DPP: Ni kosa kuwarejeshea fedha waliowekeza QNET

DPP: Ni kosa kuwarejeshea fedha waliowekeza QNET

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
12,256
Reaction score
23,357
qnet.jpg

Panda ili uvune maradufu ni kauli ya kitapeli inayotumiwa na matapeli wengi wa upatu!

Lakini tujiulize; inawezekanaje nchi ilivyojaa usalama wa taifa kuanzia uchochoroni hadi Bank wasimjue mchezesha upatu kuwa ni tapeli!

Mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano tapeli anafanya miamala kimyaa!

Tapeli anasambaa kijiji, kitongoji, wilaya, mkoa hadi taifa kimyaaa!

Hadi mwalimu mmoja anapolalamika ndipo tunajua huyu mcheza upatu ni tapeli. Katapeli bilioni 17, hilo ni kosa!

Tapeli anahukumiwa faini ni million 5 kama hana jela itamhusu!

Halafu akaunti na mzigo wote wa 15 bilioni UNATAIFISHWA! (Ni kosa kuwarudishia waliotapeliwa)

Tapeli tunamwachia aende zake (Case closed)

Mimi niliyeishia darasa la saba nisaidieni kumtambua Tapeli ni yupi!

IMG-20201218-WA0001.jpg

=========

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na kampuni ya QNET kisha kudai wametapeliwa kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Ameeleza hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ikiwa ni siku mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita kurejesha Sh5.48 milioni kwa mwalimu Rose Mgomba wa Shule ya Msingi Lukaranga aliyedai kutapeliwa.

Wasiwasi watanda kampuni ya QNET

Katika maelezo yake, Mganga alisema urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kisheria kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni upatu haramu.

Mbali na kukemea suala hilo, alizitaka taasisi zinazofanya uchunguzi kuhusiana na sakata la kampuni ya QNET kushirikiana kwani wanajenga nyumba moja.

Alisema shughuli inayoendeshwa na kampuni ya Qnet ni upatu na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ameanza upelelezi kuhusiana na sakata hilo.
 
Sijui kwanini serikali uwa hairejeshi pesa kwa wenye nazo, hata za DECI iipita nazo, na za Mr. Kuku naona zinapelekwa BOT na za QNET itakuwa hivyo hivyo. Kama wanataka kusolve tatizo wafuatilie na kufunga zote kufunga Qnet tu hawajasove jambo. Zipo nyingi kuna moja inaitwa phyto science mwaka juzi walimpiga jamaa yangu milion 15, na zipo nyingine nyingi tu.

Eti wanajifanya wanauza madawa wameunga unga vipicha eti Obama anaunga mkono kampuni hiyo, mara kikwete wanaonyesha watu picha uongo mwingi. Kujiunga ndo hivyo milioni 3 sijui uunge watu wengine 5 then hata usipofanya kazi unapokea dollar 3000 kila mwezi. Jamaa yangu akaona isiwe tabu akaunga ndugu kwa kuwalipia wewe, hizo dola 3000 alizisoma tu kwenye makaratasi na hiyo pesa aliyoweka alirudishiwa dollar 200 tu.
 
Tapeli wa ukweli ni yule anaeacha tapeli wa uwongo akusanye hela nyingi kutoka kwa wanyonge hadi zifike billions then anaenda kuzikomba zote kutoka kwa tapeli wa uwongo na kuzihamishia BOT bila ya kuwarudishia wanyonge hela zao.
 
Halafu tapeli anamwachia tapeli
 
Tapeli wa ukweli ni yule anaeacha tapeli wa uwongo akusanye hela nyingi kutoka kwa wanyonge hadi zifike billions then anaenda kuzikomba zote kutoka kwa tapeli wa uwongo na kuzihamishia BOT bila ya kuwarudishia wanyonge hela zao.
Siri Kali
 
Sijui kwanini serikali uwa hairejeshi pesa kwa wenye nazo, hata za DECI iipita nazo, na za mr kuku naona zinapelekwa BOT na za Qnet itakuwa hivyo hivyo. Kama wanataka kusolve tatizo wafuatilie na kufunga zote kufunga Qnet tu hawajasove jambo. Zipo nyingi kuna moja inaitwa phyto science mwaka juzi walimpiga jamaa yangu milion 15, na zipo nyingine nyingi tu.

Eti wanajifanya wanauza madawa wameunga unga vipicha eti Obama anaunga mkono kampuni hiyo, mara kikwete wanaonyesha watu picha uongo mwingi. Kujiunga ndo hivyo milioni 3 sijui uunge watu wengine 5 then hata usipofanya kazi unapokea dollar 3000 kila mwezi. Jamaa yangu akaona isiwe tabu akaunga ndugu kwa kuwalipia wewe, hizo dola 3000 alizisoma tu kwenye makaratasi na hiyo pesa aliyoweka alirudishiwa dollar 200 tu.
Hata waliocheza upatu/wanachama nso ni waharifu,
Hivyo Serikali inaamua kuwaadhibu kwa kutaifisha pesa zao.ili wajifunze.
 
Hizo upatu nyingine haziwezi kufungwa ni mpaka wafikishe fedha ambazo ni billions then zinahamishiwa BOT.Yaani DPP ni TRA ya kimkakati!
Ni kama mchezaji aotee afunge goli, lefa aamuru faulo lakini goli lihesabiwe
 
Hata waliocheza upatu/wanachama nso ni waharifu,
Hivyo Serikali inaamua kuwaadhibu kwa kutaifisha pesa zao.ili wajifunze.
Nieleweshe mimi mwananchi niliyeishia la saba nikuelewe!
 
Hata waliocheza upatu/wanachama nso ni waharifu,
Hivyo Serikali inaamua kuwaadhibu kwa kutaifisha pesa zao.ili wajifunze.
Lakini mkuu, unakuta kampuni kama DECI, Referal Africa, QNET zina vibali vyote, QNET iko Tanzania kwa zaidi ya miaka 6, kiasi kwamba watu wanaamini iko sawa, Mr. Kuku pia hadi alikuwa anajitangaza kwenye ma TV. Wa kulaumiwa zaidi ni vyombo vya serikali kwa kuzipa usajili kampuni za kitapeli, bora ingekuwa ni upatu baina ya kundi la watu lisilokuwa na usajili wala ofsi haya yana usajili kabisa, na wanawaaminisha kwa mapicha waliyopiga na viongozi.
 
Hizo upatu nyingine haziwezi kufungwa ni mpaka wafikishe fedha ambazo ni billions then zinahamishiwa BOT.Yaani DPP ni TRA ya kimkakati!
Kwakweli ndiyo maana nashangaa wanadeal tu na QNET, zipo kampuni nyingi za upatu na zinajulikana zina maofsi makubwa na zinaendelea kupiga watu kwa pyramid scheme kwa kuingiza watu upate commission,
 
Kama kwa misingi hiyo basi hizi kampuni za kitapel zinamkono mrefuu ...,iliii mpunga ukishakusanywa wanapita nao

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom