mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Msajili wa vyama vya siasa amebariki uamuzi wa Mbatia na Sekretarieti yake yote KUTOJIHUSISHA na siasa ndani ya NCCR Mageuzi hadi itakapoamuliwa vinginevyo (yaani endapo wataenda mahakamani), Lakini tukija upande wa wabunge wa Covid 19, wenyewe wataendelea KUJIHUSISHA na siasa ndani ya CHADEMA (ikiwemo kuiwakilisha bungeni) hadi itakapoamuliwa vinginevyo (na mahakama). Hapa nanukuu:
"Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, leo Mei 25 imebariki Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Sekretarieti yake yote kusimamishwa na kuwataka kutojihusisha na siasa ndani ya chama hicho hadi uamuzi huo utakapoamuliwa vinginevyo"
Hii imekaaje!! Sijui huko nje tunaonekanaje? Hivi hata ile aibu tu ya kawaida hakuna?