Mhe. Rais wanaotishia Utawala wako ni Hawa...

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Shikamoo Mkuu! (Sijui hata kama una kawaida ya kusoma JF au la! Naomba walau Tiss wakufikishie ujumbe wangu) maana inadaiwa JF ni ya Chadema lakini na sie tunaitumia.

Nimesikitika sana kutokana na ulivyoupokea mwito wa Chadema kukutaka utoe tamko kuhusu malipo ya DOWANS ama u-face nguvu ya Umma.

Yaani na nguvu zote zinazokuzunguka bado unahofia uwezekano ("wa kufikirika") wa kukuondoa madarakani Mzee? Tena jambo la kusikitisha unadhani uchochezi wa CDM utapata nguvu ya kuleta machafuko hapa nchini kiasi cha kuing'oa serikali yako halali (inayoongozwa kwa remote na RA) madarakani? Pole sana kwa mshtuko kama ulipata kweli. Naomba kupitia fursa hii nikupe dodoso kidogo.


Chadema kama chama (pamoja na kuwasingizia udini) hawana jeuri ya kukutisha wala kukuondoa madarakani. Kwa uchambuzi makini, kama rafiki zangu wakusanya habari muhimu za taifa watafanya kazi yao kwa makini watagundua kwamba maadui wakubwa na wanaotishia madaraka yako ni hawa wafuatao na sababu za wao kufanya hivyo. Inawezekana wakawapo wengine lakini mpaka dakika hii nawajua hawa hapa.
  1. Adui yako wa kwanza na anayeweza kukuondoa madarakani muda wowote akitaka ni huyu unayemdhania kuwa Swahiba wako, Bwana "RA". Ushahidi wote wa kimazingira unaonesha ukweli usiopingika kwamba huyu jamaa amekusaidia kufika katika kiti hicho kwa kutumia fedha zake (japo alizipora serikalini kupitia KAGODA nk.). Kama rohoni unalikubaliana na hilo ujue wazi kwamba mkono wake umefanikiwa kuzifikia zilizokuwa zinalipwa kwa Dowans na kwa kutumia hizo (akitaka) unaondoka mara moja. Kwani, unaweza hata kusukiwa mbinu ukafukuzwa na vikao vya chama chako kwa kushindwa kuongoza ama kutekeleza Ilani ya chama. Naamini tupo pamoja hata kama utakataa hadharani. Maana wewe na weye kwa kukataa tu unaongoza. Hey...! kweli...., huyu jamaa ndiye mmiliki halisi wa DOWANS japokuwa umiliki wake umefunikwa na idea ya "Powers of Attorney" maana kuna siku ulisema humjui. Uwezo wa huyu jamaa unaweza kuwanyima Ubunge baadhi wa wabunge wa chama chenu na hata watu maarufu na wenye nguvu kupoteza Uspika kwa njia ya "Gender balance issues" pale anapoamua. Sikufichi, mwogope huyu jamaa kama moto wa Jehanam. Kwa nguvu mliyomuuzia (na wewe unaijua) anaweza kufanya lolote. Kama huamini; itisha tume huru ichunguze wizi uliofanyika EPA, Richmond na ushahidi utumike kumbana RA mahakamani halafu uanze kuhesabu sekunde utakazokaa madarakani. Zikifika 60 nakula sumu. Mkuu, huyu jamaa anaweza hata kukulazimisha ujiuzulu mwenyewe na ukalitangazia taifa unajiuzulu kwa sababu za kiafya. Najua utabisha lakini roho inakusuta kwa kuwa unajua ukweli wa ninachokisema.
  2. Adui yako wa pili ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Unajua kwa nini? Mfano, matamshi ya Hosea kwa Afisa wa Ubalozi wa Marekani (miaka hiyo na baadaye kufichuliwa na wikileaks) yanatuonyesha kwamba hata hawa waliokuzunguka kwa karibu hawakubaliani na unavyoiendesha (au niseme RA anavyoiendesha) nchi hii lakini, hawana mahala pa kuzungumzia yanayowakera. Hawa ni hatari kwa kuwa kuna siku utataka kuzuia maandamano ya wanachi wanaoendelea kuchoshwa na utawala mbovu, kwa kutumia mabavu ya dola na watakugeuka (baada ya damu kidogo tu ya wananchi kupotea) kama kwa wenzetu waarabu. Kwa kauli nasema hawa wakiamua utaondoka maana hata nguvu hawatumii. Wao ni kuuchuna tu wenye machungu yao waandamane.
  3. Wanafiki ndani ya Chama chako kama alivyo Katibu wenu mkuu, huyo jamaa kutoka mkoa wa wanaume hapo ofisini kwako, na wengine wengi wenye tabia ya kuropoka ropoka (hata pale mnapokuwa hamjawasiliana) kuhusiana na jambo husika. Unakumbuka kauli yako kuhusu uchungu wa kuilipa DOWANS? (Najua haikutoka rohoni lakini...ndo ulivyosema) Katibu Mkuu alishaibuka na vitisho "Anayepinga anaweza kukihama chama maana tayari uamuzi umeshapitishwa kuwalipa nk..nk..." What do you expect from such guys". Wanawakera sana watu walio na mwanga juu ya upuuzi mnaoufanya huko madarakani na hii inachochea chuki kuliko mikutano na maandamano ya Chadema. I tell you, viongozi wengi wa Afrika ama ni waporaji au wametumwa kuwezesha matajiri waporaji, lakini wanafanya mambo hayo pasipo kuwashtua waliolala na wakishtuka hawawajibu kwa jeuri kama mnazotumia nyie. Mara "kelele za mpangaji...." Hivi unajua mtu mwenye kuelewa ulivyohandle maswala kama EPA, Richmond nk anavyojisikia uchungu mnapotoa majibu ya ki-mipasho penye malalamiko ya msingi? Yaani inawezekana mtu akatamani kufanya makosa yote ya Sehemu ya pili, Sura ya Saba ya Kanuni ya Adhabu. Unajua kwa nini? Mnajua wazi wenye makosa ni nyinyi halafu mnataka kutumia kutojua kwa wafuasi wenu masikini kumdharau mtu anayejaribu kusema ukweli. Tabia hii na hasa watu wanaokusaidia kuzifanya vinaweza kuvuruga nchi kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa sana kwa nchi na watu wake. Kama ni mapinduzi dhidi ya ungozi wako yanaweza kutoka hapa. Jamani mnakera! Raisi anasamehe suspect halafu anapohojiwa anajibu mipasho!
  4. Adui mwingine umeanza kumpandikiza wewe ukishiriana na Katibu mkuu wa chama chako. Mnasema nchi imeanza kuingia ktk udini baada ya kuona siasa zenu zilizokosa mwelekeo zinaanza kukosolewa zaidi. Kilichokupunguzia kura si udini! (na hata busara yako inakwambia ni kweli). Watu wameanza kushtukia promises za uongo ndani ya smiles zenu. Wameanza kuelewa ni jinsi gani watu ambao wao wanawashabikia wanaitafuna nchi kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu. They are not always ignorant, you know? Udini mnaodai umeanza kujitokeza, upo katika kutafuta mchawi wa failures zenu. Mimi na wewe tunajua wazi watanzania wenye uelewa wa chini na wa wastani hupendelea kuona mtu wa imani yao anashika madaraka kwa kuwa wanaona fahari hata pasipo kujua anawaletea nini. Wanaojua ndo utakuta wanamponda kiongozi mbovu pasipo kujali dini yake. Sasa unaposema udini umeanza unajua watu wa aina hiyo wanadhania nini? Wanadhani unapingwa na wafuasi wa dini nyingine kwa kuwa wewe ni dini tofauti (wakati wewe binafsi unajua wazi si kweli) na hatimaye wanaanza kuchukiana hata kwa kubishana tu. Waliosema wewe ni chaguo la Mungu mwaka 2005 walikuwa dini yako pekee? Tena wengi hawakuwa dini yako. Kwa nini wamebadilika basi? Umewaangusha na matarajio yao. JK! bado hatujawa na udini huo mnaodai unaanza kujitokeza isipokuwa kushindwa kwenu ndo kumewafanya mseme hivyo ili kuondoa kudharaulika kwa failures zenu.
  5. Kitakachokupindua ni tabia ya kutosema kweli kama... "Siwajui Richmond, Dowans, Kagoda wala sijawasamehe kwa wizi wao......" Hii ni hatari kwa kuwa mambo yanapofunuliwa na wanaojua inawakera wananchi wanaojua na baadaye wanaweza kuyafikisha kwa wasiojua vizuri and you know their reactions.
Ushauri wangu: Kama huwezi kufanya lolote kuisaidia nchi yako kupambana na matatizo ya msingi labda kweli angalia uwezekano wa kumrejeshea aliyekupa mamlaka achague mtu mwingine. Au yeye mwenyewe RA aongoze nchi tuone uwezo wake. Pengine atapunguza tamaa. Unajua hadi najikuta sijui nikuombe vipi ili uwe man enough to clear your own mess.

Hivi tukiacha politics, hapa tulipofikia, unaweza kuwakaripia watendaji wowote wanaokula rushwa na kutumia vibaya madaraka na mali ya umma kama hao wanaojilipa mabilioni kama lunch allowance katika maofisi yenu, wakakusikia?. Unaweza kusimama mbele ya wanaohitimu uafisa mathalani jeshi la polisi na kuwaambia rushwa ni mbaya? Unaweza kumwonya mtumishi wa Halmashauri anayelipa miradi hewa kwa fedha za walala hoi kuacha tabia hiyo vinginevyo umfukuze kazi?

Kama inafikia kipindi nafsi inakusuta hata unakosa ujasiri wa kuwaonya waliopo chini ya himaya hako ujue ndo chanzo cha kila tatizo ndani ya utawala wako. Watu mtapuuza hili lakini amini usiamini nchi maskini haiwezi kuendelea kama kiongozi wa nchi atakuwa hawezi kukaripia maovu hata kama ni kwa unafiki uliofichika na kuwafanya watu kuhofia adhabu. TAFAKARI!
 
..Ni maneno mazito. Tatizo jingine pia ni KUTOSIKIA...kwa hiyo yataishia yanapoishia mengine yote.
 
..Ni maneno mazito. Tatizo jingine pia ni KUTOSIKIA...kwa hiyo yataishia yanapoishia mengine yote.

KAPUNI...ila kuna siku atasikilizishwa.Kuwa na hofu ni dalili tosha kuwa kwa mbali ameanza kusikia mitetemo.Yuko ktk stage ya self denial,soon he will wake up.Laiti kungekuwa na political counselling kama ilivyo ushauri nasaha!
 
..Ni maneno mazito. Tatizo jingine pia ni KUTOSIKIA...kwa hiyo yataishia yanapoishia mengine yote.

Hilo kweli ndio tatizo kubwa la wanasiasa wetu...kutosikia... Lkaini mimi ninadhani ni kiburi...Inakuwaje mtu kama Rostam sasa kwa muda wa miaka kadhaa amekuwa news na hakuna uamuzi wowote aidha wake binafsi au chama kumjiuzulu?

Anglia kama yule mama waziri wa Ufaransa kajiuzulu tu kwa vile alikuwa na ukaribu na rais wa zamani wa Tunisia...hii ina maana kama mwanasiasa unasemwa kila kukicha kwenye media unajiuzulu ili usiharibie serikali au chama chako.

Lakini Bongo hio hakuna, Hapa juzi juzi waziri wa ulinzi Guttenberg amejiuzulu kwa kujipa title ya DR wakati tunao kina Lukuvi wamo tu serikalini na wametoa ile DR...je wanasiasa wetu ni nini kiburi au hawsikii?
 
Mie sijaelewa hivi hio kagoda ni ya rostam au manji? Maana kuna toleo moja la mwanahalis lilimtoa manji kama mmiliki
 
JK alipoambiwa kuwa yeye ni chaguo la Mungu hakudai kwamba kauli hiyo ni ya udini! Kuona kura zimepungua kwa 20% ndio anadai eti kuna udini ili ku-justify kushindwa kwake kwa kiasi hicho!
 
Nguzo,
Kagoda ni ya Rostum. Lakini alikuwa amemwomba Manji awe "fall guy" ikiwa mambo yatazidi kuwa mabaya.
 
politicianz ni vibuli!wamesahau ni nan alowpaeleka hapo

politicians wa CCM wako sahihi na wanacho kifanya (kuwasahau wanachi), kwani wanatumia pesa nyingi sana kupata ushindi, hii inafanya waamini ni pesa zao na wala sio wananchi wanao wapa kura....mkikataa pesa zao na makawapa kura..LABDA wanaweza wakaanza kufikiria tofauti
 
CCM haiwezi kujisafisha hata kidogo! wengi wa wanachama si wasafi..kuna mkubwa mooja serikalini alimshauri HOSEA namna ya kumaliza ufisadi serikalini lakini mpaka leo hakuna kilicho fanyika....
 
This might sound stupid, but I say lets flood Ikulu's mailbox! Starting with this one here, we print it, go to the nearest post office and address it to:

Dr Joker Kikwete,
President's Office,
Magogoni Road,
P.O. Box 9120,
Dar es Salaam.
 
shikamoo mkuu! (sijui hata kama una kawaida ya kusoma jf au la! Naomba walau tiss wakufikishie ujumbe wangu) maana inadaiwa jf ni ya chadema lakini na sie tunaitumia.

Nimesikitika sana kutokana na ulivyoupokea mwito wa chadema kukutaka utoe tamko kuhusu malipo ya dowans ama u-face nguvu ya umma.

Yaani na nguvu zote zinazokuzunguka bado unahofia uwezekano ("wa kufikirika") wa kukuondoa madarakani mzee? Tena jambo la kusikitisha unadhani uchochezi wa cdm utapata nguvu ya kuleta machafuko hapa nchini kiasi cha kuing'oa serikali yako halali (inayoongozwa kwa remote na ra) madarakani? Pole sana kwa mshtuko kama ulipata kweli. Naomba kupitia fursa hii nikupe dodoso kidogo.


Chadema kama chama (pamoja na kuwasingizia udini) hawana jeuri ya kukutisha wala kukuondoa madarakani. Kwa uchambuzi makini, kama rafiki zangu wakusanya habari muhimu za taifa watafanya kazi yao kwa makini watagundua kwamba maadui wakubwa na wanaotishia madaraka yako ni hawa wafuatao na sababu za wao kufanya hivyo. Inawezekana wakawapo wengine lakini mpaka dakika hii nawajua hawa hapa.
  1. adui yako wa kwanza na anayeweza kukuondoa madarakani muda wowote akitaka ni huyu unayemdhania kuwa swahiba wako, bwana "ra". Ushahidi wote wa kimazingira unaonesha ukweli usiopingika kwamba huyu jamaa amekusaidia kufika katika kiti hicho kwa kutumia fedha zake (japo alizipora serikalini kupitia kagoda nk.). Kama rohoni unalikubaliana na hilo ujue wazi kwamba mkono wake umefanikiwa kuzifikia zilizokuwa zinalipwa kwa dowans na kwa kutumia hizo (akitaka) unaondoka mara moja. Kwani, unaweza hata kusukiwa mbinu ukafukuzwa na vikao vya chama chako kwa kushindwa kuongoza ama kutekeleza ilani ya chama. Naamini tupo pamoja hata kama utakataa hadharani. Maana wewe na weye kwa kukataa tu unaongoza. Hey...! Kweli...., huyu jamaa ndiye mmiliki halisi wa dowans japokuwa umiliki wake umefunikwa na idea ya "powers of attorney" maana kuna siku ulisema humjui. Uwezo wa huyu jamaa unaweza kuwanyima ubunge baadhi wa wabunge wa chama chenu na hata watu maarufu na wenye nguvu kupoteza uspika kwa njia ya "gender balance issues" pale anapoamua. Sikufichi, mwogope huyu jamaa kama moto wa jehanam. Kwa nguvu mliyomuuzia (na wewe unaijua) anaweza kufanya lolote. Kama huamini; itisha tume huru ichunguze wizi uliofanyika epa, richmond na ushahidi utumike kumbana ra mahakamani halafu uanze kuhesabu sekunde utakazokaa madarakani. Zikifika 60 nakula sumu. Mkuu, huyu jamaa anaweza hata kukulazimisha ujiuzulu mwenyewe na ukalitangazia taifa unajiuzulu kwa sababu za kiafya. Najua utabisha lakini roho inakusuta kwa kuwa unajua ukweli wa ninachokisema.
  2. adui yako wa pili ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Unajua kwa nini? Mfano, matamshi ya hosea kwa afisa wa ubalozi wa marekani (miaka hiyo na baadaye kufichuliwa na wikileaks) yanatuonyesha kwamba hata hawa waliokuzunguka kwa karibu hawakubaliani na unavyoiendesha (au niseme ra anavyoiendesha) nchi hii lakini, hawana mahala pa kuzungumzia yanayowakera. Hawa ni hatari kwa kuwa kuna siku utataka kuzuia maandamano ya wanachi wanaoendelea kuchoshwa na utawala mbovu, kwa kutumia mabavu ya dola na watakugeuka (baada ya damu kidogo tu ya wananchi kupotea) kama kwa wenzetu waarabu. Kwa kauli nasema hawa wakiamua utaondoka maana hata nguvu hawatumii. Wao ni kuuchuna tu wenye machungu yao waandamane.
  3. wanafiki ndani ya chama chako kama alivyo katibu wenu mkuu, huyo jamaa kutoka mkoa wa wanaume hapo ofisini kwako, na wengine wengi wenye tabia ya kuropoka ropoka (hata pale mnapokuwa hamjawasiliana) kuhusiana na jambo husika. Unakumbuka kauli yako kuhusu uchungu wa kuilipa dowans? (najua haikutoka rohoni lakini...ndo ulivyosema) katibu mkuu alishaibuka na vitisho "anayepinga anaweza kukihama chama maana tayari uamuzi umeshapitishwa kuwalipa nk..nk..." what do you expect from such guys". Wanawakera sana watu walio na mwanga juu ya upuuzi mnaoufanya huko madarakani na hii inachochea chuki kuliko mikutano na maandamano ya chadema. I tell you, viongozi wengi wa afrika ama ni waporaji au wametumwa kuwezesha matajiri waporaji, lakini wanafanya mambo hayo pasipo kuwashtua waliolala na wakishtuka hawawajibu kwa jeuri kama mnazotumia nyie. Mara "kelele za mpangaji...." hivi unajua mtu mwenye kuelewa ulivyohandle maswala kama epa, richmond nk anavyojisikia uchungu mnapotoa majibu ya ki-mipasho penye malalamiko ya msingi? Yaani inawezekana mtu akatamani kufanya makosa yote ya sehemu ya pili, sura ya saba ya kanuni ya adhabu. Unajua kwa nini? Mnajua wazi wenye makosa ni nyinyi halafu mnataka kutumia kutojua kwa wafuasi wenu masikini kumdharau mtu anayejaribu kusema ukweli. Tabia hii na hasa watu wanaokusaidia kuzifanya vinaweza kuvuruga nchi kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa sana kwa nchi na watu wake. Kama ni mapinduzi dhidi ya ungozi wako yanaweza kutoka hapa. Jamani mnakera! Raisi anasamehe suspect halafu anapohojiwa anajibu mipasho!
  4. adui mwingine umeanza kumpandikiza wewe ukishiriana na katibu mkuu wa chama chako. Mnasema nchi imeanza kuingia ktk udini baada ya kuona siasa zenu zilizokosa mwelekeo zinaanza kukosolewa zaidi. kilichokupunguzia kura si udini! (na hata busara yako inakwambia ni kweli). Watu wameanza kushtukia promises za uongo ndani ya smiles zenu. Wameanza kuelewa ni jinsi gani watu ambao wao wanawashabikia wanaitafuna nchi kwa maslahi ya kikundi kidogo cha watu. They are not always ignorant, you know? Udini mnaodai umeanza kujitokeza, upo katika kutafuta mchawi wa failures zenu. Mimi na wewe tunajua wazi watanzania wenye uelewa wa chini na wa wastani hupendelea kuona mtu wa imani yao anashika madaraka kwa kuwa wanaona fahari hata pasipo kujua anawaletea nini. Wanaojua ndo utakuta wanamponda kiongozi mbovu pasipo kujali dini yake. Sasa unaposema udini umeanza unajua watu wa aina hiyo wanadhania nini? Wanadhani unapingwa na wafuasi wa dini nyingine kwa kuwa wewe ni dini tofauti (wakati wewe binafsi unajua wazi si kweli) na hatimaye wanaanza kuchukiana hata kwa kubishana tu. Waliosema wewe ni chaguo la mungu mwaka 2005 walikuwa dini yako pekee? Tena wengi hawakuwa dini yako. Kwa nini wamebadilika basi? Umewaangusha na matarajio yao. Jk! Bado hatujawa na udini huo mnaodai unaanza kujitokeza isipokuwa kushindwa kwenu ndo kumewafanya mseme hivyo ili kuondoa kudharaulika kwa failures zenu.
  5. kitakachokupindua ni tabia ya kutosema kweli kama... "siwajui richmond, dowans, kagoda wala sijawasamehe kwa wizi wao......" hii ni hatari kwa kuwa mambo yanapofunuliwa na wanaojua inawakera wananchi wanaojua na baadaye wanaweza kuyafikisha kwa wasiojua vizuri and you know their reactions.
ushauri wangu: kama huwezi kufanya lolote kuisaidia nchi yako kupambana na matatizo ya msingi labda kweli angalia uwezekano wa kumrejeshea aliyekupa mamlaka achague mtu mwingine. Au yeye mwenyewe ra aongoze nchi tuone uwezo wake. Pengine atapunguza tamaa. Unajua hadi najikuta sijui nikuombe vipi ili uwe man enough to clear your own mess.

Hivi tukiacha politics, hapa tulipofikia, unaweza kuwakaripia watendaji wowote wanaokula rushwa na kutumia vibaya madaraka na mali ya umma kama hao wanaojilipa mabilioni kama lunch allowance katika maofisi yenu, wakakusikia?. Unaweza kusimama mbele ya wanaohitimu uafisa mathalani jeshi la polisi na kuwaambia rushwa ni mbaya? Unaweza kumwonya mtumishi wa halmashauri anayelipa miradi hewa kwa fedha za walala hoi kuacha tabia hiyo vinginevyo umfukuze kazi?

Kama inafikia kipindi nafsi inakusuta hata unakosa ujasiri wa kuwaonya waliopo chini ya himaya hako ujue ndo chanzo cha kila tatizo ndani ya utawala wako. Watu mtapuuza hili lakini amini usiamini nchi maskini haiwezi kuendelea kama kiongozi wa nchi atakuwa hawezi kukaripia maovu hata kama ni kwa unafiki uliofichika na kuwafanya watu kuhofia adhabu. tafakari!

umegonga panapotakiwa mkuu..mkwere balaa jaman...superb president ironically.
 
Ukiona ajakujibu nitakupatia email address ya Salva Roymamu atamfikishia jamaa kwani hata email ya ikulu hakuna wanatumia zao binafsi
 
Nasikitika saana kwa nchi zetu hizi watu wenyemawazo mazuri kama wewe hawasikilizwi na hufa na mawazo yao mazuri, very sorry sir hatuna mda wakusikiliza mawazo yako cc ndo mataahila wenyewe tumepewa rungu tunalitumia, sanasana unataka tukuue! BCS UMETOA KAULI ZA UCHOCHEZI!
 
Umegusa panapotakiwa. Mawazo yangu ni je hii itawafikia vipi waTZ ambao sio member wa JF, habari hii inagusa inapaswa kufikiwa na watu ili waelimike.
 
Back
Top Bottom