Dowans yamuibua Mama Maria Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dowans yamuibua Mama Maria Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 31, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,849
  Likes Received: 39,839
  Trophy Points: 280
  • Asema wananchi wataichukia CCM daima

  na Waandishi wetu
  SAKATA la serikali kutaka kuilipa mabilioni ya fedha kampuni ya Dowans, limeendelea kuchukua sura mpya, ambapo safari hii mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere, ameitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete isikimbilie kuilipa kampuni hiyo badala yake ivute subira.

  Mjane huyo wa Baba wa Taifa, amesema serikali inapaswa kuvuta subira kwanza juu ya suala hilo na si kubariki malipo hayo kwa harakaharaka na kwamba iwapo Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICC), imeamuru, basi isiwe kigezo cha leo ama kesho kulipwa.

  Mama Maria Nyerere alisema hayo juzi nyumbani kwake, Mwitongo Butiama, wilayani Musoma, Mara alipozungumza na waandishi wa habari waliokuwa wameambatana na msafara wa viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), kutoka mikoa ya Mbeya na Shinyanga.

  Viongozi hao wa UVCCM waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni pamoja na kamanda wa umoja huo kutoka mkoa wa Mbeya, Mwakajumilo Isaac, na mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa wa UVCCM kutoka Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, Dinawi Gabriel.

  Katika ufafanuzi wake juu ya malipo hayo ya Dowans, Maria Nyerere alisema: "Licha ya Mahakama ya ICC kuiamuru Tanzania iilipe Dowans sh bilioni 94, ni vema serikali ikatafakari kwa umakini mkubwa na si kukimbilia kulipa!"

  Alisema viongozi wa serikali na wana CCM kwa ujumla, wanapaswa kuliangalia kwa umakini zaidi suala hilo, ili lisije kuleta athari na kusababisha wananchi kukichukia chama hicho.

  "Kwa hili la Dowans kutaka kulipwa, mimi nashauri serikali isikimbilie kulipa fedha hizo…bilioni 94 ni fedha nyingi na kama hawatafikiria kwa umakini mkubwa wananchi wanaweza kuichukia daima CCM.

  "Tusikurupuke, tusikimbilie kuilipa Dowans….huu ndiyo ushauri wangu kwa serikali na wana CCM kwa ujumla," alisema mke huyo wa Baba wa Taifa, huku akiwatania waandishi wa habari kwa kusema: "Ninyi mnataka ama hamtaki Dowans ilipwe?"

  Hata hivyo, Maria Nyerere aliwataka viongozi wa CCM kurudia utaratibu wa zamani wa Baba wa Taifa wa kutumia vikao vyake vya ndani kukosoana, kukemeana na hata kuchukuliana hatua za kimaadili ili kuzima mambo ya chama kutoka nje.

  "Baba wa Taifa aliwahi kusema kwamba bila CCM madhubuti nchi itayumba! Kauli hii ina maana kubwa sana kwa wana CCM waizingatie!" alibainisha.

  Hata hivyo, alisema siku zote amekuwa akifuatilia na kusikiliza mambo ya Richimond, Dowans na EPA, lakini baadhi ya viongozi na wanasiasa wameonekana dhahiri kuchukizwa na kuamua kujitoa kupambana na mambo wanayoona hayana faida kwa taifa na wananchi wake.

  Naye Mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Husein Bashe, alisema vijana hawapo tayari kuipokea CCM ikiwa chama cha upinzani hivyo ni vema viongozi waliopo madarakani wauambia umma kama wameshindwa kutekeleza sera za chama hicho kikongwe.

  Alisema vijana wanasikitishwa na malumbano ya takriban miaka mitatu kuhusu kampuni za Dowans na Richmond kufua umeme wakati wananchi wakiendelea kukaa gizani kwa sababu ya kutokuwapo kwa umeme.

  Alibainisha kuwa wimbo wa Dowans na Richmond umechosha na kama viongozi hawana jipya ni vema wakaachia madaraka ili kuwapisha wenye dhamira ya dhati ya kulitumikia taifa kwa maslahi ya wengi.

  Alisema inasikitisha kuona wanafunzi wengi wa shule za kata wakifeli mitihani yao kwa sababu ya uhaba wa walimu, madawati, vitabu lakini viongozi hawashtuki na badala yake wamekuwa wakiendeleza wimbo wa Dowans na Richmond.

  "Hatuko tayari kuipokea CCM ikiwa chama cha upinzani, tumechoshwa na matatizo tuliyonayo, viongozi wachape kazi na kama hawawezi waachie ngazi" alisema.

  Wakati huohuo, Chama cha Wananchi (CUF) kinatarajia kufanya mandamano ya amani Jumatatu ijayo kupinga mpango wa serikali kuilipa kampuni ya Dowans.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Julius Mtatiro, alisema maandamano hayo yataanzia eneo la Buguruni na kuishia katika viwanja vya Kidongo Chekundu.

  Maandamano hayo yatakayoongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba na kuongozwa na viongozi wa kitaifa wa CUF ambao watahutubia maelfu ya waandamanaji na kutoa msimamo wa chama juu ya suala hilo.

  Aidha, aliwataka wananchi, wanaharakati, mashirika mbalimbali na wapenzi wa CUF kujitokeza kwa wingi katika maandamano hayo.

  Kuhusu kupata kibali kutoka Jeshi la Polisi, Mtatiro alisema tayari wameshalitaarifu jeshi hilo juu ya maandamano hayo kupitia barua yenye Kumbu.CUF/AK/DSM/NKM/B/002/A2/2011/08 ya Januari 28, mwaka 2011.

  Alisema wanatarajia jeshi hilo halitajaribu kuhujumu maandamano hayo kutokana na ‘taarifa za ki-telijensia' ambazo zimekuwa maarufu hivi karibuni.

  Sakata la kulipwa kwa kampuni hiyo limekuja baada ya serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kutangaza kuamua kuilipa kampuni ya Dowans fedha hizo kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC).
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,849
  Likes Received: 39,839
  Trophy Points: 280
  Mama Maria: Kuilipa Dowans tatizo kubwa


  * Ataka CCM, wanachama watafakari kabla ya kulipa

  Na Daud Magesa, Butiama

  MJANE wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere ameibuka na kusema kulipa mabilioni ya fedha kwa kampuni ya
  Dowans ni sawa na kuwaingiza wananchi kwenye matatizo makubwa.

  Mama Nyerere amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wanachama wake wakae watafakari kwanza kabla ya kulipa fedha hizo, zinazokadiriwa kufikia sh. bilioni 94, kwa kuwa suala hilo litafanya CCM ama isiaminike, au wananchi waichukie.

  Aliitaka serikali kuwawajibisha wote wanaohusika na Dowans ili kurejesha maadili ya uongozi kama ilivyokuwa wakati wa mwalimu, badala ya kukurupuka kulipa sh. bilioni 94 bila kuangalia athari watakazopata wananchi.

  Mama Maria Nyerere alitoa kauli hiyo nyumbani kwake Mwitongo, Butiama, juzi, wakati akizungumza na Kamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Bw. Mwakajumilo Isaac ambaye pia ni Mhasibu Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Mbeya, waliomtembelea baada ya kuanguka hivi karibuni na kuumia wakati akielekea kanisani.

  Alisema kwamba jahazi hili (Tanzania) linaelekea kuzama kutokana na vurugu na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na hivyo kuwataka Watanzania watambue kuwa, 'sote tutaangamia kutokana na athari za machafuko hayo'.

  Alisema kuwa baadhi ya viongozi na Watanzania wamepoteza maadili na hivyo kutoa kauli zinazoweza kuiingiza nchi kwenye machafuko kwa maslahi ysao binafsi, na kwa manufaa yao kisiasa.

  Baadhi ya kauli hizo, alisema ni zinazohusiana na mifarakano ya kidini, na nyingine kuhusu na suala la dowans , ambayo alikuwa anaifuatulia kwenye televisheni.

  Kuhusu mabadiliko ya katiba, Mama Nyerere alisema amekuwa akifuatilia mijadala mbalimbali kwenye runinga na kuona ulivyopamba moto, na hata kijijini kwake, Mwitongo, nako mjadala unaendelea.

  Alisema kwamba Watanzania waendelee kuwa watulivu na mijadala hiyo iendeshwe kwa kushirikisha wadau na viongozi kutoka makundi yote kwa haki na usawa, huku wakizingatia umoja, amani na utulivu wa taifa ili kuenzi mazuri yaliyoachwa na waasisi wa taifa hili kwa manufaa ya wote.

  Mjane huyo wa Baba wa Taifa alieleza kuwa viongozi mbalimbali, wananchi na wadau wote wawe watulivu huku wakiliombea taifa wakati mchakato wa katiba mpya ukisubiriwa
  kuanza.

  Akigeukia sera ya Kilimo Kwanza, aliwaeleza makada hao wa UV-CCM kwamba watu hawapendi tena kilimo, hasa vijana wenye nguvu ,wamekuwa wakikimbilia mijini kufanya biashara na kusababisha maeneo mengi ya vijijini kukabiliwa na tishio la njaa huku mabepari nao wakipigania kuondoa historia nzuri ya taifa.

  "Vijana wangu, hakuna mtu ambaye angependa kuwa maskini, lakini pia huwezi kuwa tajiri kwa njia za mkato, hasa kwa hawa watumishi wa umma, jambo kubwa ni viongozi kuzingatia na kufuata maadili kama ilivyokuwa kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwl Julius Nyerere kwa kuthubutu kuwaondoa wasiofaa na kuwataja hadharani," alisema na kuongeza:

  "Serikali inapaswa iwaondoe wanaoiharibia, hata kama wanafahamiana. Pia ikihakikisha kauli za watu na wanasiasa zisizofaa kwa Watanzania, zenye lengo la kuhatarisha amani hazipewi nafasi na hatua kali zichukuliwe kwa wale wanaotoa kauli za uchochezi ili kuliangamiza jahazi la taifa letu lenye historia ya pekee na mfano kwa mataifa mengine".

  Alitoa wito kwa viongozi wa serikali kuhakikisha misingi yote ya taifa iliyoasisiwa na viongozi waliotanguliwa wanaendelea kuilinda wakiweka mazingira mazuri kwa kuboresha huduma mbalimbali za kijamii hususani vijijini ambako utoaji wa huduma hauridhishi na hauna tija.

  Alisema uduni wa huduma hizo husababisha jamii kulalamikika kutokana na wananchi wengi wa kipato cha chini kukosa huduma za afya, maji, elimu, barabara, bei nzuri ya mazao na upatikanaji rahisi wa nishati ya umeme.

  Aliwaasa Watanzania kuacha kukubali kutumiwa na watu ambao malengo yao ni kujinufaisha kisiasa na kupata umaarufu ,huku wakiliacha taifa likiangamia kutokana na kutaka kuwagawa kwamkuzungumzia ukabila, udini na rangi vitu ambavyo wakati nchi ikipata uhuru Mwl. Nyerere na waasisi wengine walivipinga kwa nguvu zote, na hadi leo tu wamoja.
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 21,271
  Likes Received: 3,946
  Trophy Points: 280
  Ivute subira au isilipe kabisa?....Mama wamemkwoti vibaya nini?
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,849
  Likes Received: 39,839
  Trophy Points: 280
  Mwisho wa CCM umefikia kikomo.....................hasa unapoona mama wa mwasisi wa chama hicho naye anakitolea nje.................kwa ufisadi.........................
   
 5. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  lkn hofu ya mama Nyerere ni ccm kuchukiwa hawaonei huruma wananchi wanaokosa huduma muhimu wkt wanalipa kodi
   
 6. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,343
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Maneno ya Bashe
  “Hatuko tayari kuipokea CCM ikiwa chama cha upinzani, tumechoshwa na matatizo tuliyonayo, viongozi wachape kazi na kama hawawezi waachie ngazi” alisema.

  Wanamwambia nani hasa maneno haya??
  Nani hachapi kazi??
  Nani aachie ngazi??

  Chama chao ndio kiko madarakani na kimeunda serikali sasa badala ya matamko nilitegemea vitendo zaidi.
  Kama bodi ya mikopo haifanyi kazi serikali ya CCM iivunje mara moja wala huhitaji maandamano.

  Tuwaachie CUF, CDM na wengine kutoa matamko na kufanya maandamano kuelezea hisia zao kwani hawana serikali ya kutekeleza matakwa yao isipokuwa kwa kushinikiza.
  CCM wafanye kazi tuone matunda ya kazi yao na sio kutoa matamko.
  Nahisi wanacheza sanaa fulani ambayo wenye macho tunatakiwa kuibaini haraka.

  UVccm in uwakilishi kwenye vyombo muhimu vya maamuzi ni vipi wanashindwa kuwabana kina Kikwete, Pinda, Ngeleja, Werema huko hadi wasubiri press conference kama ambavyo wapinzania wanafanya.

  Ninaona ni propaganda aimed at diverting our attention, esp the youth, on pressing issues.

   
 7. n

  ngoko JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hili dude DOwans ni sikio la kufa, wananchi wana perception yao, viongozi na nao wanayakwao , bahati mbaya waliyonayo viongozi haiuziki kwa wananchi lakini kwa kutumia vigezo vya kisheria wanajitahidi kusafisha dude lililoka chooni miaka nenda rudi ili lionekane safi machoni kwa watu. the experience of Tunisia, Algeria , Misri ina kila sababu ya kufika EAC na mguu wake wa I utakuwa TZ, hope mapolisi watawapelekea viongozi habari za kiintelijensia zisizochujwa ili wabadilike na kuwa pamoja na watu wao.
   
 8. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,343
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Wanaweza kuwa wamemkwoti sahihi BUT she is just being diplomatic.
  She is not vocal by nature na huyu mama akifikia kusema jambo basi ni kweli linamkera.
  Very unfortunate CCM has lost touch with reality

  Maria Nyerere is my all time Tanzania First Lady, hawa wa siku hizi mmh!!
   
 9. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mi napenda sana mabadiliko lakini usijidanganye mabadiliko kama ya Tunisia Tanzania hayaji.Intelijensia inaonesha yakija huku yatakuwa ni vita ya kidini.Akiwepo Kikwete au ikiwa hayupo.Tanzania hatuwezi kuunganishwa na madai ya mikate ya Tunisia.
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,948
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mama nchi yako ya Tanzania mpaka sasa hivi tunapumulia tu mashine.
   
 11. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,343
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hivi CCM umekuwa vipi safari hii??

  Sasa hapo tatizo lako ni Nyerere au Mama Maria au hoja alizotoa juu ya Dowans na CCM?

  Jadili hoja mkuu ndo kwanza Jtatu imeanza kwa nini unachoka mapema??
   
 12. H

  Haika JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,310
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa, Mama yetu, nakuunga mkono, huchagua maneno ya kusema,
  Akili anazo (AMI) tu kama wewe na mimi, au unadhani wewe uko juu zaidi? una access ya ukweli zaidi kuliko mama Maria?
  Hongera mama kwa kuwa Mtanzania halisi, Mwanamke, mkweli, sio mropokaji. Unasoma alama zote za nyakati, na watu wanaokuzunguka. Sio rahisi kuelewa uko katika position gani kwa nchii hii ila tunashukuru kuwa tunaendelea kujifunza character kutoka kwako.
   
 13. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,046
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka mwaka 2005 huyu mama alimpatia Jk zawadi ya Bible.. Imwongoze apate ushindi wa kishindo..
   
 14. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,331
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  Hata kama anawaonea huruma wananchi kukosa huduma, lkn kikubwa hapo ni kule kuchukiwa kwa CCM kwani kutapelekea kutokuwepo madarakani na hatimaye hata yeye kukosa POSHO (wanaendelea kufaidi matunda ya nchi hii ati)
   
 15. L

  LAT JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo unashauri JK asizongwe..... kwa sababu unampenda sana JK au...?
   
 16. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mimi wala sina mapenzi sana na JK wala na CCM yake.Azongwe sana kwa upuuzi wowote ambao kweli kafanya.Ambacho tumeshtuka nacho ni ajenda za maaskofu kupitia CHADEMA.Mpaka sasa tunachoona ni hadithi ya mwanakodoo na mbwa mwitu.

   
 17. M

  MushyNoel Senior Member

  #17
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata baba wa taifa angekuwepo angepata kichefuchefu katika hili.Tayari tunajua kwamba mashahidi walioenda kuitetea serikali wapanga kushindwa kesi.Mwakyembe alipata kushangaa ni mawakili gani hao wameshindwa kesi ndogo kiasi hicho.Kwamba watalipa lisitumbue kwa sasa cha kufanya kwa sasa na fikra zote zilenge kwenye mkakati wa nini tutafanya baada ya ubabe huo.Upepo wa kupinga ukandamizaji tayari ulianza Tunisia,ukaitikia misri baadae yemen sasa kwetu kuna uwezekano ukapita wakati ukiwa unaelekea Zimbabwe
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,466
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 0
  Ina maana baada ya baba wa taifa kututoka, wanafamilia wamekoma kuwa wananchi wa Tanzania wenye haki ya kikatiba kutoa maoni yao?
  Hebu acha mitizamo kama hii ndugu. Kutoa maoni yake huyu mama kunakuburuza vipi?
   
Loading...