Kwako SteveD, Zitto akiwa criticized unasema aachwe; haya sasa ndio matokeo yake.
Cool aid na massage ya watu aina yako (wanaosema mitambo ya Dowans inunuliwe kwa sababu April kutakuwa na shida ya umeme!) imempelekea Zitto kuyumba. Mwisho wa siku maslahi ya Taifa nyuma au kando!
Hakuna anayekataa option ya kununua mitambo mipya kabisa. Hakuna na hakna sehemu nimesema lazima Dowans. Unatukana wabunge kuwa ni ****** na flip flop? Natumai umeropoka tu katika hili.
Tupo wabunge makini, tumesoma vizuri na kuendele kujisomea na tunaelewa. TANESCO wamesema waziwazi kuwa mbadala wa kununua mitambo ya dowans ni kununua mitambo mipya kabisa.
Kamati ya Bunge imesema kamati mbili zikae na kujadili kupata mwafaka. Sijui la ziasa ni nini hapa.
Siungi mkono ujambazi wowote.Pia nipo tayari kusimama mwenyewe na kuelezea ninachoamini. Nipo tayari kubaki peke yangu iwapo ninachofanya ninaona ni sahihi na nipo genuine. Katika hili mimi na kamati yangu tupo genuine na hatuna maslahi yeyote zaidi ya kuona shirika linaendeshwa kwa faida na hivyo nasi kuwa na national champion.
I stand with the decision of my committee kwamba Kamati mbili zikutane na kujadili suala hili. Kiongozi lazima awe tayari kuchukua maamuzi magumu. nipo tayari kuwajibika kwa hili.
Ninasimamia uamuzi wa Kamati yangu kuwa suala hili liangaliwe objectively na kama itaonekana kuwa ununuzi wa mitambo hii ni manufaa kwa nchi inunuliwe.
Kwa hiyo unasimamia uamuzi wa kununua mitambo ya Dowans iwe at the expense ya watu kula majani, au hata kama hiyo mitambo ni mikuu kuu, au mipya ya hiyo inayoweza kupatikana kwa bei ya chini zaidi?
Unamaanisha ni wewe (unasimama) pekee unayeweza kufanya kitu sahihi na genuine. U-dictator au unaona Watanzania wote ni vilaza isipokuwa wewe tu ndio unayejua/kuona/kupembua sahihi na genuine!
Kama kuna mitambo ya bei nafuu zaidi na mizuri zaidi MIPYA inunuliwe.
Wewe Zitto umepata access ya taarifa zote muhimu. Umepata fursa ya kuhojiana na wataalam wa TANESCO. Umepata wasaa wa kujadili sheria ya manunuzi. Sasa leo ukianza kuzungumza kama hivi unakuwa sio kiongozi. Kama kiongozi mpaka sasa unatakiwa uwe una msimamo wako-uliotokana na taarifa ulizo nazo. Wewe inabidi uwe straight forward kama unaunga mkono ununuzi au lah. Na kama unaunga mkono basi ueleza wananchi why so? Hata wasipokuunga mkono, hakuna shida lakini sema unachoamini - kwa sababu una taarifa ambazo wengine hawana. But please at this time usije na kauli kama hizi as if hujui kama inafaa au haifai. Na kama mpaka sasa hujui kama mitambo hiyo inafaa au lah, basi jitoe tu kwenye hiyo kamati, kwa sabbau hiyo kazi huiwezi. Huhitaji kukaa na kamati yoyote ili uwe na msimamo. Kukaa na kamati kukuwezeshe kutetea hoja yako tu. Sasa basi elezea waziwazi msimamo wako hapa JF-of course kama unao- na achana na kauli za kutaka vikao vya kisiasa.
Zitto watu tulikuamini sana lakini kwa hili la Dowans umetuvunja moyo na tukuone kuwa na wewe kumbe unaweza kuhongeka tu kirahisi na huyu fisadi Rostam Azizi. Hiyo Dharura mnayoisema kumbe ni ya miaka miwili ijayo na pia bei mnaambiwa ya kununua mitambo mipya ni rahisi kuliko hii mitumba ya Dowans. Kwanini mnang'ang'ani kununu hii mitumba? Maana kuna gazeti moja juzi kama sikosei limekuquote ukisema kuwa sheria ya manunuzi ibadilishwe ili mitumba ya Dowans inunuliwe. Hapa si bure mwenzetu umeshachukua chako tayari. Na kuna uvumi usio rasmi kuwa wewe siku hizi unatembelea gari la nguvu "Hammer" na inaonekana ni mojawapo ya zawadi ulizopewa ufumbe mdomo juu ya hawa mafisadi na ufanikishe biashara zaoa haramu. Kwakweli umetuangusha sana vijana wenzako. Tulikutegemea kuwa wewe ungeweza kuwa Obama wetu kumbe wapi.
Nimepata taarifa zote ni kweli. Kamati yangu ilikubaliana na TANESCO kimsingi lakini tukasema sio vizuri kamati mbili za Bunge kupingana na hivyo kuomba kamati mbili zikutane labda wenzetu wana sababu zaidi.
Sheria ya manunuzi inasemwa kweli ndugu yangu lakini hakuna hata mtu mmoja hapa ambae kaja na kutoa kipengele gani cha sheria ya manunuzi kinakataza. Sijakiona mie. Hebu tazama na wewe, just google the Act na utueleze. Unajua sheria ya manunuzi inazungumzia kuanzia chaki shuleni mpaka vifaa complicated vya jeshi. Sheria haiwezi kuwa general (nunua kitu kipya...............). Huo mjadala pia hapa sijauona. Tunasema tu, sheria ya manunuzi, hatusemi kipengele gani na kwa mazingira gani.
Pia katika ununuzi huu, TANESCO ndio walibid kununua na sio TANESCO waliotangaza tenda. Katika mazingira kama haya sheria ya manunuzi inasemaje?
Ndio maana katika kikao hicho Kamati yangu ilishauri kuwa PPRA wawepo ili kuwa clear na masuala ya sheria ikiwemo kama kuna waiver inatolewa katika mazingira gani.
Tatizo mjadala huu umechukua emotions zinazotokana na richmond etc (which i understand) na hivyo kupoteza objectivity kwa kiasi kikubwa
Umeniwekea maneno. Ninasimamia uamuzi wa kamati yangu kuliangalia suala hili objectively na kama nchi itafaidika mitambo inunuliwe. Kama kuna mitambo ya bei nafuu zaidi na mizuri zaidi MIPYA inunuliwe.
I am never a dictator, but a bold leader. I am able to tell people what they dont want to hear. I always subordinate my personal interest to those of the nation. Always and i can prove that. I stand to be counted
I am never materialist. I am never corrupt. I am genuine. I am honest. I speak my mind. Never been slippery.
Facts peke yake ndio zinanifanya nibadili msimamo. Sio hisia za kupoteza umaarufu nk. Umaarufu nilionao (kama ninao) ni earned popularity, na sio sought! Siwezi kuogopa kuchukua maamuzi eti kwa sababu ya kupoteza umaarufu. Kama ni maamuzi magumu na ninaamini ni sahihi nitachukua na one day the truth will be known. Truth prevails.
Umeniwekea maneno. Ninasimamia uamuzi wa kamati yangu kuliangalia suala hili objectively na kama nchi itafaidika mitambo inunuliwe. Kama kuna mitambo ya bei nafuu zaidi na mizuri zaidi MIPYA inunuliwe.
Oh siku hizi natembelea HUMMER? Unaamini uvumi huo sio? Nilinunua HUMMER mwaka 2007 na nilianza kuitumia mwezi June na sikuipenda maana ilikaa kitajiri mno na kuiuzilia mbali.
Sasa unasema sasa hivi nina HUMMER....... Haya unaweza kutunga uongo na ukauamini.
Hii nimei-copy toka Nipashe:
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe, amesema ni vigumu kununua mitambo ya kufua umeme ya Dowans, kwa sababu licha ya kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma na maazimio ya Bunge, kampuni hiyo imefungua kesi dhidi ya serikali na Tanesco katika mahakama ya usuluhishi huko Paris.
Ni kweli kuna kesi. Ni kesi ya kuvunjwa kwa mkataba. Hakuna kesi ya equipments. Kuna tofauti kati mambo haya. Suala hili la kesi linakuja sasa na sio kabla. Kamati ya Nishati na Madini inajua zaidi kwa nini suala hili halikusemwa kabla. Kipengele gani cha sheria ya manunuzi kinachosemwa hapa?
Mwakyembe amesema anashangazwa na hatua ya Tanesco kung`ania mitambo ya Dowans, wakati tayari wamiliki wake wamewashtaki serikali na Tanesco huko Ufaransa.
``Dowans wametupeleka Paris katika Mahakama ya Usuluhishi, sasa iweje tung`ang`anie kununua mitambo yao katika hali kama hii,`` alisema Dk. Mwakyembe katika mahojiano maalum na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema uamuzi wa kununua au kutonunua mitambo hiyo upo mikononi mwa Tanesco, iwapo shirika hilo linang`ang`ania kufanya hivyo kinyume na ushauri wa maamuzi ya Bunge.
Bunge halijawahi kukaa mahala popote na kuiambia TANESCO msinunue mitambo. Wala Bunge halijawahi kupokea taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusu suala hili. Kanuni za Bunge zinasema maamuzi ya Kamati ni yale yaliwasilishwa Bungeni na kuamuliwa. Hilo halijawahi kutokea. Uamuzi gani wa bunge unaosemwa hapa?
Alisema kumekuwa na ujanja ujanja mwingi unaotumiwa na menejimenti ya Tanesco kuhakikisha kwamba inafanikiwa kununua mitambo hiyo kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma na maazimio ya Bunge.
Alisema uongozi wa Tanesco ``unafanya usanii`` katika kutaka kuhalalisha uamuzi wake wa kununua mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans.
Dk. Mwakyembe ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, alisema Tanesco imekuwa ikitafuta mbinu za kuhalalisha uamuzi wao wa kununua mitambo ya Dowans ambayo kisheria hairuhusiwi kufanya hivyo.
Dowans ambayo ilirithi mkataba batili wa kampuni tata ya Richmond Development LLC ya Marekani, haifahamiki mmiliki wake kisheria.
``Sisi tunasema kama kununua wanunue, wameomba vibali mara ngapi, wananunua sijui nguzo!!! wamekuja lini kwetu. Naamini kwenye hili wamegundua kuna kitu hakiko vizuri ndio wanataka kuhalalisha,`` alisema.
Alisema kamati yake ilitoa maoni, ila kuna ujanja wa aina fulani, ``Sijui wanataka nini, kana kwamba kamati nyingine ina mamlaka ya kupokea rufani dhidi ya kamati nyingine kuna aina fulani ya usanii kwenye uongozi wa Tanesco.``
Alifafanua kwamba 14, Desemba, 2008, kamati yake ilipokutana na uongozi wa Tanesco, Wizara ya Nishati na Madini pamoja waziri mhusika, waligundua kwamba Bodi ya Tanesco ilikaa siku 10 kabla na kukataa kata kata wazo la kununua mitambo ya Taneco.
``Hata hivyo, menejimenti ya Tanesco iliizunguka Bodi na kuja kwetu na sasa wamezunguka na kwenda kwa Kamati ya Hesabu na Mashirika ya Umma , ikiomba kibali cha kununua mitambo hiyo,`` alisema.
Alisema kazi ya Bunge ni kusimamia na sio kujiingiza katika shughuli za utendaji wa kila siku wa Tanesco, lakini akaonya kwamba iwapo itabainika kuwa taratibu zimekiukwa katika ununuzi huo na kuliingiza taifa katika balaa, wahusika watawajibishwa.
Alisema uongozi wa Tanesco, ``unafanya usanii`` katika kutaka kuhalalisha uamuzi wake wa kununua mitambo ya Dowans.
Dk. Mwakyembe alifafanua kwamba Tanesco imekuwa ikitafuta mbinu za kuhalalisha uamuzi wao wa kununua mitambo ya Dowans ambayo kisheria hairuhusiwi kufanya hivyo.
Alisema menejimenti imekuwa na ujanja ujanja mwingi kiasi cha kuizunguka kamati yake, na kuwasilisha maombi ya kununua mitambo hiyo kwa kamati nyingine ya Hesabu na Mashirika ya Umma (POC).
``Sisi tulitoa maoni, Tanesco ina ujanja wa aina fulani, sijui wanataka nini, kana kwamba kamati nyingine ina mamlaka ya kupokea rufani dhidi ya kamati nyingine,kuna aina fulani ya usanii kwenye uongozi wa Tanesco,`` alisema na kuongeza
``Kama wanataka kununua, wanunue na sisi kazi yetu ni kusimamia tu na sio kuwaagiza kwamba wanunue au wakatae. Watakapoamua kununua wajue kwamba wanafanya hivyo kwa misingi ya kanuni na sheria, la sivyo watawajibika,`` alisema.
Akizungumzia mjadala wa ununuzi wa mitambo ya Dowans, Dk. Mwakyembe alisema anaona umepata sura ya kisiasa, na anaona kama ni mwendelezo wa Operesheni Sangara.
``Nimesikia na kusoma kuhusu Mwenyekiti wa POC, Zitto Kabwe kwamba kamati haijawasilikiliza Tanesco. Kamati ilikutana na Tanesco na Wizara 14 Desemba mwaka jana na kuwasikiliza, kwamba hatujawasikiliza hilo si kweli,`` alisema.
Kamati ya Nishati na Madini hawakuisikiliza TANESCO tarehe 14 kwani walisikiliza serikali. Taarifa za Bunge zinaonesha dhahiri kabisa kuwa TANESCO hawakusema katika kikao hicho kwani kamati ilipomsikiliza Waziri ikatoa uamuzi.
Naye mbunge wa Nzega CCM, Lucas Selelii, amesema hatua ya baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali kupigia debe ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans kinyume na maamuzi ya Bunge, inaleta wasiwasi.
Alisema ana wasiwasi kwamba huenda kuna mkono wa mtu, anayeshinikiza kununuliwa kwa mitambo hiyo, kinyume na maazimio ya Bunge.
Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liinunue mitambo hiyo.
``Kuna mkono wa mtu, tena mkono wenyewe ni wa chuma, kwanini maamuzi yetu wenyewe tunayakanyaga, kama wanapinga, turudi bungeni,`` alisema Selelii jana wakati akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake.
suala hili halijawahi kupelekwa Bungeni. Ninaelewa kwa nini baadhi ya wajumbe wa Kamati hawataki mjadala huu kwani wanajua kuwa sehemu ya maamuzi yao yalikuwa sio sahihi na hayakufuata kanuni za Bunge.
Alisema suala la ununuzi wa mitambo hiyo lilitolewa kama pendekezo na Kamati Teule ya Bunge na kuridhiwa na Bunge kwamba mitambo hiyo isinunuuliwe.
Alisema kwanza, katika uchunguzi wa kamati hiyo iligundulika kwamba mitambo hiyo ni mibovu na pili gharama za ununuzi wake ni kubwa.
Kamati ya Nishati na Madini haijawahi kufanya uchunguzi kuhusu mitambo hii maana wao hawana utaalamu huo na wala fedha za kufanya uchunguzi wa kitaalamu. Iwapo Kamati mbili zingekutana na kuamua kufanya uchunguzi ingetakiwa Bunge litanagaze tender ya kupata consultant wa kufanya kazi hiyo. Hakuna taarifa Bungeni za uchunguzi huo ambao Selelii anasema walifanya na kugundua kuwa mitambo ni mibovu. TANESCO wao mefanya uchunguzi wa kitaalamu. Sasa tuwasikie wanasiasa au wataalamu?
Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, ni makosa kwa serikali kununua vifaa ambazo vimetumika (mitumba).
Kipengele gani cha sheria ya manunuzi na katika mazingira yepi?
Alisema kiasi cha fedha ambacho kinatakiwa ili kununua mitambo hiyo, kinaweza kununua mitambo mingine mitatu yenye ukubwa na uwezo huo huo wa kuzalisha umeme.
Selelii alisema serikali inaweza kufanikisha ununuzi huo kwa kutuma barua pepe Marekani ambako mitambo hiyo hutengenezwa au inaweza kumpeleka ambaye atashughulikia ununuzi wake na hivyo kurudi nchini akiwa na mitambo mitatu.
Rhetorics ambazo hazitaipeleka nchi popote. Unawezaje kununua turbines kwa barua pepe? let us be serious
Alifafanua kwamba Kamati Teule ya Bunge ilikwisha kamilisha kazi na mapendekezo yake yaliridhiwa na Bunge na suala hilo sasa lipo chini ya Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge.
Alisema atashangaa iwapo Kamati hiyo ambayo ipo chini ya Mwenyekiti, William Shellukindo, itakapokiuka maazimio ya Bunge.
Kwa upande wake, Mbunge wa Karatu, Chadema, Dk. Wilbrood Slaa, alisema kinachohitajika katika suala hili ni taarifa kwa taifa.
``Tunaingizwa katika mjadala, wakati hatujui yaliyomo kwenye Kamati ya Shellukindo na wala katika Kamati ya Zitto,`` alisema na kuhoji: ``Kwa nini kamati hizi mbili kila moja inashikilia msimamo wake.``
Alisema haijulikani serikali na Tanesco walikubaliana nini katika Kamati ya Zitto, na kuongeza kuwa ni vema kujadili suala ambalo mmoja amepewa taarifa zake.
Alisema hadi sasa hakuna mtu anayejua kwa uhakikia nini yaliyomo katika Kamati hizo, suala ambalo ni gumu kulijadili.
Slaa shows leadership here. Kwa nini kamati ya Nishati na Madini inakwepa kikao cha pamoja?
Alisema Kamati ya Mwakyembe ilitoa taarifa kuhusu mitambo ya kufua umeme ya Dowans, kwamba serikali inaweza kupata na kununua mitambo hiyo huko inakotengenezwa tena kwa bei nafuu.
Lakini alisema: ``Tunataka kujua maazimio ya Bunge kuhusu sakala la Richmond yamefikia wapi kwa sababu kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya Umma, iwapo mtu amebainika kughushi na kuingia mikataba, mali zake zinatakiwa kutaifishwa.``
Alihoji iwapo mkataba wa kufua umeme wa dharura kati ya Tanesco na kampuni ya Richmond, (sasa Dowans), ulibainika kuwa umeghushiwa, sheria imefuatwa ya kutaifisha mitambo hiyo.
Alisema badala yake kuzingatia taratibu hizo za kisheria, tunazungumzia hitaji la kununua mitambo hiyo.
Hata hivyo, alisema dharura hii ya umeme si ya leo, na ina tofauti gani na ile ya miaka iliyopita.
Juzi (Jumamosi), Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuelezea hali ya umeme katika Grid ya Taifa pamoja na mambo mengine, akapendekeza kuwa mtambo wote wa Dowans ununuliwe na serikali pamoja na vifaa vyote vya kuunganishia kwenye grid suala la ununuzi wa mitambo iliyotumia katika sheria ya Manunuzi iangaliwe kwa makini kwa manufaa ya sekta ya umeme na mbadala wa kununua mtambo wa Dowans ni kuagiza mara moja mitambo ya kukodisha ya umeme ya kiasi cha megawati 150 kwa njia ya dharura, ambayo inapaswa kuwepo kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.
Mhe Zito:
Kila unapojaribu kujitetea ndio unavyozidi kujichafua..... nakushauri warudishie hela waliyokuhonga!!!!
Kwako Zitto
Swali kwako Zitto: Je hii kesi kati ya Dowans na Tanesco imeshakwisha na mamuzi yakoje? Mbona mitambo iliyoshikiliwa kwa kufidia kesi kamaTanesco watashinda sasa inauzwa kwa Tanesco wenyewe? Hapa kuna mkanganyiko na kila dalili za rushwa. Bwana Zitto hebu tupe maelezo kuhusu hili.
Umeniwekea maneno. Ninasimamia uamuzi wa kamati yangu kuliangalia suala hili objectively na kama nchi itafaidika mitambo inunuliwe. Kama kuna mitambo ya bei nafuu zaidi na mizuri zaidi MIPYA inunuliwe.
I am never a dictator, but a bold leader. I am able to tell people what they dont want to hear. I always subordinate my personal interest to those of the nation. Always and i can prove that. I stand to be counted
I am never materialist. I am never corrupt. I am genuine. I am honest. I speak my mind. Never been slippery.
Facts peke yake ndio zinanifanya nibadili msimamo. Sio hisia za kupoteza umaarufu nk. Umaarufu nilionao (kama ninao) ni earned popularity, na sio sought! Siwezi kuogopa kuchukua maamuzi eti kwa sababu ya kupoteza umaarufu. Kama ni maamuzi magumu na ninaamini ni sahihi nitachukua na one day the truth will be known. Truth prevails.