Phillemon Mikael,
serikali lazima ilaumiwe maana walijuwa hili ...walipewa plan na tanesco tangu 2006...leo wanataka kumlaumu idrissa ....sio fair.maneno mengi tu bila utekelezaji ...
Mkuu wangu hapa bado kabisa sintakubaliana na wewe kwa sababu tunazungumzia strategy ya shrot term kutokana na dharura iliyosababisha mitambo hii ya Dowans kuwepo nchini..
Swala la Umeme Tanzania ni sugu, ni donda ndugu lisilopona toka mwalimu alipoondoka, ndonda ambalo kwa wale wanaosifia uongozi wa Mwinyi na Mkapa wapate kufahamu kwamba haya ni matatizo yanayotokana na vyanzo vya umeme..
Kumbuka Kikwete anaingia madarakani mwaka 2006 tayari umeme wa mgao upo katikati, Mkapa kaondoka bila suluhisho, mji mzima ulikuwa unanuka deisel na kelele za generator..biashara kubwa mjini ni generator na mashine za kuvuta maji visimani..I mean, mji mkuu wa Tanzania!..
Hivyo maamuzi yaliyopitiwa 2006 ni pamoja na umeme wa dharura (short term) ambao serikali ya Kikwete ulipitisha na kuwapa Tanesco go ahead..Hili ndilo tatizo linalotuweka hapa haya maswala ya long term tuliyakuta, yapo na yataendelea hadi kesho akija kiongozi mwingine..
Tatizo ni hawa Tanesco kwanza kuingiza mashirika kama Richmond, pili kukubali upokezananji wa Richmond na Dowans wakati mashirika yote haya mawili ni FEKI..
Sasa nachotaka mimi kuelimishwa ni kitu kidogo sana.. Ikiwa hawa tanesco walipopewa mamlaka na fedha za kutuondolea matatizo ya dharura wameshindwa kuchukua hatua bora na zenye kuponya tatizo dogo Ijewe leo mnataka sisi wananchi tuamini kwamba mapendekezo yao leo hii yana nia nzuri kwetu?..
Ebu fikiria walipopewa fedha za kwanza wamezitumia kuwapa tender mashirika manne tofauti wakati iliwezekana kabisa shirika moja lichukue tender yote tena iwe mali ya Tanesco na tukapata umeme wa Uhakika (Watsila)..lakini wapo wakachukua ku lease umeme toka mashirika ambayo hayajawahi kuvua umeme maishani!..Kwa nini waliwapa Richmond shirika feki na baadaye hata kukubali mabadilishano ya Mkataba kati ya Richmond na Dowans ambayo bado pia ni shirika FEKI!..
Leo unataka mimi niamini kwamba mitambo ya Dowans tunaihitaji kiasi hicho wakati kila kitu nyuma yake kilikuwa kubambikwa!..Yes tunahitaji hizo 100MW lakini matatizo ya mwaka 2006 hayakumalizwa na dowans.. kuna mashirika mengine manne ambayo yanatoa 2/3 ya umeme ulioongezwa wakati ule..kwa hiyo msitake kutumia mwaka 2006 kama sababu wakati Dowans hawana uhusiano na mitambo ya Watsila na Aggriko..Shida zetu zipo palepale wawepo dowans ama hawapo na kwa vile sasa hivi hatuna tatizo la mvua hivyo tuna muda kiasi wa kuagizi hiyo mitambo mipya na kuifunga..wananchi wataelewa pindi kinachofanyika hapa ni dhidi ya Mafisadi!
Hayo maswala ya Paris na Dowans tutafikishana mbali kwa sababu ndipo sisi Watanzania tutapata kumfahamu nani mmliki wa shirika hilo...
Paris twende tunataka kujua undani wa shirika hili na nani aliyekubali mabadilishano kati yao na Richmond!..kwanza hawana Ofisi wala Address itakuwa starehe kubwa kusikiliza kesi hiyo!..Yaani duh naisubiri kwa hamu, mimi naomba kazi ya ofisi ya mwanasheria mkuu kuhusiana na hawa jamaa.. Wataniroga sanaaaa!!