ACHA KULALA SOMA MAMBO NA UYAELEWE KESI ILIYOFUNGULIWA NDIO HII HAPA CHINI ISOME NA UONE KAMA KUNA POINT HATA CHEMBE NI SIASA TUPU NA BLAA BLAA NYINGI HAPA HAMNA HATA REF,SECT,AU HATA ARTICLE ZA CONTRACTS HAMNA HATA CASEPRESEDENT HAWA WANATANIA SOMA HUU UPUPU HAPA UNIAMBIE UNA NAFASI GANI KWENYE ILE HUKUMU YA DOWANS
UPUPU WA WANAHARAKATI;
1: Kwamba Bodi ya Zabuni ya Tanesco (TTB) ilikuwa na watalaam weledi katika kufanya kazi ya kuchambua zabuni, na kwa hakika huko nyuma ilikwisha kufanya kazi nyingine nyingi. Kwa maana hiyo kama kulikuwa na wasiwasi juu ya uwezo wa TTB katika suala zima la mkataba wa Richmond, basi ingebidi kupitia zabuni zote za huko nyuma na si wa Richmond pekee;
2: Kwamba kamati iliyoundwa na Wizara ya Nishati na Madini kupitia mchakato wa kufungwa kwa mkataba wa Tanesco na Richmond iliundwa nje ya utaratibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (PPA);
3: Kwamba Tanesco ilishughulikia vilivyo zabuni ya Richmond kitaalam na kufikia hitimisho kuwa kampuni hiyo, haikuwa na uwezo wa kitaalam wala wa kifedha kufanya kazi hiyo. Richmond haikuwa na historia (rekodi) ya kufanya kazi kama hiyo walioyokuwa wameomba kama moja ya sharti mojawapo la msingi la kupata zabuni hiyo ambalo liliwekwa kwenye tangazo la kuomba kazi kama hiyo (kuzalisha umeme) na angalau kuwa na mtaji wa Dola za Marekani milioni tano (wakati huo Sh. bilioni tano).
4: Kwamba hata pale kazi ya kutafuta mzabuni wa kufanya kazi ya kuzalisha umeme megawati 100 ilipochukuliwa na Wizara ya Nishati na Madini, haikufanywa na Bodi ya Zabuni ya wizara hiyo, kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria ya PPA.
5: Kitu pekee kilichorejesha mchakato wa zabuni hiyo kwa Tanesco ni kutafutwa kwa saini ya kiongozi wa Tanesco ambaye hata hivyo alilazimishwa kusaini baada ya kuambiwa kwamba kama akikataa kitu chochote kingeweza kumpata;
6: Kwa maana hii basi, mchakato wote ambao uliishia kuipa Richmond kazi ya kufua umeme wa megawati 100, ulifanyika bila kuitishwa kwa zabuni kwa mujibu wa sheria ya PPA, lakini pia bila kushirikisha mamlaka zozote ambazo kisheria zinawajibu wa kushughulikia zabuni hizo, yaani Bodi ya Zabuni ya Wizara au Bodi ya Zabuni ya Tanesco (TTB);
7: Kwamba uchunguzi wa Kamati teule ya Bunge na ule wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), uligundua kuwa Richmond haikuwa ni kampuni iliyosajilia kama jina lake lilivyokuwa linasema na hata jina la RDEVCO LLC ambalo pia Richmond ilikuwa inajitambulisha kwalo, ilikuwa ni kampuni nyingine tofauti kabisa na Richmond iliyoomba kazi ya kufua umeme nchini;
8: Kwamba Richmond ilitoa anwani sawa na ile ya RDEVCO, lakini ofisi zao zilipotembelea na Kamati ya Bunge, iligundulika kwamba (RDEVCO) haikuwahi kufanya shughuli yoyote ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia na kwa maana hiyo haikuwa na ujuzi wala fedha za kuweza kutekeleza kazi hiyo iliyoomba;
9: Kwamba TTB yaani Bodi ya Zabuni ya Tanesco ilikuwa sahihi kabisa kwa kutupilia mbali maombi ya Richmond katika kutekeleza kazi hiyo, kwa kuwa haikuwa na uwezo na haikukidhi masharti ya tangazo la zabuni la kazi ya kuzalisha umeme wa dharura wa megawati 100;
10: Kwamba Wizara ya Niashati na Madini iliishinikiza TTB na Bodi ya Tanesco kuvunja sheria kwa kupunguza siku za kutangaza zabuni kutoka 45 hadi 20; lakini utarartibu unaokubalika na PPA wa ama kutafuta kampuni ya kimataifa (International Shopping au Single sourcing) ukiwekwa kando, kwa kuwa katika utaratibu huu Tanesco ingewajibika kutafuta kampuni yenye historia ya kufanya kazi ya kuzalisha umeme wa dharura ambayo Richmond moja kwa moja isingefikiriwa kwa kuwa ilikwisha kujuliakana haina uwezo;
11: Wizara ya Nishati na Madini ililazimisha Tanesco na Bodi ya Tanesco ibadili zabuni iliyokataliwa yaani Richmond kuwa iliyokubaliwa licha ya kuwepo kwa vigezo vya dhahiri kabisa, kitaalam na uwezo wa fedha, ambavyo vilikuwa vimekwisha kumweka kando Richmond; kwa kufanya hivyo sheria ya PPA ilivunjwa;
12: Kwamba kamati iliyoundwa na Wizara ya Nishati na Madini kushughulikia zabuni ya Richmond, haikuwa na mamlaka ya kufanya kazi hiyo, ilivunja sheria ya PPA hata kama ilikuwa imechukua wataalam kutoka Tanesco na Wizarani.
13: Kwamba kamati hiyo, yaani ya wizara, ilifanya mchakato wa zabuni wa kufufua umeme wa megawati 100 ambao ushindi alipewa Richmond, kwa kutumia nyaraka ambazo Bodi ya Zabuni ya Tanesco ilikwisha kuzifuta kwa kuwa Richmond ilishindwa kutumiza matakwa ya tangazo la zabuni;
14: Kwamba Richmond aliruhusiwa kuwasilisha nyaraka nyingine za ziada kwenye kamati ya Wizara, ambazo hazikuwa kwenye zabuni iliyotangazwa Februari 27, 2006 na kisha Richmond ikashindwa; kwa kifupi kulikuwa na utaratibu wa makusudi wa kuhakikisha Richmond inashinda;
15: Kwamba wakati Richmond ilisajili jina la RDEVCO LLC Machi 2008 hii ilikuwa ni baada ya matukio mawili, kwanza baada ya kuwa imekwisha kuingia mkataba na Tanesco Juni 23, 2006 kwa bosi wa Tanesco kutishwa ili asaini, lakini pia baada ya Dowans kuwa amekwisha kuchukua mkataba huo; Lakini pia jina hilo halikusajiliwa kwenye mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura uliofikiwa Juni 23, 2006.
16: Kwamba Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ilithibitisha pasi na shaka yoyote kwamba mchakato wa ufungaji wa mkataba wa Richmond na Tanesco ulikiuka sheria ya manunuzi ya umma;