Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,103
- 136,763
Dowans wanauwezo wa kuzalisha hiyo 100MW kwa namna gani?
Mwanakijiji, kwenye hili swala la Dowans, Mkuu hueleweki.
Mwanzoni ulisema tuwaachie huru wa kina Gire na nunue mitambo, na kwamba Rostam ameshatushinda and what not.
Baadae ukamtetea Zitto, japo ukasema hukubaliani na mahitimisho yake.
Ulipoulizwa mahitimisho yako wewe ni yapi ukasema tukasome Cheche.
Kwenye Cheche kuna mahitimisho ya Jessica Fundi na Fred Katunzi.
Sasa basi, kwa sababu kwenye hili swala wewe kama Mwanakijiji unaogopa kuchukua msimamo mimi nadhani sio busara kujadili kitu na ghosti Jessica na ghosti Fredi!
Ni za kuwatetea wananchi. ... yaani mnataka niamini kwamba Watanzania hawawezi kumwamini mtu, na kutofautiana mtazamo katika jambo fulani ndo unakuwa uadui au? Binafsi ninampongeza sana Mhe.Zito kwa kuonyesha mtazamo/msimamo wake wazi. Hawa ndiyo viongozi tunaowahitaji. Tatizo la Watanzania ni 'opportunism' yaani msimamo wa mtu unaangalia upepo, huu ni udhaifu mbaya sana. Ninapata shida juu ya uwezo wetu wa kujua na kuchambua mambo. Lazima tujue kuwa kila mtu anaakili yake na hatuwezi kuwa na mawazo mamoja.

Bado sijaelewa unamaanisha nini?
Kutofautiana kupo!! Ila hili Mh Zitto alichemka vibaya sana..
Zitto kachemsha atafute inabidi namna ya kurudisha reputation nzuri aliyokuwa nayo miongoni mwa Watanzania walio wengi. Siku zote Zitto alikuwa anasimama upande mmoja na wananchi katika ya vita dhidi ya mafisadi, kwenye hili la kushawishi serikali inunue mitambo chakavu ya Dowans alikuwa upande mmoja na mafisadi.
inayetofautiana na wewe au wengi anakuwa amekosea... hiyo ndiyo shida yetu. tunatakiwa kuwapa watu nafasi ya kuonyesha wanachokiwaza au kukiamini sasa sisi tunataka wawe 'opportunists'
Ni za kuwatetea wananchi. ... yaani mnataka niamini kwamba Watanzania hawawezi kumwamini mtu, na kutofautiana mtazamo katika jambo fulani ndo unakuwa uadui au? Binafsi ninampongeza sana Mhe.Zito kwa kuonyesha mtazamo/msimamo wake wazi. Hawa ndiyo viongozi tunaowahitaji. Tatizo la Watanzania ni 'opportunism' yaani msimamo wa mtu unaangalia upepo, huu ni udhaifu mbaya sana. Ninapata shida juu ya uwezo wetu wa kujua na kuchambua mambo. Lazima tujue kuwa kila mtu anaakili yake na hatuwezi kuwa na mawazo mamoja.
Sikonge, hueleweki. Kwanza, fahamu kwamba Nyambala kasema tununue vimitambo vya 1.6MW, wewe unasema tununue mitambo ya 20-50MW. Kwa hiyo hata wewe unacho ki advocate hakiendani na alichosema Nyambala. Kwa kweli umeunga tela pointi kichwa kichwa wakati na wewe mwenyewe huonekani kui support. Pili, kuhusu faida na hasara za mitambao mikubwa na midogo, mimi sikusema ubaya na uzuri wake, ile nimesema Nyambala katoa mfano irrelevant, misrepresented, wa vi generator vya 1.6MW akasema vinafanana na nguvu ya Dowans. Si kweli!
Lakini tukiachana na mifano misreprented wa vijimitambo vya Nyambala, hata wewe umejichanganya. Umesema kuna faida ya kununua vijimitambo vidogo kama vya power plant ya Nyambala, halafu hapo hapo unasema utatoa 300MW na ni poa: "...Hii inafaida kubwa kuwa ukiharibika moja ya mtambo mdogo nchini, nchi haiteteleki. Ila sasa mkiwa na mtambo kama huu wanasema ujengwe Rufiji, na unaanza kutoa 300MW, loo ni poa ..." Una maana gani hapo, vimitambo hivi vitatoa 300MW? Hueleweki.
inayetofautiana na wewe au wengi anakuwa amekosea... hiyo ndiyo shida yetu. tunatakiwa kuwapa watu nafasi ya kuonyesha wanachokiwaza au kukiamini sasa sisi tunataka wawe 'opportunists'
mkuu umesikia mahojiano waliofanya Zitto na Mwakyembe na ITV? Mwakyembe kasema live msimamo wa Zitto si wa kamati yake.....ni wake binafsi na anamshangaa kama ndio Zitto anaemfahamu.....Zitto hakubisha....Zittto hajaonyesha msimamo wowote, na wala hajafanya jitihada zozote. Kinachofanyika sasa ni kuamua kutumia opportunity hii kuongea about Zitto. Kilichozungumzwa na kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma ni msimamo wa kamati nzima na si msimamo wa Zitto kama Zitto. Hapa JF alisema wakati muafaka ukifika atatoa views zake kama Zitto. HIvyo kama mnahitaji kujua views zake juu ya hili inabidi mjiunge nami katika kuwa na subira.
Zittto hajaonyesha msimamo wowote, na wala hajafanya jitihada zozote. Kinachofanyika sasa ni kuamua kutumia opportunity hii kuongea about Zitto. Kilichozungumzwa na kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma ni msimamo wa kamati nzima na si msimamo wa Zitto kama Zitto. Hapa JF alisema wakati muafaka ukifika atatoa views zake kama Zitto. HIvyo kama mnahitaji kujua views zake juu ya hili inabidi mjiunge nami katika kuwa na subira.
"Wale ambao zamu yao ya kula hii nchi....imepita"-Dr Mwakyembe...
Dr Mwakyembe-"nusu anayotamka Zitto sio maamuzi ya kamati yake......."
Kwanza msikieni Dr Slaa......Dr Slaa na mpito wa Dowans
Kisha wasikie Zitto na Dr Mwakyembe link below
Dowans na malumbano ya kamati za bunge
Credit:kennedyblog
Msikieni tena mbunge kijana alivyobwabwaja......msikilize kwa umakini Dr Mwakyembe.....
........... Ubaya wa Dowans ni legacy ya ufisadi wa Richmond na kanuni zinazokataza kununua vifaa chakavu.............