Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,904
- 1,364
Jamani hii kauli ya Ngeleja kwenye RED ina ukweli wowote!? kama si kweli basi kuna kila sababu ya kutilia mashaka uamusi wa serikali!!
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amewataja wamiliki wa Dowans baada ya kupata taarifa kutoka Brela kwa barua yenye kumb. namba MITM/RC/58550/22 ya Januari 5, mwaka huu ambao ni Dowans Holdings S.A, yenye hisa 81 ya Costa Rica na Portek System and Equipment PTE Limited hisa 54 ya Singapore.
Alisema wakurugenzi wa Dowans wa hapa nchini ni Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenyan).
Wakati Ngeleja akitaja majina hayo, wiki moja iliyopita Tanzania Daima ilikwisha kuwataja wanaomiliki kampuni hiyo.
Alisema hakuna sheria inayowataka wawekezaji wakitaka kuanzisha kampuni nchini ni lazima awepo mbia wa ndani, wanaweza kuanzisha wenyewe ikiwa wamefuata taratibu na sheria za nchi.
Alisisitiza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya ulipwaji fidia wa sh bilioni 94 kwa Dowans na TANESCO kupandisha bei za umeme kama ilivyoamriwa na Ewura.
"Ni upotoshaji mkubwa kuhusisha mambo mawili tofauti... migogoro ya Richmond na Dowans ilipelekwa ICC mwaka 2008, sasa kwanini watu wanaunganisha haya? Labda hii inatokana na watu kupenda kuchakachua maneno," alisema.
Alisema kuwa kuna bidhaa mbalimbali zimekuwa zikiongezeka bei lakini wanashangazwa na hatua ya Ewura kupandisha gharama hiyo kwa asilimia 18.5 na kusababisha baadhi ya makundi kutaka kuandamana wakati ongezeko la bei ya umeme ni suala la kiuchumi na kibiashara kwa shirika hilo.
Raymond Kaminyoge
SERIKALI imeamua kuilipa kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, Sh 94 bilioni kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) na kuwataja wamiliki na wakurugenzi wa kampuni hiyo ambao wote si Watanzania.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Alisema Sh.185 bilioni zilizokuwa zikitajwa kwenye vyombo vya habari ndizo ambazo kampuni ya Dowans iliiomba ICC ilipwe fidia kwa Tanesco kwa kukatiza mkataba walioingia wa kufua umeme, lakini mahakama iliafiki ilipe dola 65 milioni za Marekani.
Alisema fedha hizo zitalipwa baada ya pande hizo zitasajili uamuzi huo katika mahakama kuu.
Serikali tumekwishaamua kuwa tutailipa Dowans dola za Marekani 65 milioni, kama ilivyoamuliwa na ICC ambazo ni sawa na Sh 94 bilioni, kuchelewa kuwalipa kutatufanya tulipe riba ya asilimia 7.5, alisema.
Siyo kwamba kiasi tunachotakiwa kulipa ni kidogo, ila tumeona ni muhimu Watanzania wakafahamu kiasi halisi ambacho tunatakiwa kuilipa Dowans, alisema.
Alisema wameamua kulipa baada ya mwanasheria mkuu wa serikali, kusema kuwa hukumu hiyo ilikuwa halali na kuipinga kungeizidishia serikali gharama.
Mwanasheria mkuu wa serikali ameshauri kutekeleza uamuzi wa mahakama ya usuluhishi endapo uamuzi huo utasajiliwa katika mahakama kuu ya Tanzania, alisema Ngeleja.
Aidha Ngeleja aliwataja wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd, na hisa wanazomiliki katika mabano kuwa ni Dowans Holding S.A ya Costa Rica (81) na Portek Systems and Equipment (PTE) LTd (54).
Aidha Waziri Ngeleja huku akirejea barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brella), aliwataja wakurugenzi na nchi wanazotoka kuwa ni Andrew James Tice (Canada) na Gopalakrishnan Balachandaran (India).
Wakurugenzi wengine kwa mujibu wa Waziri Ngeleja ni Hon Sung Woo (Singapore), Guy Picard (Canada), Sulaiman Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenya).
Kiini cha sakata hilo kilianza mwaka 2006, wakati Tanesco ilipoingia mkataba wa mauziano ya umeme wa Tanesco na kampuni ya Richmond Developmen LLC.
Miezi sita baadaye mkataba huo ulihamishiwa kwa kampuni ya Dowans Holdings ya nchini Costa Rica na baadaye kwa Dowans Tanzania Ltd,
Wakati wa utekelezaji wa mkataba huo, ilizuka hoja kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wabunge kwamba mkataba baina ya Tanesco na Richmond haukuwa halali kisheria hivyo usingeweza kurithiwa na Dowans.
Suala hilo lilizua mjadala mkubwa hali ambayo Tanesco kwa kuwatumia mawakili wa kampuni ya Rex Attorneys ya jijini Dar es Salaam walivunja mkataba huo.
Baada ya kuvunjwa kwa mkataba huo, ndipo kampuni hiyo ikalipeleka suala hilo ICC kama walivyokubaliana na Tanesco kwenye mkataba.
Uamuzi huo wa ICC ulizua mjadala katika siku za hivi karibuni baada ya viongozi wa serikali kutofautiana kuhusu kuilipa kampuni hiyo au kutoilipa.
Wakati Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Samwel Sitta, akiitaka serikali kutolipa Dowans kwa kuwa kufanya hivyo ni uhujumu wa nchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akitaka kampuni hiyo ilipwe.
Majina ya owners wa Dowans jana yametolewa na sijaona jina la JK kama ilivyodaiwa na Slaa. Slaa kama kiongozi wangu shupavu amenivunja sana moyo. I need a leader I could trust na sio kiongozi mwenye Jazba na anyezungumza bila ya kuwa na facts
Hizi si zama za abuniasi kuambia uwongo ili mradi uandikwe kwenye magazeti
Unasema JK own DOWANS lete ushahidi
This is disgusting na mimi sitaki kuwa na kiongozi ambaye alikuwa ni Mchungaji na mtu wa Mungu
Unless ana ushaidi mwingine so i stand to be corrected lakini majina ya waliotajwa jana sijaona jina la JAKAYA MRISHO KIKWETE!!!!!
Bwana Padri acha uhuni umeshakuwa mtu mzima sasa,unajidhalilisha.
Kama una ushahidi kuwa jk ni mmiliki wape vijana wako wapeleke bungeni ukweli ukibainika basi bunge lim impeach.Hatuwezi kuvumilia kuwa na Rais mfanyabiashara.Kwanini unatusumbua vichwa kwa uzushi? tumia vyombo vya kisheria umshugulikie Rais badala ya kuleta mchezo wa kuigiza.Hat hivyo umepoteza hadhi maana umeprove kuw ni muongo mno
Majina ya owners wa Dowans jana yametolewa na sijaona jina la JK kama ilivyodaiwa na Slaa. Slaa kama kiongozi wangu shupavu amenivunja sana moyo. I need a leader I could trust na sio kiongozi mwenye Jazba na anyezungumza bila ya kuwa na facts
Hizi si zama za abuniasi kuambia uwongo ili mradi uandikwe kwenye magazeti
Unasema JK own DOWANS lete ushahidi
This is disgusting na mimi sitaki kuwa na kiongozi ambaye alikuwa ni Mchungaji na mtu wa Mungu
Unless ana ushaidi mwingine so i stand to be corrected lakini majina ya waliotajwa jana sijaona jina la JAKAYA MRISHO KIKWETE!!!!!
MAJAMBO haihitaji uwe genius ili kubaini kuwa watanzania tunapigwa mchanga wa macho kuhusu wamiliki wa DOWANS, kumbuka msajili wa makampuni wa COSTA RICA anasema huko kwao hakuna kampuni iliyosajiliwa kwa jina la DOWANS, lakini katika kutaja wamiliki wa DOWANS bado wanadai kampuni hiyo imesajiliwa COSTA RICA na bado MAJAMBO unawahamini kauli zao kuliko kauli ya msajili makampuni wa costa rica eti unataka ushaidi! Walivyotajwa kwa majina kuwa wameiba BOT fedha ya EPA walisema kama wewe kuwa wanataka utolewe ushahidi leo kila kitu kipo hadharani kuhusu EPA. DEEP GREEN na MEREMETA zilipotajwa wakasema ni uzushi wakadai utolewe ushahidi, lakini BUNGENI baada ya kubanwa sana PINDA akasema yupo radhi kusulubiwa kuliko kuzungumzia hizo kampuni eti itaathiri usalama wa taifa . Hadi leo watu ambao kauli zao MAJAMBO anaziamini wanashindwa kumtaja mmiliki wa KAGODA.
RICHMOND haikusajiliwa Marekani kama walivyokuwa wanadai wapambe wake, lakini ilishinda zabuni ya kuzalisha umeme Tanzania. MAJAMBO na wenzake wakaaminishwa kuwa ni kampuni safi mambo yalivyo haribika ukweli ukawa hadharani kampuni hiyo ni kimeo. MAJAMBO funguka macho nchi hii haina mwenyewe, mwenyewe nchi NYERERE alishakwenda....................... Waliobaki ni wawekezaji wa NDANI (wakoloni weusi)
majina ya owners wa dowans jana yametolewa na sijaona jina la jk kama ilivyodaiwa na slaa. Slaa kama kiongozi wangu shupavu amenivunja sana moyo. I need a leader i could trust na sio kiongozi mwenye jazba na anyezungumza bila ya kuwa na facts
hizi si zama za abuniasi kuambia uwongo ili mradi uandikwe kwenye magazeti
unasema jk own dowans lete ushahidi
this is disgusting na mimi sitaki kuwa na kiongozi ambaye alikuwa ni mchungaji na mtu wa mungu
unless ana ushaidi mwingine so i stand to be corrected lakini majina ya waliotajwa jana sijaona jina la jakaya mrisho kikwete!!!!!
Dowans kosa lao lipi? Rostam kosa lake lipi? JMK kosa lake lipi?
Jee, hamkuona yale madege yakishusha hii mitambo?
Jee hamkuona hiyo mitambo pale Ubungo?
Jee ni haki Tanesco kuvunja mkataba?
Jee mawakili wa Tanesco wamelipwa kiasi gani?
Jee mawakili wa Dowans wamelipwa kiasi gani?
Sasa mbona hajatoa ushahidi mpaka sasa?
Kumbe Dr Slaa alituongopea watanzania?????:A S thumbs_down::A S thumbs_down::A S thumbs_down:
unahitaji ushahidi gani zaidi ya kile anachokisema au akili zako mdando.