Zitto Ameomba msamaha kwa maneno yake makali aliyotoa, nadhani asamehewe 7X70
Mheshimiwa Zito, Maelezo yako kuhusu hali halisi ni mazuri sana na yanatia moyo, LAKINI baada ya hapo umetamka maneno makali sana. Dr. Slaa amewekwa kitimoto sana kama ulivyokiri hata wewe, lakini amejibu hoja kwa busara ya hali ya juu sana.
I am sure if you will go back and read what you wrote, you may not believe it yourself!!
Hata hivyo your apology is highly appreciated,
Hadi mtatoana ngeu! Nunueni mitambo ya Dowans, mwachilieni Gire.. yaishe! tuangalie mengine.
Disclaimer:: Just got back its around midnight my time with few drinks kichwani, but all in all: Lets go
Mh. Zitto, I was the one who made serious allegations of blackmail and/or corruption from Mtandao to U guys on this dowans issue. I'm not offended with ur reply though U used some slick words, but since I dished first, its all good.
Now, U are talking about serious problems within Tanesco, which we all agree but the cause of the problems are contracts that were signed in the same way U guys want to do with Dowans. Let us say Tanesco wants 200MW, so the solution is to buy 200MW generators from source companies ie GE or Wartsila right?? Here we all agree no middleman, and with the current financial crisis GE and Wartsila have very good prices, Google what other countries are doing. Unasema Tanesco wanalipa 84% ya mapato kwa kampuni zinazozalisha 42%, sasa tukinunua generators za Dowans, hiyo ratio itapungua?? No, kwa sababu haziingiliani ila ni maneno tu mnatumia kuchanganya wananchi wa vijijini, 84% blah blah, kwa hiyo on top of all those cash flow problems, solution ni kuongeza matumizi mapya ya $80 million to dowans kwenye mitambo chakavu?? Only in TZ.
Why do U insist on Dowans?? We all agree we need generators, but we want the generators from source companies where we will have warranties and other guarantees and a competitive price in this financial climate we are in.
Tanesco signed a bad deal with Songas, and Songas bought their generators from GE, Why don't we go to GE direct??? Mbona hao majambazi tukiwapa contracts wanakimbilia GE au Wartsila??? IPTL went to wartsila and Songas went to GE. This is our issue.
Now, U buy generators from Dowans, a company that does not generate electricity anywhere in this world, sasa baada ya manunuzi ikitokea tatizo na hizo generators tutaenda wapi mkuu?? Mbona Zitto tunakuamini sana lakini hapa unaact kama Viongozi wetu maboga??
Halafu unathubutu kusema eti mbona serikali inataka kununua mitambo ya IPTL, so vilevile tununue mitambo ya DOwans?? Really Zitto?? Unaona IPTL na Dowans ni sawa sawa?? IPTL tuko kwenye contract kuwalipa capacity charges kubwa mpaka 2018 I believe, so if tukinunua mitambo itasave money, WE ARE ALL UP FOR IT, sababu tutasave in the long run and it will cut down that 84% ratio U were talking about, which will improve Tanesco Cashflow situation. Sasa dowans, hatuna nao contract, kwa nini tununue mitambo yao?? PPRA ina maana gani??? Kwa hiyo msitake kuchanganya wananchi wetu huko vijijini kwa maneno mengi.
Ahsante mkuu, na I hope umeona kwa nini tunaissue na Dowans. U will do ur country a big service kama utatumia letterhead ya kamati kuandika barua GE and Wartsila kuulizia info tu ya NEW 100MW generators availability to Tanzania and at what price, then utaongea kama kijana mjanja na sio eti MD wa Tanesco kasema hivi na vile wakati unajua kabisa Chenge, Rostam, Karamagi, Lowassa wanashirikiana na huyo fisadi hapo Tanesco na Lowassa ndie alimweka hapo.
Dowans generators kwa habari za ndani zinaworth about $15 million, so sababu tunawadai $10milion, TUTAKUBALI KUNUNUA HIZO GENERATORS kwa $5million.
Kama hawataki, Powa tu maana hamna mtu yeyote dunia hii anayetaka kununua hizo generators, na mwisho wa siku Tanesco wakiwa wajanja na kusubiri, Dowans watatupa hizo generators bure maana hamna wanakoweza kupeleka.
Swali la mwisho::: Zitto hao Dowans unajua wanafanya kazi ya umeme sehemu gani dunia hii, ili wana JF walioko kona zote watembelee ofisi zao popote duniani tuone ufanisi wao???
"Suala kubwa ni ununuzi wa mitambo ya wezi au kama mitambo hiyo inafaa au haifai?" - Zitto.
Today I have heard the unexpected from this "fighter"!God bless Tanzania.
Hadi mtatoana ngeu! Nunueni mitambo ya Dowans, mwachilieni Gire.. yaishe! tuangalie mengine.
Halafu Mh. Zitto, mtiririko wa maamuzi ya maana inabidi uwe hivi:::
Tanesco imeona kuna upungufu wa 150MW
Tanesco itabidi inunue generator za MW 150
Generator hizo kwa sheria ya PPRA inabidi ziwe mpya
Tanesco itajaribu kuwasiliana na makampuni yanayotengeneza hizo generator ili tuweze kuzipata haraka na kwa bei nzuri
Na sio, unavyotulazimisha wewe yaani
Dowans wanataka kuuza generator zao kwa mabwege
Tanesco lazima inunue generator za Dowans
Sababu za kununua ni kuna upungufu wa 150MW
Mbona hata za IPTL zinataka kununuliwa??
Yaani hapo mkuu ndio umetuchosha kabisa kwa sababu lazima wewe mjanja kama sisi unayaona haya na ukiamua kutoyaona ndio yale maswala ya blackmail and/or corruption yanapokuja.
May god Bless Tanzania
Zitto, mimi nakuelewa sana lakini hili la Dowans linashughulikiwa kwa namna ya kushangaza sana. Langu ni moja tu. Nasema tununue mitambo itakayofaa kutupatia umeme tunaohitaji. Katika kufanya hivyo tusivunje sheria.
Maana yake:
a. Tenda itangazwe upya Dowans kama makampuni mengine ishindane fair and square.
b. Endapo baada ya tenda bado Dowans wakabakia miongoni mwa makampuni na wakawa kweli wanatupa kitu value for our money well and good.
c. Nje ya hapo tutatatua tatizo moja (la kukosa umeme) kwa kutengeneza tatizo jingine (la uvunjaji sheria, upendeleo, and unfair advantage!).
d. Kama itatokea kampuni nyingine ambayo inaweza kutimiza masharti yale ya tenda basi hiyo kampuni ipewe jukumu hilo.
Nimelazimisha wapi? Hakuna sehemu yeyote ambayo mimi nimelazimisha chochote na wala siwezi kufanya hivyo maana sio mamlaka yangu. Mimi nimeomba kikao cha pamoja cha kamati mbili (yenu - Nishati na Madini na yetu - Public Investments) ili kujadiliana na kupata mwafaka juu ya ushauri wa kutoa. Naomba isipotoshwe kabisa kuwa ninalazimisha chochote hapa.
Halafu Zitto naomba uwe careful sana, sababu sio kazi ya Bunge kujikita kwenye uendeshaji wa makampuni, nyie ni wasimamizi lakini wenzako wanakutega kwenye hii issue unaonekana wewe ndio unangangania hii issue ya Dowans, ingawaje mimi mwenyewe moyoni najua mambo ya kifisadi huna, lakini angle hii sababu wewe ni mwanasiasa inabidi uangalie angle zote mkuu.
Ndivyo nilivyoshauri kwa mujibu wa kanuni za Bunge. Kamati ya Nishati na Madini ilipokutana na Serikali haikutoa mbadala. Walikasirika na kusema hatutaki na kuondoka zao. Sisi tunasema hapana. Ninyi TANESCO njooni mueleze kamati hizi mbili, ile ya kisera na ile ya oversight. Kisha tunatoa alternative. Hivi ulivyoandika ndio fikra za kamati yangu. Busara ilitutuma kutotoa ushauri bila wenzetu kuwa on the loop. Hili lipo katika maandishi na ninaamini ipo siku litakuwa ni public domain.
zitto,
kutokana na mabandiko yako ina maana unapigia chepuo haya magenereta. I have got some questions to you.
Baada ya bunge kutoa mapendekezo serikali iliunda kamati tena kuangalia utelekezaji wa yale maazimio. Kwa mtazamo wako je? Utekelezaji wake umeekwenda kwa asilimia ngapi. Just guess tu sitaki upatie. Huoni kama yangekuwa yametekelezwa ingekuwa ni rahisi kwa wananchi na hata wewe kuridhia kuwa tuyanunue hata kwa mkopo?
Unajua watz wengi including myself ni/tuna mchukia sana sana sana rostam aziz? Amekuwa chanzo cha matatizo yote hapa tz mimi niko zangu huku kijijini kasulu wala sitaki kumsikia kwa gharama zozote. Unaleta na hili tena? Unamjua mmliki wa dowarns?
Hivi unajua wakati wa kushusha bei za mafuta washikaji wote walikuwa tayari kutembea kutoka tegeta kwenda kwenye vibarua vyao posta kwa miguu kuunga mkono ewura? Lije hili la dowarns? Tena mpaka mwezi wa nne? Tutajipanga tu kuliko? Nito tayari kuunga mkono hata kundamana kama yangekuwa hayo.
Hivi unajua akina mkwawa walikataa kukamatwa wakaamua kujiua? Huu ndo utaifa tunaouhitaji sio wa kuogopa mvua......... Pia kuna ile mikataba ya kiwira mbona hujaingumzia katika mipango yako ya tanesco? Huoni kama pia ni tatizo hililopelekea tanescon kwenye 84%?
Mwisho, zitto hulka yako haitofautiani sana na yangu lakini kwa kuwa umeshaamua kuwa mwanasiasa, plz kutugombeza na kutujudge sio mtaji hata kidogo. Nimeona hili muda mrefu pale watu wanapotofautiana na wewe. Pls sisi ndo mtaji wako. Tunakupenda sana ila chota hekima hii. Kuwa mstahimilivu na jua kuwa nchi hii inamatatizo mengi na we don need to hear rostam anymore.
Tatizo na ufisadi wa nchi hii ni rostam na sitaki kusikia amepewa hata penny
Hiyo paragraph ya mwisho mkuu,nimeshindwa kukupata!!Sheria ya manunuzi si msahafu,kweli.Lakini je,ndo tumeanza utaratibu wa kuvunja/kupindisha sheria zetu ili tu zikidhi matakwa fulani??Kwakuwa tu leo hii tunataka kununua mitambo used ya Dowans ndipo tusahau kuwa kuna sheria zinazotuongoza katika manunuzi??Hii ikiendelea tutajikuta tukisema kuwa sheria zote kwa ujumla wake sio misahafu,so where could there be the Rule of Law???Ushauri wako mzuri sana na nimeuchukua. Kuwa careful ni muhimu sana. Kuwa real na kuconfront existing problems ni muhimu zaidi. Tatizo tulilonalo ni kwamba hivi sasa nchi imekuwa polarised (kama ni sahihi neno hilo). Huwezi kuwa na hoja na watu wasikupe kundi. Hili ndio ninalolipnga kwa nguvu zote. Ni lazima watu wawe huru kufikiri na kusema bila kupewa makundi (and U did it).
As i said before, on IPTL it was a matter of exemplifying cases of waiver etc maana watu wanaona sheria ya manunuzi kama msahafu tena bila kutaja kipengele.
Hebu angalia 'waliofinance' kampeni za ccm kwa vipindi tofauti vya uchaguzi mkuu:Nik kweli kwenye taarifa za saa 2 usiku huko nyumbani Waziri Ngeleja amesema serikali wameiamuru Tanesco kutoshiriki kwenye zabuni ya ununuzi wa mitambo hiyo kufuatia ushauri wa kamati ya bunge.
Nadhani uamuzi wa awali ulichochewa na ushawishi wa watu fulani ambao wanaaminika kuimiliki Dowans; bila shaka ni mzimu wa Richmond bado unaiandama serikali.