DPP: Ni kosa kuwarejeshea fedha waliowekeza QNET

DPP: Ni kosa kuwarejeshea fedha waliowekeza QNET

Kwanini hawa Qnet wamechelewa kuanza kushughulikiwa, na ni kwanini Kigwangwallah alisaidia hawa matapeli? Kuna mgao alipata? Achunguzwe
Haya qnet etc huwa wana waingiza public figure kama gea tu,yawezekana kingwa alikuwa hajui lolote khsu qnet nmna inavyofanya kazi!
Na kuhusu kuchelewa mara nyingi maumivu na malalamiko yanapotokea ndiyo serikali inatia mkono..
Kama serikali inania na dhati imepige maarufuku biashara zote za aina hii

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 

Q NET Waombwa Kujenga Kiwanda Tanzania​


21 Sept 2017
Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji imeishauri kampuni ya uuzaji bidhaa kwa njia ya mtandao ya QNET kufungua kiwanda chake nchini Tanzania
 

Q NET Waombwa Kujenga Kiwanda Tanzania​


21 Sept 2017
Wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji imeishauri kampuni ya uuzaji bidhaa kwa njia ya mtandao ya QNET kufungua kiwanda chake nchini Tanzania

Aiseeeeh nashika kichwa!
 

22 Mar 2019
QNET is one of Asia’s leading direct selling companies, offering meaningful products in diverse markets. Our focus is to enable people to rise through solutions that power entrepreneurship and enhance lifestyles.
Source: QNET AFRICA
 
Binafsi naona hizo kampuni za upatu hazina kosa kama mtu anawaza kuna pesa za bure tu bila kufanya kaz waendelee kupigwa tu hakuna namna
 
Uyo Mwinyi anasema hatofukua makaburi? Ayafukue makaburi tujue kama kweli anafanya maamuzi magumu. Maamuzi ya kusimamia fedha za umma sio magumu ila kuwakamata waliotoka madarakani kwa kuiba hela za umma na kuwafungulia mashtaka ndio maamuzi magumu!
 
Qnet uyu,wanampelekea nani dhuluma
Mwanangu kwel wew bi darasa la 7...yaan umechanganya madesa vibaya mno

Yaan hata kungamua umeshindwa kuwa Mr kuku na Qnet ni vitu viwil tofaut...

Sasa kama umeshindwa hilo...jambo dogo tu...huu uzi wako hauna maana..kwa maana hyo yaan hunaelewa hata scenario nzima zikoje..ni kwamba umedandia train kwa mbele..nakuomba ufanye utafit wa mada yako na ulete uzi mwingne hapa.

Ovyo kabisa...wa Tz ni lawama tu wakat hzo pesa mnapeleka wenyew...lawama nyiiiing

Halaf sasa cha ajabu wachangiaj wote wa uzi nao wanajadili utopolo aliouchanganya mtoa mada..dah..kumbe kenge ni weng humu
 
Sheria nyingine ni kandamizi sana. Anaeumia hapo ni mwananchi wa kawaida. Mbele ya safari waje watokee watu warekebishe hili, halina unafuu kwa waathirika.
 
Panda ili uvune maradufu ni kauli ya kitapeli inayotumiwa na matapeli wengi wa upatu!

Lakini tujiulize; inawezekanaje nchi ilivyojaa usalama wa taifa kuanzia uchochoroni hadi Bank wasimjue mchezesha upatu kuwa ni tapeli!

Mwaka wa kwanza, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano tapeli anafanya miamala kimyaa!

Tapeli anasambaa kijiji, kitongoji, wilaya, mkoa hadi taifa kimyaaa!

Hadi mwalimu mmoja anapolalamika ndipo tunajua huyu mcheza upatu ni tapeli. Katapeli bilioni 17, hilo ni kosa!

Tapeli anahukumiwa faini ni million 5 kama hana jela itamhusu!

Halafu akaunti na mzigo wote wa 15 bilioni UNATAIFISHWA! (Ni kosa kuwarudishia waliotapeliwa)

Tapeli tunamwachia aende zake (Case closed)

Mimi niliyeishia darasa la saba nisaidieni kumtambua Tapeli ni yupi!



=========

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa kwamba kufanya hivyo ni kosa.

Ameeleza hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ikiwa ni siku mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Geita kurejesha Sh5.48 milioni kwa mwalimu Rose Mgomba wa Shule ya Msingi Lukaranga aliyedai kutapeliwa.

Wasiwasi watanda kampuni ya Qnet

Katika maelezo yake, Mganga alisema urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kisheria kwa sababu biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni upatu haramu.

Mbali na kukemea suala hilo, alizitaka taasisi zinazofanya uchunguzi kuhusiana na sakata la kampuni ya Qnet kushirikiana kwani wanajenga nyumba moja.

Alisema shughuli inayoendeshwa na kampuni ya Qnet ni upatu na tayari Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ameanza upelelezi kuhusiana na sakata hilo.
Msomi wetu asitoe uamuzi wa jumla kama huu. Ndio hiyo biashara ni haramu, je muathirika alijua hilo? Kama qnet imerejesha hizo pesa, kwa nini muathirika asirudishiwe pesa zake? Anayepaswa kupewa adhabu ni qnet na sio aliyetapeliwa. Kufanya kinyume ni wizi kwa upande wa serikali inayotaka kukomba pesa za kila mtu na isiyotosheka.
 
Back
Top Bottom