Dr. Angella Mabula (The Lady) atoa somo zito

Dr. Angella Mabula (The Lady) atoa somo zito

Naibu waziri wa makazi na mbunge wa Ilemela katoa somo zito la kukabiliana na msongamano Mwanza. Kasema ili kukabiliana na msongamano wa magari, Barabara ya Airport Igombe kayenze Sangabuye Kongolo hadi Magu inapaswa kuwekwa lami, Ili abiria wanaoshuka na ndege waendao Magu Lamadi Bunda hadi Musoma hawatahitaji kupita mjini kati.

Barabara ya Ilemela Kiseke hadi Buswelu nayo inapaswa kuwekewa lami, hii itasaidia watu watokao Ilemela na Airport kwenda Buswelu na Igoma haitawalazimu kwenda mjini kati, kwa kweli huyu mama anaona mbali sana, sasa tunaomba wakuu hebu wayafanyieni kazi mawazo ya huyu mbunge wetu.

Pia, Kasema serikali inapaswa kuharakisha kukamilisha uwanja wa mwanza ili uwe International, watalii sasa wapitie Mwanza badala ya KIA kwani kutoka mwanza hadi serengeti ni km 160 tu wakati kutoka KIA hadi serengeti ni 360km, hii itawapunguzia sana gharama watalii na kuwafanya kutopoteza muda mwingi barabarani. Hongera sana.

Na Mlima Kilimanjaro pamoja na Ngorongoro Creator wazihamishie Mwanza basi ili Dream zake zitimie.
 
Mama mabula uko vizur sana kiwia na wenje walitupotezea mda sana lakin nashukuru sasa tuna wabunge hodari sana asante angelina kwa wazo zur
 
Huyu mama Professionally nadhani ni Mhasibu. Kuwa Naibu waziri wa Ardhi na Makazi ni Ubakaji wa Ajira za watu bure.

Kwanza mawazo yake hapo yapo Kijimbo zaidi tu (Ilemela) si Kimji wa Mwz mzima. Huto tudege tuwili tuna abiria gani wa kuweka Jam Mwz? Ni wa Watanzania wangapi hupanda ndege hadi kuweka Jam? Acheni utoto!!!

Jiji la Mwz ni la hovyo ktk kupangwa!!! Viwanja havijapimwa karibia 70% ya mji wote. Milimani uoto wa asili unaondoka kwa uvamizi huku maliasili na mipango miji wakitizama tu. No toilets ; No water to those areas!!
Kwa nafasi yake kwa kushirikiana na Waziri Mchapa kazi (Lukuvi) Mwz lingekuwa Jiji bora baadae. Tutambue kuwa hapa ndio Rais hutua na kulala na hata kamazi yake nadhani yapo hapa. Boresheni heshima ya Jiji la pili.

Mwanza itakuwa na Jam, Dar cha mtoto.
Kuna barabara kuu Kisesa-Mjini-Usagara ina paswa kuwa njia 6 au Zaidi. Ndio main road pekee kwa mwz.

Barabara ya Mkuyuni-Nyakurunduma- Buzuruga ijengwe kwa lami. Mkuyuni -Kanyerere -Igoma iwekewe Lami.

Barabara ya Buhongwa-Igoma iwekewe lami.
Barabara ya Pepsi-Bugando-Town ipanuliwe.

Barabara ya town -Rick CityMall (Ghana) ipanuliwe iwe njia 6.

Barabara ya Town - Kisesa ipanuliwe iwe njia 6.

Ma afisa ardhi na Mipango miji wa Jiji la mwz wahamishwe wote, wamegeuka madalali na wapiga hela tu hapa mjini.

Umesahau ile ya Usagara-Kisesa iwekwe lami, ile ya Airport-Igombe-kayenze-bujashi nayo
 
Mwanza inahitaji bara bara za kutosha kukabili msongamano wa magar. Naunga mkono wadau waliotangulia kuzitaja barabara muhimu zinazounganisha jiji na mitaa yake. Mi naongezea barabra nyingine ni butimba sweya hadi luchelele ikaungane na barabara ya nyegezi malimbe. Buhongwa_mahina hadi igoma iungane na barabara ya mkuyuni nyakulunduma mahina. Hi zote zikijengwa kwa kiwango cha lami nafikiri zitasaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza msongamano wa magari.
 
Naibu waziri wa makazi na mbunge wa Ilemela katoa somo zito la kukabiliana na msongamano Mwanza. Kasema ili kukabiliana na msongamano wa magari, Barabara ya Airport Igombe kayenze Sangabuye Kongolo hadi Magu inapaswa kuwekwa lami, Ili abiria wanaoshuka na ndege waendao Magu Lamadi Bunda hadi Musoma hawatahitaji kupita mjini kati.

Barabara ya Ilemela Kiseke hadi Buswelu nayo inapaswa kuwekewa lami, hii itasaidia watu watokao Ilemela na Airport kwenda Buswelu na Igoma haitawalazimu kwenda mjini kati, kwa kweli huyu mama anaona mbali sana, sasa tunaomba wakuu hebu wayafanyieni kazi mawazo ya huyu mbunge wetu.

Pia, Kasema serikali inapaswa kuharakisha kukamilisha uwanja wa mwanza ili uwe International, watalii sasa wapitie Mwanza badala ya KIA kwani kutoka mwanza hadi serengeti ni km 160 tu wakati kutoka KIA hadi serengeti ni 360km, hii itawapunguzia sana gharama watalii na kuwafanya kutopoteza muda mwingi barabarani. Hongera sana.
Hizo kilomita za KIA hadi Serengeti zimekosewa.
 
Mwanza inahitaji bara bara za kutosha kukabili msongamano wa magar. Naunga mkono wadau waliotangulia kuzitaja barabara muhimu zinazounganisha jiji na mitaa yake. Mi naongezea barabra nyingine ni butimba sweya hadi luchelele ikaungane na barabara ya nyegezi malimbe. Buhongwa_mahina hadi igoma iungane na barabara ya mkuyuni nyakulunduma mahina. Hi zote zikijengwa kwa kiwango cha lami nafikiri zitasaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza msongamano wa magari.

Ishort wafuate masterplan ya mwanza 2015~2035
 
Kutoka city centre mpaka Kisesa barabara ipanuliwe iwe njia sita. Kisesa-Usagara ikamilishwe itapunguza msongamano wa magari makubwa na madogo yanayotoka barabara ya Musoma.
 
National Housing wanakamuliwa kwelikweli,kabakiza kuwapa kadi za mchango wa harusi tu,ni kama hilo shirika lina ubia na jimbo
 
Back
Top Bottom