S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 88
Susuviri,
Kwanza kabisa nianze na swali lako ambalo umeuliza kama Dorwan's ni kampuni ya Rostam na Lowassa..
Mkuu, nitasema:- NB:- Hapana KISHERIA, na Ndiyo KIUJANJA...
Kuna mchezo ambao unatumiwa na viongozi wa Tanzania pamoja na nchi nyingi maskini..
Kama ilivyokuwa Richmond, hutafutwa mtu wa kuaminika mwenye uraia nje ambaye anaweza kuwa Mbongo au mtu wa nje ambaye anaweza kufungua kampuni huko nje kihalali kulingana na deal lilipo Tanzania. Shirika hufunguliwa na wanahisa ndio hao viongozi wenyewe lakini hakuna kabisa mikono yao ndani ya shirika hilo. Hata hapo Bongo kina Manji, Load Rajpar, Jeetu Patel na wahindi wengine wengi tu wametumiwa ktk masdeal kama haya.. nadhani unakumbuka ile list ya Mob ya Mkapa na M Bank.. ni ktk mchezo huo huo.
Sasa tatizo la uharamu wa deal la Richmond KISHERIA sio mkataba wenyewe isipokuwa ni shirika lenyewe. Richmond ni kampuni hewa kama ilivyobainika lakini mkataba wake ulifuata sheria zote pamoja na kwamba hazikuwa for the interest of our Country, yet kisheria mkataba wenyewe ni genuine kama ilivyo mikataba mingine such as Barricks.. Sasa kufungiwa kanyaboya ktk mkataba na tukakubali na kuweka sahihi inatufunga sisi ktk Mkataba huo isipokuwa tu tatizo likaja kwa shirika lenyewe Richmond... Na kama unakumbuka Mh. dr Slaa alipoanzisha vagi la Richmond tulikuwa na kila haki kisheria kuvunja Mkataba kwa sababu kwanza walishindwa ku deliver kisha tukaja gundua kuwa halikuwa shirika halali Marekani wala Tanzania...
Kwa Ujanja ujanja bila kufuata sheria na haki tukapigwa changa la macho, mkataba kuhamishiwa shirika la Dorwans (Halali)ambalo pia tayari lilikwisha pangwa ili kuvuruga ushahidi wa Richmond kama shirika feki..
Sahihisho dogo tu mkuu Mkandara... aliyekuwa AG wakati wa Lowassa ni Mwanyika na si Chenge. lakini ufafanuzi wako ni mzuri sana, Umeweka wazi kwa kiasi fulani ni jinsi gani ambavyo Tanzania inaelekea kupoteza mchezo huu. Kosa tulilolifanya ni kutovunja mkataba wakati tulipobaini kuwa Richmond ni hewa. pale ndipo palikuwa pa kuchukulia point. lakini sasa tumeuvaa mkenge kwa sababu Dowans kama kampuni/shirika hawana matatizo yoyote, na mkataba waliorithi nao hauna matatizo yoyote. Ukichunguza kwa undani, katika kesi ambayo Dowans wamefungua, Richmond, ambayo sisi ndiyo tulikuwa na matatizo nayo, haihusishwi kwa karibu. Hivyo hapa sarakasi ni serikali vs Dowans, yale majigambo yetu kuhusu Richmond wala hayawezi kutusaidia kwenye kesi hii, tujiandae tu kuwalipa hawa wajanja fedha zetu
Yebo Yebo,
Nakubali maneno yako lakini unatumia sheria ipi hasa kwani huko Swiss wanataka kujua kuhusiana na Richmond!... Kama ilikuwa kampuni hewa swala sio kuuliza wao kwa nini ilikuwa shirika hewa bali kujiuliza sisi kwa nini tuliweka mkataba na shirika hewa Marekani ambalo kama sikosei lilisajiliwa Tanzania na account yao ilikuwa ikipokea malipo..Pili kisheria, kama lilikuwa shirika hewa waliweza vipi kuingiza nchini hizo generators na zikaanza kazi wakati tukifahamu ni shirika hewa..
Njew ya yoyte haya Dorwan's haihusiki na kabla hawajanunua mkataba sisi tuliwatazama uwezo wao na kupitisha mabadilishano..
Tulipokubali mabadiliko ni hatua ya kuonyesha hatua ama niseme hukumu yetu ktk kuliondoa shirika hewa badala ya kulifikisha mahakamani, hivyo Dorwan's kisheria tumeichagua sisi wenyewe...
Kwa lugha ya mtaani mkubwa wangu unaweza kumtumia ndugu ama rafiki yako kufunga ndoa hata kama yeye sio mme wa kweli.. Kisheria ndoa hiyo inakubalika maadam umeanguka na mke kaanguka sahihi na imekuwa registered..
Duh kama kulikuwa na kahuruma kidogo kutoka kwa muungwana naamini kataisha wamejichimbia kaburi let me take my wisky nibaki kusikilizaHehehehe yangu macho maana naona movie ya kumkamata Lowassa na Rostam hiyooo ndio inataka kuanza tunamalizia hili trailer la Epa na Alex Stewart then movie lenyewe linaanza, noja nitafute coca yanngu mie mapemaaaa
Naona Gemu la RICMOND bado bichi, hivi kwanini Muungwana asiwaweke Rostam na Edo kwenye kachumba kadogo kwa kuhujumu uchumi?
Kwa maelezo haya nakubaliana na Njia ya mkatao anayoshauri Kichuguuu, kwa sababu inaonyesha wazi baadhi ya watu ndani ya serikali wanataka bado kuhakikisha Dowans wananufaika na pesa na wavuja jasho wa Tanzania. Hivyo kwa kutumia sheria kuna uwezekano mkubwa tukauvaa mkenge. Afterall Wafaransa wana uchungu gani na nchi kama Tanzania? Hao majaji wakikatiwa na kuahidiwa mgawo baada ya kushinda kesi watakuwa na tatizo gani.Kama Uingereza walijua kuwa Rada wanayotuuzia sisi taifa masikini haikuwa tunayostahili na bei yake ilikuwa juu sana, lakini bado wakaona tuinunue,unategemea nini kwa Mfaransa??
Kama mkataba wa Richmond uligundulika ni feki kwa mujibu wa kamati then kuurithi mkataba huo hakuufanyi usiwe feki. Ni kuwa DOwans walirithi mkataba ambao ni batili
Mkuu sio majaji watakao tuhanithi ni hao hao waliopo Tanesco na Wizarani
Sasa Wanazuia hiyo mitambo kwa faida ya nani jee wakishindwa kesi itakuwaje kama ni kufuata ushauri wa mwanasheria wao ni bora watafute mwingine tuu
Hili tumeshalikoroga kabisa kwanza hata hiyo hasara waliyotupa watanzania inashinda hata ya Alex stewart
Yebo Yebo,
Nakubali maneno yako lakini unatumia sheria ipi hasa kwani huko Swiss wanataka kujua kuhusiana na Richmond!... Kama ilikuwa kampuni hewa swala sio kuuliza wao kwa nini ilikuwa shirika hewa bali kujiuliza sisi kwa nini tuliweka mkataba na shirika hewa Marekani ambalo kama sikosei lilisajiliwa Tanzania na account yao ilikuwa ikipokea malipo..Pili kisheria, kama lilikuwa shirika hewa waliweza vipi kuingiza nchini hizo generators na zikaanza kazi wakati tukifahamu ni shirika hewa..
Njew ya yoyte haya Dorwan's haihusiki na kabla hawajanunua mkataba sisi tuliwatazama uwezo wao na kupitisha mabadilishano..
Tulipokubali mabadiliko ni hatua ya kuonyesha hatua ama niseme hukumu yetu ktk kuliondoa shirika hewa badala ya kulifikisha mahakamani, hivyo Dorwan's kisheria tumeichagua sisi wenyewe...
Kwa lugha ya mtaani mkubwa wangu unaweza kumtumia ndugu ama rafiki yako kufunga ndoa hata kama yeye sio mme wa kweli.. Kisheria ndoa hiyo inakubalika maadam umeanguka na mke kaanguka sahihi na imekuwa registered..
ICC Paris inasema kwamba it is a standard arbitration clause that any dispute arising out of or under this contract shall be settled by arbitration in accordance with the rules of the CHAMBRE ARBITRALE DE PARIS (61, Bourse de Commerce, 2, rue de Viarmes, 75040 PARIS cedex 01, Tel:+ 33 (0)1 42 36 99 65, Fax : + 33 (0)1 42 36 08 54), of which both the Parties hereto declare to be cognisant and which they hereby accept .
Kutokana na hapo Juu ni wazi kwamba Tanesco hawana cha kujibu hapa kama hawaikubali au hawaikukubali tangu mwanzo hiyo ICC Paris , na kama wasipoikubali au kutoitambua basi ina maana kwamba hiyo kesi ya Dowan Hakuna , case ni Void ab nitio.
Kama TANESCO wanaikubali ICC Paris, ndani ya article 7 ya ICC Paris, wanachotakiwa ni either kujiwakilisha wenyewe na kutoa facts za case kama ambavyo Bunge la Tanzania chini ya Mwakembe lilivyogundua madudu ya Dowans au kumteua mwanasheria toka popote pale duniani na kuwawakilisha , na hili likisha fanyika basi hawa waliochaguliwa inabidi pia chini ya Arbitration Chamber of Paris organise arbitration in conformity with its legal status and follow regulations that define the different applicable rules during arbitration proceding.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ICC Paris soma hapa chini.
Chambre Arbitrale de Paris