DPP: Ni kosa kuwarejeshea fedha waliowekeza QNET

DPP: Ni kosa kuwarejeshea fedha waliowekeza QNET

Msomi wetu asitoe uamuzi wa jumla kama huu. Ndio hiyo biashara ni haramu, je muathirika alijua hilo? Kama qnet imerejesha hizo pesa, kwa nini muathirika asirudishiwe pesa zake? Anayepaswa kupewa adhabu ni qnet na sio aliyetapeliwa. Kufanya kinyume ni wizi kwa upande wa serikali inayotaka kukomba pesa za kila mtu na isiyotosheka.
Ulichoandika umekielewa lakini! Au huelewi hata kilichomezani
 
Sijui kwanini serikali uwa hairejeshi pesa kwa wenye nazo, hata za DECI iipita nazo, na za mr kuku naona zinapelekwa BOT na za Qnet itakuwa hivyo hivyo. Kama wanataka kusolve tatizo wafuatilie na kufunga zote kufunga Qnet tu hawajasove jambo. Zipo nyingi kuna moja inaitwa phyto science mwaka juzi walimpiga jamaa yangu milion 15, na zipo nyingine nyingi tu.

Eti wanajifanya wanauza madawa wameunga unga vipicha eti Obama anaunga mkono kampuni hiyo, mara kikwete wanaonyesha watu picha uongo mwingi. Kujiunga ndo hivyo milioni 3 sijui uunge watu wengine 5 then hata usipofanya kazi unapokea dollar 3000 kila mwezi. Jamaa yangu akaona isiwe tabu akaunga ndugu kwa kuwalipia wewe, hizo dola 3000 alizisoma tu kwenye makaratasi na hiyo pesa aliyoweka alirudishiwa dollar 200 tu.
😁😁 Niliwahi kumtembelea dada yangu binamu Mmoja hivi akaanza kunipa story Kama hizi sijui kapata kampuni gani inayo Fanana na Bitcoin so wanasemina inafanyika kempisky so anakwenda next weekend mwenyewe alikuwa anadai kwamba huo mchongo ukitiki tu anakuwa mult millionaire Mimi nikawa na msikiliza tu huku kimoyo moyo na muambia Ndugu tayari umeshapatwa na bwana Pepsi ndio unakwenda kulizwa hivyo ...

Yaani jinsi alivyokuwa anaamini kuhusu huo Mchongo unadhani mlokole vile anavyoamini masuala ya ufufuo na uzima ..Mimi sikutaka kumshtua niliachana nae ageuzwe mjinga ndio wali wao
 
😁😁😁😁
Tapeli wa ukweli ni yule anaeacha tapeli wa uwongo akusanye hela nyingi kutoka kwa wanyonge hadi zifike billions then anaenda kuzikomba zote kutoka kwa tapeli wa uwongo na kuzihamishia BOT bila ya kuwarudishia wanyonge hela zao.
 
Halafu yule waziri aliyetmbuliwa mkopa pikipiki ndie waliyetumia mgongo wake kuaminisha umma. Good morning milionea kidogo tu niwape michango ya harusi yangu waniuzie saa milioni 5 nashukuru Mungu ni mwema.
😁😁
 
Panda ili uvune maradufu ni kauli ya kitapeli inayotumiwa na matapeli wengi wa upatu!

Lakini tujiulize; inawezekanaje nchi ilivyojaa usalama wa taifa kuanzia uchochoroni hadi Bank wasimjue mchezesha upatu kuwa ni tapeli!

Mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano tapeli anafanya miamala kimyaa!

Tapeli anasambaa kijiji, kitongoji, wilaya, mkoa hadi taifa kimyaaa!

Hadi mwalimu mmoja anapolalamika ndipo tunajua huyu mcheza upatu ni tapeli. Katapeli bilioni 17, hilo ni kosa!

Tapeli anahukumiwa faini ni million 5 kama hana jela itamhusu!

Halafu akaunti na mzigo wote wa 15 bilioni UNATAIFISHWA! (Ni kosa kuwarudishia waliotapeliwa)

Tapeli tunamwachia aende zake (Case closed)

Mimi niliyeishia darasa la saba nisaidieni kumtambua Tapeli ni yupi!



=========

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Ameeleza hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ikiwa ni siku mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita kurejesha Sh5.48 milioni kwa mwalimu Rose Mgomba wa Shule ya Msingi Lukaranga aliyedai kutapeliwa.

Wasiwasi watanda kampuni ya Qnet

Katika maelezo yake, Mganga alisema urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kisheria kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni upatu haramu.

Mbali na kukemea suala hilo, alizitaka taasisi zinazofanya uchunguzi kuhusiana na sakata la kampuni ya Qnet kushirikiana kwani wanajenga nyumba moja.

Alisema shughuli inayoendeshwa na kampuni ya Qnet ni upatu na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ameanza upelelezi kuhusiana na sakata hilo.
Kwanini kumuuzia mtu uhuru wake nao usiwe kosa! Unatuhumiwa kosa kama ni la kweli ama si la kweli unawekwa mahabusu kisha DPP anakuambia mjadiliane ili akuachie, mjadala toa kiasi fulani cha pesa nitakuachia bila masharti! Huu si utaratibu wa utawala wa sheria hata kidogo.
 
Hyo ndio dawa ili watu akili iwajie waache kupenda hela za mteremko we uliskia wapi unaweka laki tano sijui baada ya miezi 6 una milion 5 sijui umekaa kitako kwako mtu anakufugia kuku akuletee hela...

DPP hvi hvo wacheni wajinga wakusanye nyie bebeni mana tunapiga kelele kila siku humu hawaelewi
Imagine 😁
 
😁😁 Niliwahi kumtembelea dada yangu binamu Mmoja hivi akaanza kunipa story Kama hizi sijui kapata kampuni gani inayo Fanana na Bitcoin so wanasemina inafanyika kempisky so anakwenda next weekend mwenyewe alikuwa anadai kwamba huo mchongo ukitiki tu anakuwa mult millionaire Mimi nikawa na msikiliza tu huku kimoyo moyo na muambia Ndugu tayari umeshapatwa na bwana Pepsi ndio unakwenda kulizwa hivyo ...

Yaani jinsi alivyokuwa anaamini kuhusu huo Mchongo unadhani mlokole vile anavyoamini masuala ya ufufuo na uzima ..Mimi sikutaka kumshtua niliachana nae ageuzwe mjinga ndio wali wao
Vipi sasa hivi ashakuwa tajiri? Hahaha chezea pesa wewe watu wanapigwa kwa matamaa yao
 
Mambo niliyo jifunza...

1. Idara za serikali hazina ushirikiano, yaani ziko ziko tu!

2. Usalama wa taifa wanatakiwa wajichunguze kama bado wanastahili kuendelea kuitwa TISS au usalama wa CCM!

3. Inawezekana hii issue ilikua planned na serikali ili pesa zikiwa nyingi wazikwapue kwa kisingizio kwamba hazirudishwi.
Sio inawezekana huo ndio uhalisia huyo Mr kuku waweza kukuta alikuwa na backup ya hao hao na pesa ya mtaji alitoa serikalini. Kilichokuwa kinaendelea kuhusu kesi yake Ni maigizo tu
 
Tapeli wa ukweli ni yule anaeacha tapeli wa uwongo akusanye hela nyingi kutoka kwa wanyonge hadi zifike billions then anaenda kuzikomba zote kutoka kwa tapeli wa uwongo na kuzihamishia BOT bila ya kuwarudishia wanyonge hela zao.
Yaani ni ile ya mwizi kukamata mwizi na kunyanga'anya mali alizoiba na kuzitaifisha. Wote ni wezi tu. Ina maana hata TAKUKURU wanapookoa mamilioni ya wastaafu waliotapeliwa wanapaswa kuzipeleka BOT sio kuwarudishia waliotapeliwa!
 
Mpaka madhara yatokee ndiyo mnakumbuka na penyewe kwa watu baada ya kulalamika,,
Hili taifa sijui likoje eti ndiyo linasema linawataalamu, kumbe hakuna kitu wote wanajua matumbo tu..
H2i Mungu anawaona na 90,000/= yangu mpaka kaofisi kamefungwa______
 
Huu ni wizi wa wazi wazi unaotaka kufanywa na serikali kupitia DPP.

Sitaki kuamini kwamba serikali imekosa hela kiasi hicho mpaka inaamua kutumia uonevu unaofanywa kwa wanainchi wake Kama fursa ya kujikusanyia pesa.

Poor government
Poor DPP.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
DPP anapenda fedha za bure bure sana

Sioni mantiki kwanini DPP Anasema ni makosa kuwarudishia wawekezaji fedha zao walizowekeza huko kwenye UPATU!! Mtu unapowekeza mahala anategemea kupata returns na kama hapati hiyo ndio RISK ya kuwekeza; mbona hata kwenye mabenki ni hivyo hivyo; benki inapofilisika wale walioweka fedha zao katika benki husika kuna kiasi cha fedha zao wanarudishiwa!!!

Dpp anatumia sheria ipi kutaifisha pesa za watu! Huo ni uporaji wa fedha za masikini kitu ambacho serikali inatakiwa kuwasaidia wananchi wake warudishiwe pesa yao badala ya kuwapora.

Huu unaoitwa UPATU [ wazungu wanaita PONZI SCHEME] ni mchezo ambao hata serikali yetu inaufanya kwa kutumia fedha za wafanyakazi zinazowekwa kwenye Pension Funds na ndio maana mifuko kama NSSF inakuwa na matatizo ya kuwalipa wafanyakazi wanapostaafu!!!! Tofauti yake tu ni kwamba UPATU huo unachezwa na serikali!!!!

Orodha ya waathirika wa michezo hii ipo, sasa kwanini serikali inapoifunga hii michezo isiwarudishie wahusika fedha zao? Onesheni kwa vitendo kuwa nyie ni seriklai ya wanyonge badala ya kupiga mayowe tu!!!
 
Hebu acheni kulialia kipindi cha kuishi kwa ujanja ujanja kishapita na mda was kufanya Nazi...kisheria hill in kosa na wahusika wote wana makosa ushasikia serikali inawarudishia waliowekeza kwe biashara ya bangs....na hili sio Tanzania tu..cheki hapo sheria za beberu zinavyosema Pyramid schemes are illegal in New York State, as well as in many other states. Article 23A of the General Business Law of the State of New York §359-fff sets forth the criminality of initiating and participating in pyramid schemes (also known as chain distributor schemes
Swali rahisi kuliko yote ni hili.
Kwanini serikali iruhusu kampuni ya Qnet kuingia nchini, kufanya shughuli zake kwa uwazi na kulipa kodi (ndivyo inavyoelezwa) kwa zaidi ya miaka sita hapa Tanzania wakati ni upatu usioruhusiwa?

Nani anapaswa kuanza kulaumiwa katika hili la Qnet?
 
Mpaka madhara yatokee ndiyo mnakumbuka na penyewe kwa watu baada ya kulalamika,,
Hili taifa sijui likoje eti ndiyo linasema linawataalamu, kumbe hakuna kitu wote wanajua matumbo tu..
H2i Mungu anawaona na 90,000/= yangu mpaka kaofisi kamefungwa______
Hahahah
 
Back
Top Bottom