[DOWANS] JK: Siijui, Serikali: Siijui, Wananchi: Hatuijui! Serikali: Lazima walipwe DOWANS! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

[DOWANS] JK: Siijui, Serikali: Siijui, Wananchi: Hatuijui! Serikali: Lazima walipwe DOWANS!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Oct 12, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana JF,
  Naomba mnisaidie kwa tatizo ninalonipata kichwani mwangu hasa baada ya kuwa hivi juzijuzi nimejua kusoma na kuandika. Nadhani mtanipa msaada kwa moyo mmoja baada ya kuwa nimeeleza kiwango changu cha uelewa na elimu yangu. Hii ni kuhusu mimi mtoa mada:-

  Elimu ya msingi - Nilifeli vibaya sana na nilikuwa wa pili kutoka mwisho Ki- mkoa huko Shinyanga

  Sekondari - Kwa vile wazazi wangu walikuwa wakulima na wafuga kuku waliamua kunipeleka Sekondari angalau nisiwe kama wao, walau nijue gudi moningi. Nilipata division 0 ya points 35.

  High Level - Kwa sababu wazazi wangu walikuwa na moyo walinipeleka A - level ya binafsi ili niwe nasoma wakati nikitafuta CREDIT 3 ili niweze kufanya mtihani wa form Six. Nimemaliza miaka 6 nasoma kutafuta Credit lakini zimegoma. Miaka 6 yote nimeambulia D ya Uraia. Angalau najua haki zangu kiasi. Na sasa naona nimejua kusoma na kuandika na ndio niko kwenye peak japokuwa nimeamua kurudi kijijini kwetu Bubuga nalima mbogamboga.

  Sasa pamoja na uelewa wangu kuwa mdogo, kijijini kwetu yamekuwa yakifika magazeti kadhaa likiwemo mwana halisi na mengineyo na vilevile tuna viredio ambavyo huvitumia kusikiliza taarifa mbalimbali zikiwemo hotuba za Raisi. Kama hayo magazeti na Redio hazikudanganya,.......

  Nimesikia kauli hizi hapa:----

  Raisi : Siijui Dowans na wala sijui wamiliki wake

  Serikali : Haiijui Dowans maana kiongozi mkuu haijui

  Wananchi : Jamani hivi Dowans ni nani, majibu kutoka serikalini : Hatuwajui!!!!!

  Tena Raisi aliwahi kusema ; Hajui kwa nini Tanzania ni Maskini!!!

  Kauli ya Sasa Hivi : - Serikali na CCM wanasema lazima Dowans ilipwe, Nimezima redio weeeeee, lakini magazeti yameandika, Mahakama inasema Dowans lazima ilipwe. Hapa mimi mwenzenu nimekwama. Naombeni wana Jf wenzangu wenye uelewa na akili timamu, labda mie kwa vile nilifeli kiasi hiki inawezekana ni jibu jepesi ila mimi sijui. Nisaidieni jamani nisaidieeni. Nawaaminia wasomi wa nchi hii akiwemo Raisi hebu nisaidieni mie Education background yangu mmeiona. Nyie wenye akili nisaidieni. Huyo ambaye humjui unafikiaje hatua ya kumlipa bila kuwaomba radhi wananchi kuwa unamjua ila ulikuwa unavunga???????? Unataka kumlipaje kiasi kikubwa hivi ambaye humjui na wewe ni maskini na hujui kwa nini wewe ni maskini na umepata wapi fedha za kumlipaaaa??????? AAgghhh?!!!!!,..,.,.<>>_+": Nawasilisha.
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Jamani nasubiri msaada
   
 3. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  aisee, kaaazi kwelikweli
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hapo nadhani umeshamaliza kila kitu kwani mkuu wa kaya lazima ataishia kusema hivyohivyo au akamwiga nape..
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hee interesting..
   
 6. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hilo tu hata umasikini wetu hawaujui
   
 7. W

  Welu JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Ukiona hata rais mwenye vyombo vya upelelezi hajui, basi hata sisi hatuwezi kuijua.
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Kwakua hujui kusoma na wala kuandika kama mimi basi tufanye hivi; kesho kutwa tuingie barabarani mimi na wewe! ili tukafundishwe kusoma na kuandika na namna ya kutamka Do-once!
   
 9. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,959
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Aaah JK atoe tamko.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nadhani ata tutakayemlipa pia hatumjui
   
 11. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kweli kazi tunayo na hii serikali ya Magamba..mpaka tuiondoe madarakani itakuwa imeshamaliza kuuza kila kitu nchini .
   
 12. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ninyi ni wazushi, kwani hapa ninani kawaandikia na kuwasomea?
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pole sana mkuu wangu ndio tumeliwa, Wadanganyika leo wanatafuta kujifunika blanketi wakati kumekucha!..
   
 14. j

  jigoku JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kama hajulikani nani aliandikisha kesi na nani atalipwa? na mlipaji ni masikini.bwana eee,huu ni usanii na ndo maana ni vema tukatae ili watakaopingana nasisi tunaoandamana tuwaulize mnamtetea nani ili alipwe?maana porojo zimezidi.
  pole sana kwa kutojua kusoma ila uko updated
   
 15. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  na hayo malipo wanampa nani? au wanayatoa kama tambiko?
   
 16. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Sasa ukiona hivyo ujue wewe unaakili kuliko serikali ikiongozwa na raisi wao. . Ni upupu uliopindukia
   
 17. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waanze Bakwata
   
 18. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Sijuhi
   
 19. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,212
  Likes Received: 10,549
  Trophy Points: 280
  du! nashindwa nikusidiaje lakini na ungana na muheshimiwa hapo juu hebu tutoke barabarani hiyo tarehe 14/10/2011 halafu utajua ni nani aneyelipwa hizo pesa zote! sawa
   
 20. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #20
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Shukrani sana wazee wanguu, Serikali si itoe walau tamko kama tunaisingiziaaaaaa???

  Naungana na Dr Slaa lazima tuandamane tarehe 14 hiyo lazima. Kama ni bustani yangu ya mboga nitamwagilizia maji mengi siku moja kabla ili niingie mtaani
   
Loading...