AMARIDONG
JF-Expert Member
- Jun 24, 2010
- 2,502
- 180
- Thread starter
- #21
Mkuu Son of Soil nimekusoma na nimeona Logic yako, lakini hatuwezi kuuacha ukweli eti kwa sababu Dowans walizalisha na kuuza umemem kwa TAnesco
Mkuu hoja inarudi nyuma kabisa na wala sheria haianzi juu kuja chini bali inaanza chini kuja Juu
Richmond walishakiuka masharti ya mkataba, Wao waliingia Ubia na Dowans Bila kuwashirikisha Tanesco ikiwa na maana kuwa huo Mkataba kati ya Dowans na Richmond ni batili, kwa hiyo Dowans Amekuja Tanesco kama mtoto HAramu amepewa nguvu na Richmond bila kumshirikisha Upande wa Pili, hicho kifungu kinainyima Dowans Haki ya kulipwa chochote hata kama walizalisha na kuuza umemem kwaTanesco
SAHIHI NDUU KITUKO EMBU TUJIKUMBUSHE KIDOGO RIPOTI YA BUNGE AMBAYO INAONYEHS TANESCO WALIINGIA MKATABA HALALI NA DOWANS JAPO KWA KUSHURUTISHWA NA WIZARA,NA HAPA MIMI NDIO NASEMA HAWA WALIOIPOTOSHA TANESCO TUWAFILISI,TUWAFUNGE ILA DOWANS WALIPWE HARAKA KUEPUSHA BALAA ZAIDI
Ripoti ya Mwakyembe inasema kuwa
"Tarehe hiyo hiyo 28 Novemba 2006 uongozi wa TANESCO ulimshauri Mwenyekiti wa Bodi kama ifuatavyo:-
(i) Mkataba kati ya Richmond Development Company LLC na TANESCO hauruhusu kukabidhi majukumu ya Mkataba kwa Kampuni nyingine isipokuwa kwa maafikiano ya pande mbili za
Mkataba (Kifungu 15.12)." Tarehe 4 Disemba, 2006 (chini ya siku kumi tangu Karamagi adokeze nia ya Richmond kuhamisha mkataba)
TANESCO walipokea barua kutoka Richmond ambayo ilionesha kuwa kampuni hiyo ilitaka "kutumia haki yake chini ya Kifungu 15.12 cha Mkataba ili kuhamisha majukumu yake yote ndani ya Mkataba huo kwenda kwa DOWANS Holdings, S.A. Aidha, Richmond Development Company LLC ilieleza kwamba tarehe ambayo TANESCO itaridhia mapendekezo hayo iwe ndiyo tarehe rasmi ya kuhamisha mafao na majukumu yote kwa DOWANS Holdings, S.A na kwamba DOWANS Holdings, S.A itawasilisha vielelezo vya utambulisho wake kwa TANESCO"
Hata hivyo, barua hiyo ambayo TANESCO waliipokea Disemba 4, inaonesha kuwa iliandikwa Novemba 9, karibu mwezi mmoja kabla. Siku moja kabla ya kupokea barua ya Richmond kutaka kuhamishia mkataba wake kwa Dowans yaani tarehe 8 Disemba, 2009 TANESCO ilikuwa imeiandikia Benki ya Citibank isaidie kufanya uchunguzi wa kujua kampuni ambayo Richmond ilikuwa inataka kuhamishia mkataba wake ilikuwa ni kampuni gani na yenye uwezo gani kwani japokuwa masharti ya Mkataba yanaruhusu Mkataba kuhamishwa, TANESCO ingependa kufahamu hasa ni nani anayehamishiwa Mkataba huo"
Kamati Teule haikufanikiwa kupata majibu ya Citibank ila iliambiwa kulikuwa na shinikizo toka Wizarani "kuwa viongozi wa Wizara kama kawaida yao waliishinikiza TANESCO kukubaliana na ombi la Richmond Development Company LLC la kuhamisha mkataba." Ni kutokana na hilo tarehe 21 Disemba, 2006 TANESCO ikaiandikia kampuni ya Richmond kukubali uhaulishaji wa mkataba huo kwenda kwa Dowans kwa barua yenye SEC. 388/12/206 ambapo pamoja na mambo mengine ilitaka "ipate hati ya uthibitisho kutoka Dowans Holdings, S.A ya kuridhia uwajibikaji kamilifu katika kutekeleza Mkataba wa tarehe 23 Juni, 2006, kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC."
Hivyo tarehe 23 Disemba 2006 Mkataba ukaingiwa kati ya TANESCO na Dowans S.A ambao ulikuwa ni kuhamishia mkataba kati ya TANESCO na Richmond kwenda kwa Dowans Holdings S.A.
Kwa mujibu wa ripoti ya Kamati Teule kusainiwa kwa mkataba huo kati ya TANESCO na Dowans Holding S.A kulileta mambo matatu muhimu ;
-"Tarehe 23 Disemba 2006 ndiyo siku rasmi ambayo Richmond Development Company LLC imekabidhi rasmi majukumu yake ya utekelezaji wa Mkataba kati yake na TANESCO kwa Dowans Holdings S.A";
- "Dowans Holdings, S.A itatekeleza majukumu ya Mkataba uliotiwa saini kati ya TANESCO na Richmond Development Company tarehe 23 Juni, 2006 kwa masharti yote kama yalivyo katika Mkataba";
- "Malipo halisi na madeni ndani ya Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC, sasa yatakwenda kwa Dowans Holdings, S.A kuanzia tarehe 23 Disemba, 2006."