Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,580
- 23,914
BAADA YA KUUPITIA VIZURI MKATABA WA TANESCO NA RICHMOND WA JUNE 2006,NA BAADAE NIKAUPITIA MKATABA WA DOWANS NA TANESCO WA DECEMBER 2006,PAMOJA NA MADUDU YOTE AMBAYO RICHMOND WALIYAFANYA DHIDI YA TANESCO BADO KULIKUWA NA CONCERT YA WAZIRI NA SERIKALI HATA KAMA TUNASEMA RICHMOND WALIHAMISHA MKATABA KWENDA DOWANS BILA KUWAELEZA TANESCO SI KWELI KWANI WAZIRI KARAMAGI ALIKUBALIANA NA RICHMOND..blah blah blah !
Kwanza unatakiwa ujifunze adabu na kwa kuanzia ujifunze internet etiquette, you are shouting na sisi si viziwi. Pili ujifunze heshima na ujue kuwa nchi kamwe haiwezi kuyumbishwa na wezi na matapeli. Tatu ujifunze uzalendo kwa nchi yako na taifa lako na uache kabisa kupotosha mambo kwa kuleta utetezi wa kijinga. Lazima ujue kuwa nguvu ya Umma ni paramount - shuhudia inavyofanya kazi hivi sasa dhidi ya ving'ang'anizi kama Mubarak wa Egypt. Wakumbuke Mao Tse Tung wa China, Nicolae Ceausescu wa Romania, Mohamad Reza Pehlavi wa Iran, Ferdinand Marcos wa Phillipines na karibuni Bel Bela wa Tunisia, walivyong'oka kwa nguvu za Umma !
Son of soil unatamka bila aibu kuwa liwapo na liwe Dowans lazima walipwe, hivi hapa unaongea kama nani na hii jeuri na dharau kwa Watanzania unaitoa wapi ? Je wewe ndiye Kikwete mwenyewe ama mbia wake ? Sasa ngoja na mimi nikutamkie wazi kuwa Dowans ikilipwa basi wewe, Kikwete na hilo genge lenu la wezi muanze kutafuta hifadhi nje ya Tanzania yetu. Nina hakika kuwa tukikataa kuburuzwa na hawa wezi, nchi nyingi zitatuunga mkono kwa msimamo wetu na tutajijengea heshima kubwa tofauti na unavyodai. Mahakama gani itabariki vitendo vya kitapeli na wizi na kuvihalalisha kwa sababu ya kuwa huduma ilipatikana, huu ni ujuha wa sheria.
Dowans ni Kikwete first and foremost ndipo wanafuatia hao wabia wake kina Rostam, Lowassa, Karamagi and the rest of the gang of thieves. Mtakuja wengi humu na mtatetea hadi mtokwe povu lakini mkae mkijua kuwa mmeisha kilukoroga na sasa mkae tayari kulinywa pamoja na machungu yake. Kikwete atazunguka dunia nzima, atasuluhisha hadi waChechnya lakini mwisho wa safari ajue tunamsubiri atupe maelezo kwa nini mchana anafuja hela zetu kwa kuwalipa matapeli halafu usiku anatembeza bakuli kama Matonya akiomba msaada. Imefikia mahali mtu unasita kutaja taifa lako, no enough is enough Kikwete must go - ni ama yeye au sisi wazalendo !