Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,095
- 43,307
Unaamini based on what?
Keshasema huyo Mkuu wa TANESCO kwamba umeme ukikatika asilaumiwe (according to what I am reading in here) kwa hiyo ina maana anaashiria yupo to stay.
Wewe unaamini ata quit within hours based on what?
Kwanza, unaonyesha jinsi gani ulivyo slow, Id ni mkurugenzi wa TANESCO na Bill ni waziri wa Nishati na madini. Wana mandate ya kulizungumzia hilo unalotaka nilizungumzie. Kwa vile wewe ni kuwadi wao uliyesema wanunue mitambo ya Dowans eti April kutakuwa na shida ya umeme, hutaki niwaulize maelezo kama wanayo au nini kingine kikuhangaishacho?
Pili acha uzushi, wapi nimesema wengine hawatakiwi kulizungumzia! Hii tabia yako ya uzushi na uchinganishi lini utaiacha?
Any way, naona umechukua kijiti kwenye tabia ya mwa fulani - arboreal in nature. Keep the spirit up.
I want to state here in explicit terms that, I, Kabwe Zuberi Zitto (MP), Chairman Public Investments Committee of Parliament of Tanzania, stand with TANESCO on their desire to acquire gas fired turbines to improve electricity generation to the country. I stand firm to my decision and ready to be held accountable to that. I do this in good faith. I am genuine and honest. People can say all what they want to say, so long as this decision is mine based on the information i have, technical information. So long as i reached to this decision without any influence whatsover, i stand by it.
Nimetukanwa sana humu. Nimesimangwa sana humu na kuzushiwa kila aina ya tuhuma. Ninajijua kuwa sina bei. Siwezi kununuliwa na yeyote. Ninajijua na nimekuzwa kusimamia yale ninayoamini hata nikibaki peke yangu. Siyumbi. Siyumbishwi. Niliokuwa nao Chuo Kikuu wanajua nilivyo.
Nimefuatilia sana mjadala huu na kuona umejaa hisia kali sana. Ninajua ni hisia za watu wanaopenda nchi yao. Ninajua ni hisia za kizalendo. Sina mashaka na hili hata kidogo. Hata hivyo uongozi hauendeshwi kwa hisia tu. Uongozi wa nchi ni zaidi ya hisia na maneno matupu (hot air).
Nimesema hapo awali kuwa kwa kuwa Watanzania wamezoea kuwa na viongozi wala rushwa na waongo, itawachukua muda kukubali viongozi honest. Hata hivyo, muda huo utafika tu.
Hata hivyo, ni vema sana tujifunze kuheshimu maamuzi ya watu wengine. Kwamba leo mtu akiamua usivyotaka kanunuliwa? Je hayo maamuzi mengine hayawezi pia ya kununuliwa? Hapana, nadhani pale ambapo mwingine ana maamuzi tofauti ni vema kuheshimu maamuzi hayo bila kumwita kila aina ya majina mabaya.
Mimi binafsi, ninaamini kabisa kuwa hoja za TANESCO kuhusiana na suala la equipments hizi ni hoja zenye mshiko. Hoja za Kamati ya Nishati na Madini ni hisia za kisiasa.
Sio kweli kuwa TANESCO hawakuja katika kamati na alternatives. Walikuja na alternatives kadhaa na zote tulizijadili.
- Walieleza kushindwa kwa Kiwira kuzalisha 50MW mwezi huu na pia 150MW mwezi wa Septemba.
- Walieleza mradi wa Kinyerezi wa 240MW kushindwa kuanza kupitia PPP kufuatia wawekezaji kukosekana
- Walieleza mradi wa umeme wa upepo Singida kukwama
- Walieleza kuhusu mradi wa 300MW wa Mtwara.
Katika hili mnawalaumu TANESCO bure tu. walitoa altrnative ya Dowans. walisema mbadala ni kununua mtambo mpya lakini walitahadharisha muda kwani mitambo mipya haipo tayari imetengenezwa na kuwekwa katika show room. Huwa inakuwa ordered kwa mtengenezaji na kuundiwa, kisha kufungwa na baadae kuwa commissioned ndio uanze kazi.
Mwanakijiji alizungumzia umeme wa Zambia. Tunanunua umeme wa Zambia na ndio unatumika Sumbawanga. Umeme huu ni mdogo sana na ubora wake pia ni mdogo. Kimsingi nchi zote za SADC zina tatizo kubwa sana la Umeme isipokuwa (potentialities) Msumbiji, Tanzania na Congo DR.
Mwanakijiji alizungumzia Stigler's gorge. Huu ni mkakati wa muda mrefu. It takes time kujenga hydro plant. Kule Kigoma wanajenga Malagarasi mini hydro, itachukua miaka 2 (8MW).
Ni rahisi sana kuzungumza masuala haya lakini realities are different. Ninashauri baada ya mjadala huu wa TANESCO na DOWANS kuwa umekwisha (TANESCO wameumaliza) tuanze mjadala sober kuhusu 'energy sector' in Tanzania. Tuwe proactive na sio reactioneries.
Power masterplan ipo. Haitekelezeki. Energy policy ipo. Tujadiliane baada ya kadhia hii ili tuone nchi yetu iendaje katika sekta ya Nishati.- 2
based on gut feeling
thanks mkuu;
idris ana matatizo yake lakini sometimes ana maamuzi ya kiume... Kama hili la u-turn ni kweli, basi ni dume haswaa (ps: Hapa simuhusishi chochote kuhusu epa/bot etc.]
alkaloids ni chungu sana lakini zina medicinal properties
Gut feeling feeling yako kwamba Mkurugenzi wa TANESCO atajiuzulu in a few hours iko founded on what facts? Kwamba, imeonekana ana makosa fulani hivyo hawezi kuvumilia skandali, au akisubiri sana atafukuzwa, au kushitakiwa, au nini hasa cha kumfanya ajiuzulu?
Au hii ni "gut feeling" umeotea tu kama wanaoangalia mbalamwezi wanatabiri mvua na future events?
ndiyo kama hiyo.. ndiyo maana ya imani...!
Aksante.
Nilidhani kuna la zaidi, some kind of an educated guess.
Ngeleja, Dr Rashidi you cannot fool us again
Reports emanating from State House yesterday said the president has not intervened in the Dowans gas turbine wrangle. In other words, the matter has not attracted State House.
Mr President, we ask you to intervene in the mess created between the ministry of energy and minerals and TANESCO to save the face of the TANESCO board. They have a strong headed chief executive and an unpredictable minister. They all deserve a sack for seeking to embarrass the government by saving faces of Richmond suspects.
Kwanini Mwakyembe ahusike na kutafuta mitambo mipya ya kuzalisha umeme na siyo Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Idrissa Rashid!? Kama kazi imemshinda basi ni bora aachie ngazi haraka sana.Hata kama kununua mtambo mpya kunahitaji miaka miwili, hili lilipaswa kufahamika na Wataalamu wa TANESCO akiwemo Mkurugenzi Idrisa Rashid na hivyo kuanza kulifanyia kazi mapema na siyo kusubiri miezi michache kabla ya nchi kuingia kizani ndiyo kutaka kuishinikiza nchi kununua mitambo michakavu iliyojaa ufisadi.
Jamani siku nzima inaisha, mbona Mh. Zitto leo kasusa kabisa kuendelea na huu mjadala baada ya idris kuhitimisha?? Mimi nilijua sasa ndio Mwenyekiti wa PAC atatuletea umakini wake kuepusha nchi kwenda gizani kama Dr. Idris alivyotishia baada ya plan ya Dowans kukwama, kumbe kelele zote zilikuwa sio za kusaidia nchi bali Dowans.
Ama kweli ishi uone.
Mh. Zitto I'm not attacking U personally, I'm just attacking Chairman wa PAC ambae alitaka kuteletea madhara makubwa na hasara wananchi wa Tanzania.
Mbona hapa kama una personal issue na Zitto? Ameshasema aliyosema mbona unamshupalia hivi? What gives?Jamani siku nzima inaisha, mbona Mh. Zitto leo kasusa kabisa kuendelea na huu mjadala baada ya idris kuhitimisha?? Mimi nilijua sasa ndio Mwenyekiti wa PAC atatuletea umakini wake kuepusha nchi kwenda gizani kama Dr. Idris alivyotishia baada ya plan ya Dowans kukwama, kumbe kelele zote zilikuwa sio za kusaidia nchi bali Dowans.
Ama kweli ishi uone.
Mh. Zitto I'm not attacking U personally, I'm just attacking Chairman wa PAC ambae alitaka kuteletea madhara makubwa na hasara wananchi wa Tanzania.
Dr. Idris hawezi kusema alichosema na akaendelea kuwa madarakani!!