Hatimaye serikali imeamua kutonunua mitambo ya Dowans SA kwa mujibu wa waliosikiliza BBC. Tovuti ya GlobalPublishers katika taarifa yao leo iliyoambatana na picha wamesema kuwa:
Picha hiyo ina maelezo yafuatayo:
Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Ngereja, leo alielezea azma ya Serikali kununua mtambo wa kuzalisha umeme Megawati 112 .5 kutoka kampuni ya Dowans ili kuongeza nguvu ya nishati hiyo kufuatia ongezeko la watumiaji wa Nishati hiyo. kulia ni Naibu wake Mheshimiwa Adam Malima.
My Original story (now corrected?)
ili kusaidia kupunguzo tatizo la nishati nchini. Uamuzi huo umetangazwa leo rasmi na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja pamojana Naibu Wake Mhe. Adam Malima.
Uamuzi huo umekuja licha ya pingamizi kubwa la Kamati ya Bunge inayoongozwa na Mhe. Shelukindo na licha ya taarifa ya kuufunua mchezo "uliochezwa" iliyoandikwa kwa kifupi tu kwenye "kijarida kimoja" uchwara ambacho kimelinganishwa na "radio mbao" kinachotoka kila jumanne kwenye mtandao!
Uamuzi huo yawezekana kuhitimisha mjadala wa wa Richmond na Dowans uliodumu kwa muda mrefu nchini. Kampuni ya Dowans kutoka Saudi Arabia, Afrika ya Kusini na Costa Rica ndiyo ilirithi mkataba usiokuwa halali wa Richmond.
Baadhi ya watumishi wa Richmond ndio pia walikuwa watumishi wa Dowans na mmoja wa maafisa wa juu wa Tanesco wakati wa mchakato wa Richmond ndiye alikuja kuwa mmoja wa wahandisi waandamizi wa Dowans.
Tetesi ya kijarida hicho (ambacho inadokezwa kinatarajiwa kuifunua zaidi Dowans wiki ijayo) zinasema kuwa kampuni ya Dowans inauhusiano na Afisa mmoja wa Kijeshi kutoka kutoka nchi moja ya Mashariki ya Kati mwenye uhusiano wa karibu na mmoja wa Wafanyabiashara maarufu nchini ambaye amekuwa akitajwa tajwa kwenye tuhuma za ufisadi na kuhusishwa sana na mkataba wa Richmond. Mfanyabiashara huyo ambaye ana nafasi ya uongozi wa kisiasa amekuwa akikanusha kuhusika na makampuni hayo!
Wachunguzi wa mambo ya nishati na siasa wanadokeza kuwa mfupa ambao ulimshinda Lowassa inaonekana Mhe. Ngeleja ameuweza.
Habari ndiyo hiyo!
I hate to be the bearer of bad news.. or is it?