Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,361
- 2,734
Ndugu wana JF,
Naomba mnisaidie kwa tatizo ninalonipata kichwani mwangu hasa baada ya kuwa hivi juzijuzi nimejua kusoma na kuandika. Nadhani mtanipa msaada kwa moyo mmoja baada ya kuwa nimeeleza kiwango changu cha uelewa na elimu yangu. Hii ni kuhusu mimi mtoa mada:-
Elimu ya msingi - Nilifeli vibaya sana na nilikuwa wa pili kutoka mwisho Ki- mkoa huko Shinyanga
Sekondari - Kwa vile wazazi wangu walikuwa wakulima na wafuga kuku waliamua kunipeleka Sekondari angalau nisiwe kama wao, walau nijue gudi moningi. Nilipata division 0 ya points 35.
High Level - Kwa sababu wazazi wangu walikuwa na moyo walinipeleka A - level ya binafsi ili niwe nasoma wakati nikitafuta CREDIT 3 ili niweze kufanya mtihani wa form Six. Nimemaliza miaka 6 nasoma kutafuta Credit lakini zimegoma. Miaka 6 yote nimeambulia D ya Uraia. Angalau najua haki zangu kiasi. Na sasa naona nimejua kusoma na kuandika na ndio niko kwenye peak japokuwa nimeamua kurudi kijijini kwetu Bubuga nalima mbogamboga.
Sasa pamoja na uelewa wangu kuwa mdogo, kijijini kwetu yamekuwa yakifika magazeti kadhaa likiwemo mwana halisi na mengineyo na vilevile tuna viredio ambavyo huvitumia kusikiliza taarifa mbalimbali zikiwemo hotuba za Raisi. Kama hayo magazeti na Redio hazikudanganya,.......
Nimesikia kauli hizi hapa:----
Raisi : Siijui Dowans na wala sijui wamiliki wake
Serikali : Haiijui Dowans maana kiongozi mkuu haijui
Wananchi : Jamani hivi Dowans ni nani, majibu kutoka serikalini : Hatuwajui!!!!!
Tena Raisi aliwahi kusema ; Hajui kwa nini Tanzania ni Maskini!!!
Kauli ya Sasa Hivi : - Serikali na CCM wanasema lazima Dowans ilipwe, Nimezima redio weeeeee, lakini magazeti yameandika, Mahakama inasema Dowans lazima ilipwe. Hapa mimi mwenzenu nimekwama. Naombeni wana Jf wenzangu wenye uelewa na akili timamu, labda mie kwa vile nilifeli kiasi hiki inawezekana ni jibu jepesi ila mimi sijui. Nisaidieni jamani nisaidieeni. Nawaaminia wasomi wa nchi hii akiwemo Raisi hebu nisaidieni mie Education background yangu mmeiona. Nyie wenye akili nisaidieni. Huyo ambaye humjui unafikiaje hatua ya kumlipa bila kuwaomba radhi wananchi kuwa unamjua ila ulikuwa unavunga???????? Unataka kumlipaje kiasi kikubwa hivi ambaye humjui na wewe ni maskini na hujui kwa nini wewe ni maskini na umepata wapi fedha za kumlipaaaa??????? AAgghhh?!!!!!,..,.,.<>>_+": Nawasilisha.