Kwa kumalizia ni RA na wenzie wametuingiza mjini hapa na wanasheria wetu wanatakiwa kujiuzulu pamoja na menejimenti ya Tanesco. Vilevile wale wote waliosign mkataba huu wafikishwe mahakamani kwa kulitia taifa hasara maana sijawahi kuona mkataba wa ovyo kama huu ambao mtu anaruhusiwa kutransfer mkataba kwa mtu mwengine bila kushirikisha upande wa pili ni jambo la kushangaza. Vilevile sidhani kama inawezekana hii kesi ikawa appeal maana wao wamerely katika Laws of Tanzania , ila wanaweza kufungua kesi ya udanganyifu kwa Dowans kuwa ni kampuni feki ila sijui kama nia hiyo ipo ikisha wawadai fidia ya mabilioni ya fedha kwa hasara (kwani hata ICC wamesema kama wangelifanya utafiti vizuri Tanesco ingelikuwa na valid defence of misrepresentation and falsity) hivyo basi wanaweza kuwatingisha huko ikawa
lakini mtu yoyote mwenye akili huwezi kwenda kwenye abitration ambayo mwisho wa siku haikupi chance ya ku-appeal . sema kwa sababu serikali kupitia hiyo tanesco walijipanga kushindwa ndio maana wakajipeleka kichwa kichwa na utetezi goi goi ili kufanikisha walicho kuwa wanata. nacho ni kuilipa dowans
Mkuu mimi siyo mwanasheria ila nakumbuka kuna sehemu kwenye hiyo ruling, appeal kama haina nafasi. The decision was final! Nilielewa au ignorance ilichukua nafasi?
Mkuu,Mdondoaji said:In the end I am sad to say hizi pesa zitalipwa to waungwana hakuna janja hapa na kodi yangu italiwa ila wanaweza kufungua kesi ya udanganyifu halafu hela zetu zikarudia kwa njia hiyo. Nimekasirika sana hata maji leo sitaki nimesusa!!!!
Mkuu,
Kabla hujakasirika kiwango hicho, hivi waweza kunisaidia? DOWANS walilirithi mkataba huu toka kwa 'kampuni hewa' ya RICHMOND, sasa kwa mawazo yangu ni kuwa "hakuna mkataba" au TANESCO/Serikali waliingia mkataba mpya na DOWANS? Kivipi na kwanini?
Baada ya kugundua kuwa RICHMOND ilikuwa "FAMBA" bado wanasheria wetu wa TANESCO waliendelea kuiacha serikali na shirika letu kuingia mkenge mwingine kama huu?
Kutojua sheria kunatusababishia wengine kushindwa kuelewa kwanini kila kitu kimeenda hivi, enlighten me please
Mkuu,
Kabla hujakasirika kiwango hicho, hivi waweza kunisaidia? DOWANS walilirithi mkataba huu toka kwa 'kampuni hewa' ya RICHMOND, sasa kwa mawazo yangu ni kuwa "hakuna mkataba" au TANESCO/Serikali waliingia mkataba mpya na DOWANS? Kivipi na kwanini?
Baada ya kugundua kuwa RICHMOND ilikuwa "FAMBA" bado wanasheria wetu wa TANESCO waliendelea kuiacha serikali na shirika letu kuingia mkenge mwingine kama huu?
Kutojua sheria kunatusababishia wengine kushindwa kuelewa kwanini kila kitu kimeenda hivi, enlighten me please
Sina cha kusema zaidi ya kubadili fani bna kusoma sheria maana mambo mengi yanafanywa kiolela tu na wanasheria wanaangalia tu na kubaki kupiga makelele badala ya kuchukua hatua!
Hivi kweli mnaamini Wanasheria wa Tanzania walioshiriki kupelekwa huko ICC na kukubali mapema kuwepo vipengele hivyo vya arbitration wakati Tanzania yenyewe inayo Mahakama ya Biashara na utaratibu wa kutatua migogoro ya kibiashara walifanya hivyo kwa sababu hawajui au hawana uwezo?
....................... Sasa kwa mujibu wa hii kesi Dowans wana haki ya kudai compensation kwa kuvunja makubaliano unless kama Tanesco wangelifanya makubaliano ya kumaliza haya maswala nje ya mahakama ndio ingelikuwa ishu nyengine...........!!!!
....................... Ukitaka kujua soma sheria ya Tanzania Investment Act. Utaona ni kiasi gani Serikali imejikoroga katika ku-guarantee favourable conditions to Investors. Pia usisahau Tanzania ni member wa MIGA (Multilateral Investment Guarantee Agency). Sasa tusipolipa hawa Dowans najua watatumia mwanya huo kupiga kelele Duniani kuonyesha kwamba Serikali ya Tanzania haiheshimu wawekezaji na hii inaweza ikakimbiza sana wawekezaji na kuiweka Tanzania katika black list ya investment destinations....................