Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
KWA USHAURI WANGU,SERIKALI IWALIPE DOWANS HIZO BILLION LAKINI SASA IRUDI KWA KINA KARAMAGI NA WENGINE WOTE WALIOHUSIKA KUIRUBUNI TANESCO WAKAMATWE,WAFILISIWE NA WAWEKWE NDANI HUU UWE MFANO.
Serikali ni nani na kina Karamagi ni nani! Serikali = Kina Karamagi (Hapa neno Karamagi linawakilisha 'Mafisadi'. Hakuna mtu anaweza kujiadhibu.
Watanzania tunapiga kelele sio ili Dowans wasilipwe, bali tunakataa mchakato mzima wa Richmond na Dowans. Hakuna njia nyingine ya kuonyesha kuwa tunalaani Serikali kwa mikataba ya aina hii, zaidi ya kupiga kelele kuwa Dowans wasilipe. Mwisho wa siku serikali italipa, lakini italipa ikijua kuwa at least huu wizi wa sasa haukufanyika kirahisi kama walivyotaka (kama wanajali). Tunajua kuwa ni kwa kelele za namna hii masikio ya watanzania wengi ambao bado wamelala yatafunguka na wataamka. Tunajua mafisadi CCM kwa hili la Dowans watazidi kujiweka pabaya. Huu ni mtaji kwa wanamabadiliko wote, na wanatakiwa wachange karata zao vyema hapa, hakuna kulegeza kamba.
Nakumbuka maneno ya Mtikila kuwa "Dowans imeshushwa na Mungu kumuondoa Kikwete"