Elections 2010 Double Standard

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
jana tume ya uchaguzi imetupilia mbali ombi la wakristu la kubadili siku ya kupiga kura (31 oct) kwani ni siku ya ibada.

Ivi kweli ingekua ni siku ya Ijumaa na waislam wangeomba ibadilishwe, ombi lingetupwa kweli?
 
Hivi waislam wakikataa Ijumaa, wayahudi na wasabato wakakataa Jumamosi, wakristo wengine wakakataa Jumapili, Freemasons wakakataa Jumatatu, Buddhist wakakataa Jumanne,wahindu wakakataa Jumatano, Wiccans wakakataa Alhamisi.

Na wote wakakubaliwa na mahakama, uchaguzi utafanyika lini ?
 
Mimi ni mkristo na sioni kama kuna tatizo lolote la kura kupigwa jumapili. Mambo mengine hayahitaji hata watu kupoteza muda wao kuyajadili. Mbona siku zote tunapiga jumapili na bado tunaendelea kuabudu bila shida
 
Ndugu zangu swala ni kuvumiliana tu.
Hivi siku Waislamu wakikataa siku ya mapumziko isiwe Jumapili badala yake iwe Ijumaa itakuwaje?
Kwani kwa maana halisi mwisho wa juma ni Ijumaa na mwanzo wa juma ni jumamosi.
 
Back
Top Bottom