Sasa hivi Zitto kazama kisiasa na kimaadili vile vile. Zitto hawezi kuandikwa vizuri kwenye RAI ya sasa na bado ukaamini kuwa ni Zitto yule yule. Hivi rai ilinunuliwa na nani vile? Sasa nilipoona tu positive news za Zitto ndani ya RAI nikajua kumekucha. Inawezekana CHADEMA bado wanaangalia upepo. Lakini naibu katibu mkuu wa CHADEMA akiandikwa vizuri kwenye RAI hatuhitaji kuuliza maswali mengi. RAI si Tanzania Daima na kwa siku za nyuma tulikuwa tukiona. Tusubiri kuona makala za Mbowe tena kwenye rai? Let's wait and see...... Pengine ni mawazo tu!
Mag3.
Tunashindwa kumuunga mkono Zitto si kwa sababu ya kufurahia kuanguka kwake. Ni kwa sababu ya logic rahisi. Zitto sasa hivi ana positive coverage RAI, unataka tuamini kuwa RAI iko balanced katika reporting yake? Imebadilika? May be.
Lakini logic rahisi ni hii. Zitto anaungana na TANESCO pamoja na Wizara ya madini na Nishati kuunga mkono ununuzi wa mitambo ya Dowans, na kwa maneno yake mwenyewe issue siyo tunanunua wapi. Issue ni kuwa tupate solution. Nakubaliana na huu msimamo ikiwa tungekuwa tunanunua bidhaa rahisi. Hiki tunachonunua ni MITAMBO!!! Reputation ya muuzaji kwenye bidhaa kama hizi ni muhimu kuliko kitu kingine chochote. Kununua mitambo ni kufungua mahusiano ya muda mrefu, kwani mitambo ina vitu vingi ambavyo hata ukimleta mtaalam gani hawezi kuona vyote na kujiridhisha kuwa kinachosemwa na muuzaji ni sahihi. Ndo maaana tunahitaji kujua reputation ya muuzaji, ili ikitokea tatizo huko mbeleni turudi kwake. Na kwa issue kama ya mitambo tatizo lazima litatokea dogo au kubwa!!!!
Sasa ikiwa unanunua kutoka kwa mtu ambaye humjui vizuri ni kama kununua CD kwa machinga barabarani. Unabeba ukifika nyumbani, ukiweka kwenye DVD player yako ile CD ikagoma basi unatulia na kujiridhisha kuwa "after all nimenunua shilling elfu tatu tu". Je unataka tufike hapo? Mitambo ile hatuinunui kwa elfu tatu wala milioni tatu.
Zitto anayajua yote hayo. Atueleze kwa nini sasa hivi yuko tayari kununua relationship (kununua mitambo ni kununua relationship) ya muda mrefu, bila kuwa na uhakika wa unayenunua hiyo relationship kutoka kwake? Au Zitto anajua zaidi kuhusu huyu Dowans ni nani na ana uhakika naye. Mbona hatuambii wengine wote ili tukaondoa wasiwasi???
Tunategemea consistency kutoka kwa mtu tunayeamini kuwa ni kiongozi mzuri. Tungetarajia kuwa Zitto, Kabla ya kutoa support yake angeuliza maswali ambayo wote tungeyaona na kujua. Viongozi wazuri hawako predictable, ila wako consistent. Kama ni republican atakuwa conservative always. Suala la kutokuwa predictable lisichanganywe na consistency. Nyerere was somehow not predictable, lakini he was consitent mpaka anakufa. Kwa suala kama hili wala usingejiuliza nyerere angekuwa upande gani!!!
Zitto????? Let's wait and see. Lakini so far utetezi alioutoa ni shameful. Ndo maana KGM and other well wishers wa Zitto wanakuwa concerned. What has gone wrong?
Ukweli tangu Dr. Idrisa aingie tanesco kunamabadiliko fulani mita za luku zimekuwa za kumwaga, kuunganishwa sasa ni chap chap, longolongo za wasoma mita hakuna tena. Hawa wanaonyonya mafuta ya transforma tumeshajiundia sungusungu wenyewe, mtaani kwetu tumeajiri korokoroni pamoja na kulinda mtaa wanalinda na transforma. Ila hili la kukiuka maamuzi ya bodi linataka kufanana na kesi ya liyumba vile! nadhani takukuru wanaliona hili, watamchukua maelezo sio muda mrefu.
Nadhani Dr. anatakiwa aajiri Strategic planning manager pia.
Ni kweli kuna a lot of well wishers katika mjadala huu lakini KGM na moelex23 sio miongini mwao. Wao kwao hii ni nafasi ya "kummaliza Zitto" wanasahau kuwa tofauti na vijiwe vingine Jamboforum kuna watu makini wasiokubali kubabaishwa na cheap spinning kama zao. Mchango kama wako ndio tunaweza kusema kuwa una nia njema na Zitto pamoja na Tanzania yetu kwa ujumla. Keep it up
omarilyas
Kubali au usikubali mitambo ya Dowans ikinunuliwa haitafanya kazi zaidi ya miaka mitatu bila kwenda chini na kuhitaji major repair itakayogharimu si chini ya Dola milion 10. Halafu baada tu ya kununuliwa Dowans itayeyuka majini na mtengenezaji wa mitambo ndo atasema ukweli.
Let's go out tutangaze tenda mapema (ilikuwa possible since july last year tulipovunja mkataba na Dowans). Shetani na mungu wote wanajua kuwa tulipovunja mkataba na Dowans tulikuwa na mahitaji ya umeme. Ingetangazwa tenda sasa hivi tungekuwa tuko kwenye final touches za kupata mitambo mipya. Wakati mkataba wa Dowans unavunjwa watu ndani na nje ya TANESCO walikuwa buzy kuandaa mazingira yatakayosababisha kununuliwa mitambo ya Dowans iwe kama kusukuma mlevi.
Muda huo ndo sasa na wamepata new and unexpected supporters. Sasa ni wakati wa kula. Dr. I may go ahead and buy the Machines. He knows what he will be buying. But he know also that in Tanzania it is easy to get away especially when you are well connected. He has important people who trust him. What he fears is to blow-up their trust. This will happens if he buys Dowans. I bet he doesn't.
And Zitto, the staunch supporter of Dowans? Well let's wait and see him join Kaburu, his homeboy. Keep your eyes open, it will happen men/women!!!!!
Nadhani Dr. anatakiwa aajiri Strategic planning manager pia.
Wakuu,
Hivi kelele zote hizi bado hakuna anayesema mtambo mpya wa kununua huu hapa?
Angalau Zitto ameonyesha hafuati upepo na yuko tayari kukosa umaarufu wa kisiasa kwa kitu anachokiamini.
Wanasiasa wote wamehamia Dar kupiga kelele za mtambo, hakuna uamuzi unachukuliwa, nchi giza totoro baada ya muda tunajiuliza eti kwanini hatuendelei?
Haya makundi yanayopingana yangeliweza kukaa pamoja na kujadiliana kwa wiki na kisha kuamua cha kufanya sio kama sasa wanasiasa wamegeuka watalaamu wa umeme.
Wacha wengine tuwajibike!
PM hakuna kitu kuhusu ZITTO, ameshaingia mkenge na mimi binafsi ile blank support niliyokuwa natoa kwa Dr. Slaa na kina Zitto naiamishia kuanzia leo kwa Dr. Mwakyembe, Mama Kilango na Seleli.
Zitto tulikuwa naye hapa for almost 4 days tukimpa mambo ya jikoni na mikorogo itakayotokea, lakini katupuuza na kututukana.
Sasa kweli ukimpa hayo mahojiano mtu ambaye hajui Tanzania, ukamuambia guess yupi ni kutoka chama cha upinzani, si atapick Dr. mwakyembe??
Dr. Mwakyembe hapa anatetea maslahi ya nchi na sisi wananchi, na Zitto anatetea maslahi ya Dowans, simple as BLACK and WHITE.
Halafu Mh. Zitto usipende kuchanganya mambo kwa kumention tu vitu unavyoambiwa eti serikali inakosa bilioni 58 watu wa migodi kwenye mafuta wanayotumia kwenye private generator zao, je kisa ni sababu hatujanunua mitambo ya Dowans au kisa ni misamaha ya kijinga serikali inayotoa na jie bunge kuridhia??? Unafikiri hata kukiwa na umeme, watu wa migodi watatupa generator zao au watatumia hiyo loophole ya tax refund kwenye mafuta ya hizo generator??? Give me a break!!!
Wewe acha maneno mingi bwana, unataka kuniambia ZITO hajui anachokifanya?. Hivi unajua humu janvini Zito alifikia hatua ya kutukana watu? Hakujua alichokuwa anafanya?. Tulishaamua kupambana na MAFISADI basi hatua haja kumwangalia mtu usoni.
Zito ni Fisadi kama MAFISADI wengine hivyo hatuna urafiki naye maadamu tumeshaamua kupambana na mafisadi. Ukweli nikuwa tunasikitika lakini hatuna Jinsi. Mimi nimeshaandika huko nyuma kwamba Wapenda mageuzi tumepata pigo sana. Mimi sina umaarufu wowote lakini napenda mageuzi sana. Tuliyemweka mbele tukamwamini ametusaliti sasa unataka tucheke naye.
Fisadi ni Fisadi 2.
Moelex23;
Usimpe mtu yeyote a blank check iwe Dr. Mwakyembe, Seleli, Mama Malecela, Zitto, Slaa etc.
Dont give anyone a blank check, they all need to qualify for one.
- Zitto inaelekea (a) Ana-kaulevi ka madaraka aliyopewa kwenye kamati, (b) Ana-ukosefu wa uzoefu wa mambo ya uongozi na biashara (c) Ameonyesha kuwa ni mgumu kukubali hard criticism. Lakini at least he has a record behind him ya kupigania wananchi. Tusimuweke pembeni bali tuendelee kumdadisi na kumsaidia ikibidi.
- Lakini mtu kama Mama Malecela sio wa kuamini kabisa, she is a populist na sijaona matendo yake yakafanana na anayopigiaga kelele. Ameifanyia nini nchi hadi hivi sasa badala ya kujipandishia tu chati kwa kelele bungeni?
- Dr. Mwakyembe na Seleli wana maneno mazuri tunayotaka sikia, lakini hawajawahi kusimamia kidedea issues ambazo wanazijua kwa undani kuliko watu wengine na zina utata hadi leo (Richmond-Dowans). Baada ya kuandika ripoti, Dr. Mwakyembe akiwa ni mwanasheria, je wamefanya nini zaidi kuhakikisha kuwa Richmond-Dowans inakuwa dealt with once and for all?
Mitambo haijatengenezwa na DOWANS ila DOWANS walinunua kutoka katika kampuni inayotengeneza mitambo hiyo. Katika hili naamini ni muhimu kufuatilia zaidi na kujua jinsi gani Tanzania itaathirika ama kufaidika itakapotokea matatizo yanayohitaji uhusika wa waliotengeneza mitambo hiyo na kujua mikataba kati ya DOWANS na hiyo kampuni inasemaje na kampuni yenyewe ina hali gani kwa sasa tukichukulia hali ya kiuchimu duniani.
Again kaka ingawa una tone kali katika huu mjadala lakini wazi kuwa upo genuine katika nia na mawazo yako.
omarilyas
Kwa karibu masaa sita ka nzi kalikuwa kametulia kwenye ukumbi makao makuu ya Tanesco ambapo Mkurugenzi wa Shirika hilo Dr. Idris Rashid alikuwa aje kuzungumza na waandishi hususan suala kununua majenereta ya kufulia umeme ambayo yanamilikiwa na kampuni yenye utata wa umiliki wake na yenye kuhusishwa na kampuni ya kifisadi ya Richmond, Dowans.
Hata hivyo, muda si mrefu uliopita mtumishi wa Tanesco aliingia ukumbini na kuwaambia waandishi waliokuwa wanasubiri kwa muda mrefu kuwa Bw. Idris hatozungumzia nao na kuwaomba radhi.
Hata hivyo, vyanzo vyetu vyenye uwezo wa kupenya kuta na madari vinadokeza kuwa suala la Dowans limefikia mahali pagumu ambapo sasa Tanesco wako tayari kuachana na wazo hili ili kutafuta vyanzo vingine vya umeme wa dharura na ya kuwa wametilia maanani "kelele" za wadau mbalimbali. Hili linakuja baada ya sauti za Spika wa Bunge la Muungano Mhe. Samuel Sitta na Mbunge wa Kyela Mhe. Harrison Mwakyembe kupaza sauti zao kupinga mpango huo. Ujumbe ambao umepokelewa toka kwa watunga sheria hao ni kuwa yeyote atakayenunua majenereta ya Dowans ajiandae kuwajibika Dodoma kama walivyowajibishwa wengine!
Tishio hilo ambalo limepokelewa kwa hisia ya kunyong'onyea limetuma ujumbe ulio wazi kuwa endapo serikali itatekeleza au kutoa baraka kwa Tanesco kufanya kitu ambacho wanajua hawapaswi kufanya basi patakuwa hapakaliki. Hadi hivi sasa kundi kubwa la wabunge waliosimama upande wa ripoti ya Kamati Teule kuhusu Richmond, limeshajipanga tayari kuanzisha "kasheshe" jingine ambalo linaweza kabisa kuitikisa serikali.
Hata hivyo, Dr. Idris inaonekana bado amekuwa na 'kichwa ngumu' hasa baada ya serikali na kamati za Bunge zote kuiachia uamuzi wa mwisho kuhusu suala la mitambo. Hata hivyo, kuna imani kuwa alichofanyiwa Dr. Idris ni kupewa kisu ashike, tatizo ni kuwa amepewa upande wa makali huku mpingi ukiwa umeshikwa na wengine ambao wako tayari kuuvuta.
Kutokana na hili, kuna kila dalili Dr. Idris anaweza kutangaza kujiuzulu wadhifa huo kitu ambacho alijaribu kukifanya muda si mrefu uliopita kuhusiana na suala la kampuni ya saruji ya huko Tanga. "Hayuko tayari kujitundika mwenyewe kitanzini kwa kamba yake mwenyewe!" amedokeza mmoja wa watu wanaojua suala hilo.
Sasa hivi kinachosubiriwa ni muda tu kuona Dr. Idris atafanya nini huku akijua kuwa tayari anahusishwa na kashfa ya rada suala ambalo nalo hajalitolea maelezo yoyote. Hadi hivi sasa uchunguzi wetu unaonesha kuwa asilimia 90 ya uamuzi uliofikiwa hadi sasa ni kutoendelea na suala la Dowans.
Hata hivyo upande mwingine bado unadokeza kuwa endapo serikali haitanunua mitambo ya Dowans na hivyo kuwasababishia hasara "wawekezaji" hao ambao walikuwa na uhakika kuwa serikali itanunua mitambo hiyo basi Watanzania "watakiona" kwani upungufu mkubwa wa umeme ambao tulidokeza unakuja mwezi wa nne, utaifanya serikali iipigie magoti Dowans na hata kununua majenereta yale yale katika bei ya juu!!
"Watanzania hawawezi kuvumilia kukaa gizani muda mrefu hasa huku mjini, kwa hiyo usishangae hao hao wanaopinga sasa wakaja baadaye kutaka serikali inunue mitambo hiyo aidha kutoka kwa dowans au kwa mtu atakayekuw ameinunua" alisema mdokezaji huyo.
Uwezekano wa kutokea yote mawili ni mkubwa zaidi. Hata hivyo, kama dhamira ya kuwalipa Dowans kwa gharama yoyote itatekelezwa basi kuna dalili Dr. Idris na timu yake watacheza bahati nasibu na kuendelea na mradi huo wakijua kuwa huko Bungeni tayari wana kura za kutosha kuzuia mapigo ya kina "mwakyembe".
Zito ni Fisadi kama MAFISADI wengine hivyo hatuna urafiki naye maadamu tumeshaamua kupambana na mafisadi. Ukweli nikuwa tunasikitika lakini hatuna Jinsi. Mimi nimeshaandika huko nyuma kwamba Wapenda mageuzi tumepata pigo sana. Mimi sina umaarufu wowote lakini napenda mageuzi sana. Tuliyemweka mbele tukamwamini ametusaliti sasa unataka tucheke naye.
Fisadi ni Fisadi 2.
Omari kaka, sio "spin" sasa makampuni makubwa yanaajiri Strategic Managers/Directors, kwa ajiri ya kuandaa Long term objectives na strategic missions. Kuna pia "Strategic Business" ambayo inatakiwa iwe directed na huyu Strategic Manager.
Kwa majibu hayo machache tu inaonyesha kuwa kwa msimamo wa Serikali, Dr. Mwakyembe na kundi lake wameanguka na Mh. Zitto na kundi lake wameibuka kidedea.
Lakini tusubiri filimbi ya mwisho..
==========Moelex23;
Usimpe mtu yeyote a blank check iwe Dr. Mwakyembe, Seleli, Mama Malecela, Zitto, Slaa etc.
Dont give anyone a blank check, they all need to qualify for one.
- Zitto inaelekea (a) Ana-kaulevi ka madaraka aliyopewa kwenye kamati, (b) Ana-ukosefu wa uzoefu wa mambo ya uongozi na biashara (c) Ameonyesha kuwa ni mgumu kukubali hard criticism. Lakini at least he has a record behind him ya kupigania wananchi. Tusimuweke pembeni bali tuendelee kumdadisi na kumsaidia ikibidi.
- Lakini mtu kama Mama Malecela sio wa kuamini kabisa, she is a populist na sijaona matendo yake yakafanana na anayopigiaga kelele. Ameifanyia nini nchi hadi hivi sasa badala ya kujipandishia tu chati kwa kelele bungeni?
- Dr. Mwakyembe na Seleli wana maneno mazuri tunayotaka sikia, lakini hawajawahi kusimamia kidedea issues ambazo wanazijua kwa undani kuliko watu wengine na zina utata hadi leo (Richmond-Dowans). Baada ya kuandika ripoti, Dr. Mwakyembe akiwa ni mwanasheria, je wamefanya nini zaidi kuhakikisha kuwa Richmond-Dowans inakuwa dealt with once and for all?