Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

Napendekeza mama Migiro arudi Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuendelea na kazi yake ya uhadhiri.Tasnia ya elimu ya sheria bado inamhitaji
 
candid Zama hizi historia hamtambii mtu ambaye hakuwa na mchango chanya kwa taifa/jamii yake.Yeye kuwa makamu katibu mkuu wa UN amechangia nini kwenye maendeleo na ustawi wa wanajuia wa UN, tz ikiwemo?.Achalia mbali na utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ,Je amefanya nini ambacho wenzake hawakufanya chenye manufaa kwa jumuiya ya kimataifa? .

Je ameacha jina zuri la kutangazwa watanzaia tu viongozi wazuri wa kukabidhiwa majukumu kimatifa ndicho ninachoongelea. Mfano Anam
 
Je ameacha jina zuri la kutangazwa watanzaia tu viongozi wazuri wa kukabidhiwa majukumu kimatifa ndicho ninachoongelea. Mfano Anam
candid Kwa maoni yangu yule mama ni Incompetent ndio maana hakuongezewa muda kuendelea na kazi yake,so hawezi tuachia jina zuri kwa jamii ya kimataifa ,hata Mama Tibaijuka aliondolewa UN-HABITAT kiujanja kwa Scandal.
 
Last edited by a moderator:
Mama karibu nyumbani wewe ni moja ya majembe tunayoyategemea ...... tunakutakia safari njema ya kurudi Tanzania.

Ujuzi uliopata ulete nyumbani si haba kuwa mwanamke wa kwanza duniani kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) asilani dunia haijawahi kupata katibu mkuu mwanamke wa UN kwa ngazi uliofikia umekuwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo cha juu zaidi UN.
 
Kuna mama mmoja juzi juzi ametoka UN amewepwa wizara ya mazingira, sasa huyu nae si vibaya akapewa wizara ,

Anna Tibaijuka amepewa wizara ya Ardhi; aliporudi alikuwa na moto sana lakini kumbe ilikuwa nguvu ya soda!! Kero zote anazopelekewa anazipeleka kwa wasaidizi wake nao wanapeleka kwa wasaidizi wao na hao wasaidizi nao wanapeleka kwa wasaidizi wao as a result mlolongo unakuwa mrefu usioisha na kunakuwa hakuna action yeyote inayochukuliwa; na kwa vile sio mfuatiliaji hakuna kero zozote zinazotatuliwa na yeye amekuwa rendered ineffective!!
 
Jk atamteua kuwa mbunge

Mama anasitahili kuteuliwa kuwa mbunge sifa anazo.......haya si majembe ya kuyaacha kuwa butu ni muhimu akaenda bungeni kulima.


Mambo ya nje ampatie mama huyu Benard Membe hatoshi
 
Kuna mtu alihoji, "UN amefanya jambo gani ambalo anaweza kulisema mbele ya Watanzania kama mtaji zaidi ya kuwakilisha?"
 
Mtu yeyote hata kama msafi akiwa ndani ya CCM na nchafu tu... Maana atakuwa anashiriki kulinda maovu na wezi wa rasilimali za kitanzania... Safari hatutaki Rais mwenye kaharufu ka mambo ya nje, tunataka Rais ambaye atakuwa anaumiza kicha kwa ajili ya Tanzania na watanzania..

Siyo Rais ambaye katika miaka mitano mwaka mmoja yoko angani au nchi za nje.
 
Niliposikia kuwa iyo post ilikuwa ya Mwandosya ila fitna za JK ndo akampa huyu mama no wonder UN wakaona hana haja ya kuextend tenure yake.
Ila imekula kwake maana JK alikuwa akimsubiri uyu mama ampe uwaziri!
Ila JK na akina mama damu damu anaweza mpa ata ukurugenzi
 
Huyu mama kawa mzee ghafla au ni macho yangu ? IMG_4509.JPG
 
candid Kwa maoni yangu yule mama ni Incompetent ndio maana hakuongezewa muda kuendelea na kazi yake,so hawezi tuachia jina zuri kwa jamii ya kimataifa ,hata Mama Tibaijuka aliondolewa UN-HABITAT kiujanja kwa Scandal.

Naona vigezo vya kuchekacheka ndivyo vilivyowapeleka huko vinginevyo kuna ambao wangeondoka na majina mazuri tu.
 
Pale Slaa pangemfaa sana, lakini kigezo kimoja ni lugha za kimataifa zaidi ya nne, sasa sijui Slaa anazo ngapi baada ya Kimbulu? Labda Kiarabu maana si Muiraq?
 
Pale Slaa pangemfaa sana, lakini kigezo kimoja ni lugha za kimataifa zaidi ya nne, sasa sijui Slaa anazo ngapi baada ya Kimbulu? Labda Kiarabu maana si Muiraq?
Hapo hapahitaji mtu aliyehifadhi juzuu? Au kuhesabu zile shanga njiani?
 
Back
Top Bottom