursa hiyo kumwelezea Ban kama kiongozi ambaye yuko mstari wa mbele kuhakikisha kila mtoto angalau analala kwenye chandarua na wajawazito hawapotezi maisha kutokana na uzazi.Migiro alishukuru kwa moyo wa dhati wasaidizi wake wa karibu aliofanya nao kazi akiwa Naibu Katibu Mkuu na kwamba bila wao asingefika alipo, alishukuru pia wadau wakiwamo mabalozi kwa ushirikiano wa hali na mali waliompa muda wote wa uongozi wake.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa na Dkt Asha-Rose Migiro katika hafla ya kumuaga rasmi iliyofanyika leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
  [​IMG]
  Dkt Asha-Rose Migiro akiongea katika hafla hiyo ya kumuaga rasmi
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiongea katika hafla hiyo
  [​IMG]
  Dkt Asha-Rose Migiro baada ya kupokea zawadi ya maua katika hafla hiyo ya kumuaga rasmi
  [​IMG]
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Hale penshen sasa asilete uroho wa madaraka tanzania maana magamba hawaridhiki hasa hawa sampuli za batrida,
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Umoja wa mataifa ulimpenda sana ila Watanzania wanampenda zaidi arudi nyumbani
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jk atamteua kuwa mbunge
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Je, ameacha jina zuri la Tanzania kuhusu wajibikaji au ameacha tu jila historia kwamba Tanzania ilikuwa na Naibu katibu mkuu umoja wa mataifa?
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Lazima iwe hivyo kwani mkweree hamna koo anazoziona hapa nchini isipokuwa zawakina Asha Rose na Mwanaidi Sinare!! Ndio maana hata dada zao wanakomba teuzi kubwa kubwa za mkweree!! Hongereni wakina mama.
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Akirudi vp ataanza kujipanga kwa ajiri ya urais au atapewa uwaziri?
   
 8. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Kuna mama mmoja juzi juzi ametoka UN amewepwa wizara ya mazingira, sasa huyu nae si vibaya akapewa wizara ,
   
 9. m

  mamajack JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  yule mama anamipango mingi utekelezaji zero kabisaaaaaaaaa,nadhani hata huyu sina niwalewale.magamba hawana product ya kujivunia.
   
 10. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  kama wapemba vile!!kazi kwelikweli
   
 11. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  karibu nyumban,karibu dada asha,rose sahaban mtengeti migiro,,,kazi umeifanya na heshima umeijenga,,,,,,come back home with comfidence,,,,mungu aliyekufikisha huko usimuache,,,,watumikie wa tz,,tuna tatizo la uongozi,,,tumekosa mtu anayeheshimiwa na jamii katika watawala wetu,,,nasema watawala kwakua hatuna kiongozi,,,tumekosa dira na mwelekeo kama taifa,,,,,,,tunaongozwa na matukio,,chama chako kinahenyeshwa kwata na umma unaohitaji mabadiliko,,,chenyewe kinasaka wachawi badala ya kuleta mabadiliko,,,,,,kinasubiri kilazimishwe,,,,,njoo upesi ,,,njoo usikawie,,,,njoo na mbadala njoo tofauti,,,njoo uwaone wa tz masikini wasio na matumaini tena,,kila siku heri ya jana,,,,,ukifika jipange,,,usake urais ili 2015,,ushindan ndan ya chama chako uwe mgumu,,na uchaguzi uwe mgumu ,kuupata urais kuwe kugumu,,huenda wapiga kura wakaheshimiwa,,,,,njoo,,ulete changamoto,,,haiwezekani wenzetu wanafuta umasikin ,,na kuboresha maisha cc tungali tunakoroma usingizi,,,,udiniiii,,udiniiii,,uamshoooo,,muunganoooo,,nyambafu kabisa,,huku nchi ikiporwa kila uchao na huduma za jamii zikiporomoka,,,,nan anajali,,,,,hapa nalia,,nalia kwakua najiuliza nani ametuloga,,,,ajira hamna,,maadili kwisha,,hata ule umoja wetu kama taifa unasambaratishwa na hoja za udini na ukanda,wallonacho na wasionacho,,,, mungu atusaidie,
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kifaa hicho kinarudi, magwanda ya khaki kaeni chonjo.
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,839
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Anarudi na kukuta chama chake kinanuka kinyesi cha Nyani watanganyika wamekihama.
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,740
  Trophy Points: 280
  Atakuwa mbunge.
   
 15. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  candid Zama hizi historia hamtambii mtu ambaye hakuwa na mchango chanya kwa taifa/jamii yake.Yeye kuwa makamu katibu mkuu wa UN amechangia nini kwenye maendeleo na ustawi wa wanajuia wa UN, tz ikiwemo?.Achalia mbali na utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ,Je amefanya nini ambacho wenzake hawakufanya chenye manufaa kwa jumuiya ya kimataifa? .
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hiko alikotoka kachemsha, asipewe chochote apishe na wengine wajaribu, sio kila siku watu hao hao, hizo ndo fikra potofu za CCM mnaziendeleza
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  zomba, huyu mama amefanya nini cha maana wakati akiwa UN?
   
 18. u

  umumura Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  hana lolote, ndo welewale, itakuwa na maana akafundishe watoto udom
   
 19. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Ban Ki moon nomaa...kamtimua..halaf kila nikimuangali huyu mama inaonekana anapenda sana misifa..we mtazame gustures
   
 20. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  karibu nyumbani!
   
Loading...