Double Standard Kuhusu Kauli ya "Zanzibar Sio Nchi!"

ninslachokiamini mimi wazanzibar ni wajanja sana na wanakataa muungano huku wakisikilizia hivi kweli wabara nao hawataki muungano lakini ukweli ni kuwa wazanzibar wanataka muungano mno kuliko sisi watu wa bara.
 
Mkuu sina jazba yoyote wala chuki, niko fiti kwa kile ninachosimamia, wala usinipe pole kwa kuwa sijakwazwa au kuumia popote kwenye mjadala huu! Unaposema Wazanzibari hawataki Serikali 2 au zaidi umenukuu kauli ya nani? Mimi nimewanukuu akina Amani, Jumbe na kuhusu Sera za CUF.

Kwa kuongezea tu CCM Zanzibar walimvua uanachama Mbunge kwa kudai Serikali 3, akanyang'anywa Kadi na kuambiwa kuwa hiyo sio Sera ya CCM! Sasa wewe uko nchi gani mwenzetu?

Kwa habari ya Dola vs Nchi, mimi sijazungumzia Dola, kama unataka mjadala wa kama Zanzibar ni Dola au la anzisha tu tutatoa mawazo yetu!

Buchanan,

Nanukuu usemi wako ambao NASEMA SIO SAHIHI.

Hukumu ya Mahakama ya Rufani-Kesi ya Uhaini (Machano Hamis and others vs R case) kuwa "Zanzibar Sio Nchi" na kwamba "Uhaini hauwezi kufanywa dhidi ya Rais wa Zanzibar"

MAHAKAMA ilisema ZNZ SIO DOULA lakin kamwe, asilan, abadan haiwezi na HAIKUTAMKA KUWA ZNZ SIO NCHI. Fanya marejeo ya kesi hiyo utajiona namna ulivyopotoka.

Lakin kauli ya waZNZ kudai mamlaka kamili ipo wazi kabisa kila siku makamo 1 wa rais Znz analizungumzia hilo na ndio msimamo wa waZnz wote wanataka mamlaka kamili.

Nakupa pole kwa kuziba masikio kusikia msimamo wa Znz.
 
ninslachokiamini mimi wazanzibar ni wajanja sana na wanakataa muungano huku wakisikilizia hivi kweli wabara nao hawataki muungano lakini ukweli ni kuwa wazanzibar wanataka muungano mno kuliko sisi watu wa bara.

Je unajua kuwa ni NYERERE ndie aliekwenda Znz kuomba waungane?

lakin inaingia akilini kwa mwenye akili timamu kuona nchi yenye watu zaidi ya milioni 45 kuungana na Znz yenye watu chini ya milioni moja na nusu TENA MUUNGANO WA PASU KWA PASU?

Tena nchi kubwa inauza na kulikana jina lake na kujivika la muungano. Je hiyo ni akili kweli? au kuna namna hapo?

Utaishia kuamini tu bila kujipambanua nakupa Pole sana
 
Muungano ukivunjika kama mnavyotaka mnafikiri mtabaki Tanganyika? Anzeni kufanya land reclamation sasa hivi ili eneo liwatoshe huko baadaye! Just an advice!

Lakin na nyie mumejipangaje na changamoto hizi

1. nani mwenye mamlaka ya kuchinja. Je mumeshalipatia ufumbuzi?
2. mfumo kristo kuendesha nchi
3. malalamiko ya waislam kwa serikali na mgawanyo wa madaraka katika mamlaka.
4.MoU ya kanisa na Serikali.
na mengine mengi.

Je mumejipanga vipi?
 
Je unajua kuwa ni NYERERE ndie aliekwenda Znz kuomba waungane?

lakin inaingia akilini kwa mwenye akili timamu kuona nchi yenye watu zaidi ya milioni 45 kuungana na Znz yenye watu chini ya milioni moja na nusu TENA MUUNGANO WA PASU KWA PASU?

Tena nchi kubwa inauza na kulikana jina lake na kujivika la muungano. Je hiyo ni akili kweli? au kuna namna hapo?

Utaishia kuamini tu bila kujipambanua nakupa Pole sana

Nyerere alipropose Muungano kwa Karume ambaye alirespond "Nipo tayari hata sasa!" Leo hii mnaanza kumkejeli "Baba wa Taifa la Zanzibar?" Acheni hizo bana!
 
Nyerere alipropose Muungano kwa Karume ambaye alirespond "Nipo tayari hata sasa!" Leo hii mnaanza kumkejeli "Baba wa Taifa la Zanzibar?" Acheni hizo bana!

Nyerere ndie aliyevuka maji kwenda ZNZ kuomba muungano. JE HUJUI HATA HILO?

VIPI MUUNGANO WA PASU KWA PASU. JE KUNA USAHIHI HAPO AU NDIO HIVYO TENA?

Pole sana
 
Tanganyika haijawahi kufa hata siku moja. Tanganyika ilijibadilisha jina na kuwa Tanzania na baadae ikafanya kama walivyofanya wakoloni, wakajifanya protactorate kwa Zanzibar.
Iwapo umri wako unafikia 50 mpaka 45 unaweza kukumbuka kuwa hakukuwa na aina ya hii ya muungano wakati wa Abeid Karume.
Ajabu watu wanapiga kelele sasa kuhusu wimbo wa Taifa na amiri jeshi wa vikosi na hata bendera wakati vitu hivi havijawahi kuondoshwa Zanzibar.
Wakati wa Karume hakukuwa na uwakilishi wa Zanzibar kwenye Bunge ukiachia mawaziri kama Sepetu na Mwinyi. Karume alikuwa Amiri jeshi wa vikosi vya Zanzibar na yeye ndie aliyechagua mkuu wa majeshi ya Zanzibar. Haya yote na mengine ya utambuzi wa Zanzibar yalifanywa na Nyerere akiwepo, sasa kunakuwa na chungu ya maneno kuwa muungano uliokusudiwa ni huu tulionao sasa.
Kama unafikiri Tanzania bara ilibaki kama nchi yenye mamlaka yake naomba uniambie Serikali ya Tanzania bara ni ipi? Na Rais wa Tanzania bara ni nani? Kama utaniambia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndio Rais wa Tanzania Bara, je! ina maana Mwinyi alipokuwa rais wa Jamhuri wa Muungano ndiye aliyekuwa Rais wa Tanzania Bara. Kama ndio Hivyo hapo ni naki wa kulalamika kati ya wabara na wazenji? Maana wametawaliwa mpaka na Mzanzibar lakini wao hakuna hata mmoja wao anayeweza hata kuwa Diwani huko zenji.
 
Wakuu,

Si mara ya kwanza kwa Pinda kutamka kuwa "Zanzibar Sio Nchi" halafu kukazua mtafaruku mkubwa sana hadi tukaona purukushani za kubadili Katiba ya Zanzibar, 1984 ili ku-create "nchi" iitwayo "Zanzibar!"

Ni siku za nyuma tuliona aliyekuwa Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, pamoja na Majaji wengine wakitamka katika Hukumu ya Mahakama ya Rufani-Kesi ya Uhaini (Machano Hamis and others vs R case) kuwa "Zanzibar Sio Nchi" na kwamba "Uhaini hauwezi kufanywa dhidi ya Rais wa Zanzibar" kwa kuwa "Zanzibar Sio Nchi!" Hukumu hiyo haikuleta hasira yoyote kwa Wazanzibari lakini aliponyanyua mdomo "Mtoto wa Mkulima" kukawa na mzozo mkubwa sana ambao kila mmojawetu anaujua!

Swali ni kwamba kwa nini Wazanzibari hawakukasirishwa na kauli ya Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan wakaja kukasirishwa na kauli ile ile lakini ikasemwa na Pinda? Why double standard? Au ni chuki tu kwa watu wa bara/ Tanganyika? Juzi tena Pinda "kazungumzia kuwa wanaotaka Tanganyika waeleze ni Tanganyika ipi waitakayo!"

Hili nalo limeleta "hasira" kwa Wazanzibari hapa JF utafikiri alikuwa anazungumzia kuhusu "nchi" yao! Hawa watu huwa siwaelewi kabisa! Ila wakipewa vyeo huku Bara kwenye Wizara ambazo si za Muungano wako kimya kama wamemwagiwa maji ya baridi! Lakini utasikia eti "Waziri Mkuu Pinda mwisho wake ni kisiwa cha Chumbe!" Hatusikii wakisema Makamu wao wa Kwanza wa Rais ambaye hata Katiba ya JMT, 1977 haimtambui mwisho wake wapi!

Wao wenyewe wame-acquire ardhi na kuishi Tanzania Bara bila bughudha yoyote! Hao ndo Wazanzibari bwana!!!

mmmh Same old bullshit .....
 
wanapenda 'nchi yao'
basi hilo tu hakuna jingine,huu muungano upo tu..na kuhusu hili hata ccm nao wapo hivyo hivyo ila wao kwa sababu muungano huu asili yake ni wa kichama zaidi(tanu na asp)huwa kuna mambo wanabana kimya ili kupata muradi wao na ulwa wao. wanajua kuichezea karata ya muungano ..na upande wa pili unatumika ipasavyo kuwatumikia ccm zanzibar....
hao ndio wazenji bwana
 
Kama unafikiri Tanzania bara ilibaki kama nchi yenye mamlaka yake naomba uniambie Serikali ya Tanzania bara ni ipi? Na Rais wa Tanzania bara ni nani? Kama utaniambia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndio Rais wa Tanzania Bara, je! ina maana Mwinyi alipokuwa rais wa Jamhuri wa Muungano ndiye aliyekuwa Rais wa Tanzania Bara. Kama ndio Hivyo hapo ni naki wa kulalamika kati ya wabara na wazenji? Maana wametawaliwa mpaka na Mzanzibar lakini wao hakuna hata mmoja wao anayeweza hata kuwa Diwani huko zenji.

Ngugu yangu hii ni haki kuniuliza jawabu? Kwani Mwinyi si alikuwa Rais wa Zanzibar na alikuwa na Mawaziri wake na alipokuwa Rais wa Muungano aliunda Baraza la Mawaziri wa Zanzibar? Hebu hawa Mawaziri wenu kina Sitta , Magufuli, Chenge na wengineo ni wa Serikali gani?
 
"NJE YA MUUNGANO HAKUNA ZANZIBAR BALI KUNA UNGUJA NA PEMBA" (J.K. Nyerere, 1995). wanadai wasichokijua hao. By the way, washanyonya sana lakini hawakui, waacheni wakajitegemee watatia akili.
 
cha kushangaza Mhe Pinda huyu huyu even baada ya kupigwa vijembe kwa kauli yake bado hajalearn kwamba mfumo wa mbili haukubaliki. Sijaona kikubwa katika matamshi yyake zaidi ya kuwaamsha wazanzibari walioambiwa wao ni nchi ndani ya nchi, alipotamka Mhe Pinda tena bungeni ndio vuguvugu la kubadili katiba lilipoanza. Sio double standard, atakumbukwa kwa kuamsha demokrasia iliokuwa katika usingizi mzito. Kwa kauli ya mahakama still wazanzibari hawakuliona kubwa pia kwa wakati ule hasa kwa vile wanajuwa mamlaka ya kuipindua hayatakuwepo hasa baada ya muungano na kwamba suala la ulinzi ni la muungano na hivyo lisingewezekana. Iko mifano ya miungano ya defence kama wa EU ambapo nchi mwanachama hawezi kupinduliwa japo kuwa nchi husika zimebaki sovereign kamili, Charter zao zimeweka wazi kuzilinda nchi wananchama. Lakini Kauli ya Pinda kama kiongozi mkuu wa serikali ndio iliopiga msumari wa ukweli kwamba hakukuwa na nchi kama ambavyo wazanzibari walivyoamini.
 
Muungano wa Serikali 3 utaongeza kero zaidi ya kuzipunguza! Ukiangalia Rasimu ya 2 utaona tayari matatizo yatakayokuwa created na hizo Serikali!
Katiba ya Muungano (kwa mujibu wa Rasimu hiyo) sio Supreme kwa maana kwamba katiba 3 (ya Zanzibar, Tanganyika na Muungano) zina hadhi sawa!
Nyerere aliwahi kusema kwenye kitabu chake cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania" kuwa "Mafahali wawili hawakai zizi moja" na kwamba Tanganyika atakuwa Gorbachev wa kuiua Tanzania na akifanya hivyo atajimaliza mwenyewe!"
Kwa hiyo hapa tusidanganyane, tunaruka mkojo na kukanyaga kinyesi!
Unasema nini?
Unaogopa Tanganyika kuwa Gorbachev?
Tanganyika itajimaliza yenyewe?
Hii ndio hofu yako inayokufanya ukatae Tanganyika?

Unachotaka kusema hapa ni kuwa Kama Tanganyika isingeungana na Zanzibar, Tanganyika ingekuwa imeshajimaliza?
Ingejimaliza vipi? Au itajimaliza vipi?

Kwa hiyo muungano upo ili kuisaidia Tanganyika isijimalize? Fafanua hii hoja uliyoiibua mkuu.
 
Back
Top Bottom