NCCR Mageuzi yamsimamisha James Mbatia kufanya shughuli za Chama

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wake, James Mbatia kufanya shughuli zote kisiasa za chama hicho mpaka pale atakapoitwa kwenye mkutano mkuu kujieleza.

20220521_122040.jpg


=======

Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shuhhuli zozote za chama hadi mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma inazowakubali.

Uwamuzi huo umefanyika leo Jumamosi Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza amesema walipokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini.

Amesema pamoja na mabadiliko hayo kulikuwa na ajenda nyingine ambayo ni kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara kutokana na maazimio hayo wanasubiri barua rasmi ili kutoa taarifa.

"Tuna orodha yetu tutaenda kuangalia kama mlivyoona wajumbe wapo na akidi imetimia hivyo tunangoja barua rasmi kisha tutaenda kupitia na katiba yao," amesema Nyahoza.

Pia soma > Mgogoro NCCR Mageuzi: Timu Mbatia wachukua ofisi, wasema umefanyika uhaini ndani ya chama,
 
Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wake, James Mbatia kufanya shughuli zote kisiasa za chama hicho mpaka pale atakapoitwa kwenye mkutano mkuu kujieleza. https://t.co/oESTFbJvKNView attachment 2232853
Bora huko nccr viongozi wapo huru kumuhukumu mwenyekiti wa chama. Upande wa pili mwenyekiti huwa haguswi hata pale anapotoa boko mchana kweupe. Na anapojitokeza wa kujaribu kufuata sheria za chama dhidi ya kiongozi wa chama basi anakiona cha mtema kuni. RIP Chacha Wangwe.
 
Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wake, James Mbatia kufanya shughuli zote kisiasa za chama hicho mpaka pale atakapoitwa kwenye mkutano mkuu kujieleza.

View attachment 2232853
Japo Waliomsimamisha hawajataka kutupa sababu ya Maamuzi yao haya, ila kwakuwa tunajua ni Mchagga na anatokea Mkoani Kilimanjaro kwa Mashemeji zangu tumeshajiongeza na kujua ni nini.
 
Akienda mahakanani utasikia,"kuna vigogo wa CCM wapo nyuma yake". 😁.
 
Back
Top Bottom