AMARIDONG
JF-Expert Member
- Jun 24, 2010
- 2,502
- 180
Baada ya kuupitia vizuri mkataba wa TANESCO na Richmond wa June 2006, na baadaye nikaupitia mkataba wa Dowans na TANESCO wa December 2006, pamoja na madudu yote ambayo Richmond waliyafanya dhidi ya TANESCO, bado kulikuwa na concert ya Waziri na serikali, hata kama tunasema Richmond walihamisha mkataba kwenda Dowans bila kuwaeleza TANESCO. Si kweli kwani Waziri Karamagi alikubaliana na Richmond.
Jambo la pili na muhimu ni kwamba nimepitia hukumu ya ICC kwa mapana yake na kipengele kimoja ambacho waamuzi wa ICC wanakishikilia bango ni kuwa Dowans waliperfom na TANESCO walipokea umeme wa Dowans.
Hili ni la muhimu na Watanzania wanatakiwa kujua hata kama mkataba wa TANESCO na Dowans ulikuwa sio halali, bado unawishwa kuwa halali kwa sababu ya TANESCO kupokea umeme wa Dowans. Kama TANESCO wasinglipokea umeme wa Dowans basi mkataba ungekuwa batili, lakini as long as the Dowans performed and TANESCO received those whether one or hundred megawatts, maana yake ni kuwa kulikuwa na mkataba halali na TANESCO kuuvunja ilikuwa ni batili.
Kwa ushauri wangu, serikali iwalipe Dowans hizo bilioni lakini sasa irudi kwa Kina Karamagi na wengine wote waliohusika kuirubuni TANESCO wakamatwe, wafilisiwe na wawekwe ndani. Huu uwe mfano.
Angalizo: Kama TANESCO na serikali yetu ikikataa kuwalipa Dowans, balozi zetu nje ya nchi zitakuwa attached na mwisho wa siku tutawalipa kwa riba kubwa sana.
Watanzania, msioogope kuwalipa Dowans bilioni 94, hao Dowans wameshalipwa zaidi ya bilioni 172 mpaka sasa kwa ajili ya mitambo waliyoinunua kwa shilingi bilioni 60. Nchi hii ina hela nyingi sana, kazi yetu tunatakiwa kuwadhibiti wale wanaotumia fedha zetu vibaya.