Sakata la TANESCO, Mheshimiwa Rais, tunaomba utoe kauli... wananchi tumechoka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la TANESCO, Mheshimiwa Rais, tunaomba utoe kauli... wananchi tumechoka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masanja, Dec 30, 2010.

 1. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Nimeisoma hukumu ya ICC/msuluhishi/arbitrator kati ya TANESCO na DOWANS lakini kwa mtu yeyote mwenye uelewa wa sheria, ni hakika facts zote hazikutolewa. Na nina mashaka kwamba kulikuwa na collusion kati ya mshtaki na mshtakiwa..(walikuwa kitu kimoja)..ilmradi hiyo pesa ilipwe na hela za walipa kodi. Maana ile decision ukiisoma unaona kwamba wahusika walifanya njama. Yaani ni yale yale ya Radar na ile hukumu ya juzi pale London (maana BAE walikubali kosa through plea bargaining na kulipa faini..ilmradi mahakama isiandike kwenye hukumu neno "corruption"..yet kwetu huku Tanzania tumeambiwa vingine kabisa!. Nitajitahidi kuzi-summarize niziweke hapa kwa lugha rahisi wananchi mzisome. Maana nadhani watu tumeshafanywa wajinga kabisa as if hatukwenda shule.

  From my judgement..huu mkataba (TANESCO na DOWANS) haukuwepo..PRECISELY BECAUSE THE CONTRACT WAS BUILT ON ILLIGALITY..WHICH NULLIFIED ITS ENFORCEABILITY FROM THE TIME IT WAS CONCLUDED. Na uwezo wangu mdogo lakini naelewa kabisa..kama mkataba umeafikiwa kwa hila au udanganyifu hauwezi kuwa mkataba halali.....Clearly, Mwakyembe alituandalia report. (ambayo ilimuondoa Lowassa).....na wengi tuliisoma..tunajua kabisa Richmond haikuwepo..ilikuwa ni kampuni hewa. Kwa hiyo isingeweza kurithisha mkataba kwa DOWANS kwa sababu tayari huo mkataba haukuwepo kisheria! Huhitaji PhD ya International Law kutoka Stanford au Cambridge kulijua hili. Nina imani hata WEREMA analitambua hili..ila anacheza na fikra zetu watanzania.

  Mwanzoni wengi tulikaa kimya kwa sababu tulijua ni mambo ya kisheria yatamalizwa kisheria. Lakini ukweli ni kwamba, its politics vs. politics. Yaani hapa..kesi ya TANESCO ilikuwa rahisi sana. Maana wale waliosign mkataba walidanganya from the biggining..kitu ambacho hata polisi ni kosa la jinai. Unfortunately nilichogundua it is highly likely huu mkataba ni " deal" la watu kwenye "system". Lakini kinachouma ni kwamba..wanaoumia ni sisi wananchi wa kawaida..ambao tunahangaika kila kukicha na haya maisha kwa sababu ya watu wachache sana. Mimi nadhani kwa kweli serikali yetu na wanasheria wetu hawajatutendea haki kabisa they should be ashamed of themselves. I have read the judgement na naona TANESCO wanted to loose from the beggining.

  Hivi kweli kama taifa ambalo kila siku tunashinda kuomba vyandarua vya malaria....kwa akina Ray Chambers....tumeamua kuukubali huu udhurumaji kirahisi rahisi hivi? Hivi ni kweli tumekubali kulipa Billion 185 (na kuendela mpaka deni litakapolipwa) kwa Kampuni hewa? Mimi naomba viongozi wetu especially Raisi wetu na wabunge waache mzaha...This is serious its not politics anymore..its about the survival of the nation and its people. Na huu umasikini unaotukabili ni dhihaka ya hali ya juu kuambiwa tulipe hizo billions wakati hata sasa umeme hatukupata na wala mpaka leo hatuna! Jamani hivi viongozi wetu kwa nini wanakuwa wagumu kuelewa au wanafanya maksudi? Please Kikwete stop this! It pains. To all men and women in this poor country called TANZANIA.

  Kwanza kabisa hii Kampuni hatujui mmiliki wake..kila mtu hata RAIS wetu wako kimya kuhusu nani mmiliki halali wa hii kampuni, sasa hiyo hela tunamlipa nani? Au viongozi wetu wamekula njama ya kutudhulumu sisi raia? Wanachokifanya ni kutwambia mjadala umefungwa? Jamani hizo pesa ni kodi zetu tuna kila haki ya kuhoji matumizi yake. Na hii siyo kutafutana ugomvi. Ni haki yetu ya kiraia kabisa. Sisi kama raia wa Tanzania TUNAHUKUMIWA kwa sababu eti tulivunja mkataba wa kufua umeme. Lakini tuliuvunja na nani? huyo mwenye kampuni kwa nini asijitokeze hadharani? Sisi wananchi ambao tunalala gizani tukamuuliza maswali? Maana viongozi wetu wana majenereta hawajui dhahma na kero ya huu umeme wa Tanzania. Cha kusikitisha zaidi huo umeme hatukupata hata wa kuwasha balbu moja ya jikoni! Leo tunaambiwa tulipe hayo mabilioni kwa taifa ambalo halina nyuma wala mbele.

  Jamani mimi nadhani Watanzania sasa tuache ushabiki wa kisiasa tujipange kuuliza maswali magumu kwa hawa watawala wetu ambao wanaiendesha nchi yetu kama kampuni binafsi ya Mohamed Enterprises. Its tragic kweli kabisa sisi kama taifa kusimama na kusema kwamba tuna uhuru wakati hatuwezi hata kuamua au kutambua kipi kinatufaa kipi hakitufai.Inauma Kuona kwamba wale tunaowaamini ndo wanatuzunguka na kutufanya sisi ni wajinga. Nimemsikiliza Werema Jaji Mkuu..nimesikitika sana...kuona mwanasheria mkuu kama yeye anaweza toa kauli kama zile as if haijui sheria. Watu tunaweza kuwa na imani tofauti ya kisiasa. Lakini kuna mambo ambayo lazima tufike mahali tuyapiganie kwa maslahi ya hili taifa letu.

  As we move forward nategemea Rais wetu atakuja na kutoa kauli thabiti dhidi ya huu udhurumaji wa mchana kweupe...Please Mr. President..stand up and be counted....tunalalamika kila siku mikataba mibovu..but ultimately the buck stops at your table..maana wewe ndo kiranja mkuu na baba mkuu mwenye nyumba.

  Kama vipi..mimi nitajitolea BURE kuandika LEGAL OPINION kwenye hii HUKUMU YA ICC kati ya DOWANS na TANESCO kumshauri Rais wetu afanye nini baada ya hapa.... Kama aliyepewa hilo Jukumu haliwezi. I am ready to do it..for the sake of my country and its people. Tunasoma tuwezi kulisaidia taifa letu. Sasa kama hatuwezi hata kutetea maslahi ya taifa at its hour of need, ni usaliti.

  I challenge my fellow compatriots. Lets stand up and say no to this day time robbery of our hard earned shilling.
   
 2. F

  Fareed JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ijumaa, tarehe 31 Desemba 2010, huenda Rais Kikwete atahotubia taifa kwa TV ikiwa ni hotuba yake ya mwisho wa mwaka. Kwa jinsi nilivyomsoma Kikwete kwa miaka 5 iliyopita, atazungumzia uchaguzi wa 2010 umekwisha, life goes on. Atasema taifa linahitaji ku-heal kutokana na majeraha ya udini ya uchaguzi. Atazungumzia kilimo kwanza, safari zake za nje kuomba misaada ya vyandarua na chakula. Ataipongeza pia Taifa Stars kwa kushinda kombe la challenge. Atatangaza mkakati wake wa kuwainua wasanii wa bongo fleva na movie za Tanzania. Atasema uchumi unapaa na mfumuko wa bei umedhibitiwa. Atalaumu mdororo wa uchumi, ukame na bei za mafuta duniani kuwa chanzo cha serikali kutotimiza ahadi zake. Atawakumbushia Watanzania kauli yake kuwa foleni za magari Dar ni ishara ya maisha bora.

  Hatazungumzia masuala makubwa ya kitaifa yaliyopo sasa hivi -- kama vile ufisadi mkubwa wa kuitaka serikali iilipe Dowans (Rostam Aziz) 185.5 billion shillings, kuongezeka kwa bei ya umeme, mgao unaoendelea wa umeme, madai ya katiba mpya, taarifa za WikiLeaks kuwa yeye Kikwete hataki Mkapa na vigogo wengine wachunguzwe kwa tuhuma za ufisadi, hali ya umasikini kuzidi, vijana wa taifa kukata tamaa na maisha, kuchunguzwa kwa matokeo ya kura za urais, kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, wananchi kutokuwa na imani na serikali yao, etc.

  Huyu ndiyo Rais Kikwete ambaye tunaye mpaka mwaka 2015! Je, tutafika?
   
 3. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tuwekee hiyo nakala ya Hukumu ya ICC nasi wa huku mbugani tuisometuielewe maana hukumu hiyo lazima iwataje wahusika. Na kama haiwataji basi hata wewe umesoma ambayo ni feki tu.
   
 4. mwanatanu

  mwanatanu JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Jk kama nilvyoongea kwenye thread nyingi ni kuwa hatajali chochote sasa hivi kwa vile wa uhakika wa kuongoza miaka 5 ingine....jamani hamuoni ni kitu kisichomwuma kabisa. .
  rais gani anakaaa kimya wakati wa janga? Matatizo haya ya umemme ni janga je Jk kafanya nini zaidi ya kwenda Malawi kwa ajili ya uzinduzi wa kaburi ya ex first lady...jamani kweli huyu ndio rais mtategemea aongolee loloete kuhusu dowans?

  Mimi kinachonishangaz zaidi ni kuwasikia Pinda na Werema wanadiriki kusema kuwa kuwalipa ni lazima?... hakuna hata mmoja wao amekemea chanzo cha matatizo haya...bilioni 185 kwao ni vijisenti hakuna hata mmoja wao anaonyesha hata ile kahuruma ka uwongo kusema tunaibiwa wankubali Dowans walipwe ni nani huyu Dowans wanamwogopa kiasi hicho?....bil 185 ni gharama ya 185 miles ya barabara...sijui ni vitanda vingapi vya hospitali....nobody cares hawa ni WAHAINI na sisi ndio tumewaweka hapo na sasa watunyae kichwani
   
 5. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,084
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  ataka kwambia Kiherehere chenu, mwanzako anakula mayai, wala hajui if Dowans exists ( a pretender), nasema hivi kwani ange respond kama kweli ana uchungu
  na nchi hii
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Taifa hili ni la watu waliokata tamaa. Wengi hawaamini kama kuna haja ya kutetea chochote kwani wamekata tamaa. Wakipiga kura hawaoni kama matokeo yaliyotarajiwa na wengi yanatokea. Wakimsimamisha mgombea wakidhani atawatetea wanashangaa anajiondoa.
  Wakiwaona wabunge wenye mwamko na wanaotetea maslahi yao, baada ya muda wanaona wakitetea Mafisadi na kutoa ushauri wa ajabu ajabu ghafla. Wakisikia kelele za haki bungeni ghafla wanasikia mjadala umefungwa.
  Wakimtarajia Meya fulani kwa idadi halali ya kura zinazojulikana wazi wanasikia matokeo mengineyo. Wakisikia watu wamepatikana na mabilioni kwenye account zao na wameliingizia taifa hasara mara wanasikia maneno kama " Hili ni jembe la zamani" au huyu ndiye anayefaa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili ya taifa kwani ni mfano wa kuigwa. Wakisikia mtu kaua na hana Bima mara wanasikia lipa faini kidogo nenda zako.
  Wakisikia kuna tenda mahali nao wakaambatanisha kila sifa waliyonayo ya kibiashara mara wanasikia hii imepewa kampuni mashuhuri ya ---- ghafla wanashtukia ni kampuni ya mtoto wa kigogo aliyemaliza chuo kikuu miaka si mingi lakini ana uwezo wa mabilioni ya pesa na kampuni nzuri tu inayoweza kushinda tenda ya mabilioni.
  Wakisikia kuna vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa kubwa mara wanasikia waliowatuhumu au kuwakamata wakifukuzwa kazi.
  Wakisikia chombo cha habari cha serikali kilipendelea chama tawala, wakati wanatarajia marekebisho na haki sawa wanasikia " wewe uliyekuwa mkurugenzi ondoka kwani hukupendelea chama tawala vya kutosha."
  Wakisikia ameteuliwa Mkurugenzi wa TAasisi ya KUkamata na KUgawana RUshwa mara wanashangaa kaamriwa usije kukamata na kugawana ya wakubwa, kamata hawa wanaowahonga polisi.
  ILI MRADI UTAWALA ADILIFU NA SHERIA HAUPO , BASI MWANACHI WA KAWAIDA HAJUI ATARAJIE NINI. Imegeuka siasa ya sasa kuwa ni ya UNYAMA NA KUJITEGEA. Na wengine wanafuata ya UJIMA NA KUJIMEGEA. Huhitaji kuwa nabii kutabiri kuwa Serikali inaendelea kuondoa amani na utulivu kwa matendo mengi yasiyo ya haki. HAKI IKIONDOKA AMANI INAONDOKA.
  Hivyo watu wameacha mambo yaende yanavyoenda kwani hawaoni kama kuna mabadiliko na hata nia ya kuyaleta.
  Mungu akusadie utetee hata kama ni wewe mmoja tu. Tutakuunga mkono na tutasimama hata kama ni wawili tupige kelele. Historia itatukumbuka ili kuliondoa taifa hili katika utumwa huu mpya na mbaya zaidi.
   
 7. c

  chamajani JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Iweke hiyo Legal Opinion wana JF waiboreshe zaidi then tumpe Malaria Sugu amfikishie mkulu na ampige picha wakt wa kumkabidhi.
   
 8. c

  chamajani JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, unachosema ni true prediction, hatozungumzia issue hizo, si unakumbuka majibu aliyotoa pale alipoulizwa hali ya nchi ameionaje baada ya kuzunguka nchi nzima katika kipindi cha campaign-Jamaa tu msanii mpaka anaboa ile mbaya
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Masanja, machungu uliyo nayo katika hili swala ni makubwa, lakini kaa ukijua kuwa si.wewe pekee, tupo wengi na wengi wataongezeka kwa machungu ya mgao wa umeme yaliyopo. Basi kama tutaacha usahaulifu, wahujumu uchumi waliosababisha haya yote watacheka leo lakini kesho machungu yatakuwa kwao!
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu Masanja..............RA ana Power of Attorney ya DOWANS........alirithishwaje mkataba feki/hewa...........only God Knows.............

  Namchukia Mugabe kwa matendo ya kijinga aliyofanya kule Zimbabwe.........lakini kusema ukweli...........Steve Dii alisema tunahitaji mtu kama Mugabe kufanya maamuzi magumu.............nina hakika hata JKN RIP asingekubali huu upuuzi unaotokea kwenye hii kesi...........viongozi wetu bado hawaoni...........nini maana ya Taifa....tena lenye rasilimali kama Tanzania..............
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahah,am so gladay,ulichokiongea ndo kimezungumzwa na mumewe salma
   
 12. britanicca

  britanicca JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2017
  Joined: May 20, 2015
  Messages: 3,066
  Likes Received: 3,570
  Trophy Points: 280
  Icc
   
Loading...