Mnaomtetea Mbatia toeni hoja za msingi acheni kutafuta kichaka vya kujificha

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Nimeona baadhi ya watu wanaopinga MBATIA kufukuzwa uanachama ndani ya NCCR MAGEUZI wakitoa hoja isiyo ya msingi ambayo wanataka kuimezesha kwenye vichwa vyetu ya kudai kuwa kufukuzwa kwake kumechangizwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa huku wakisahau MBATIA siyo wa kwanza kufukuzwa uanachama na chama chake.

Kuna viongozi wengi wa vyama vingine vya upinzani ambao pia walifukuzwa uanachama na vyama vyao, Je ofisi ya Msajili ilihusika katika hayo?

ZITTO KABWE alifukuzwa uanachama ndani ya CHADEMA baada ya kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa jambo ambalo lilimkera sana Mbowe na Wenzake, akaundiwa Kila aina ya Tuhuma, akaitwa Msaliti, Mamluki, anatumiwa na CCM, anatumiwa na Usalama wa Taifa, anatumiwa na Ofisi ya Msajili na kadharika.

Pia, ikumbukwe kuwa migogoro ya ndani baina ya wanachama na viongozi ilimwondoa Mzee MREMA (RIP) ndani ya NCCR MAGEUZI akahamia TLP. Mambo kama hayo pia yalimwondoa HAMAD RASHID CUF na kufutwa uanachama na kuamua kuanzisha chama chake ADC.

Hivyo hivyo walifanya wafuasi wa Marehemu Maalim SEIF mbele ya Prof. LIPUMBA alipogoma kuunga mkono upitishwaji wa LOWASSA kugombea Urais.

Sasa swali la kujiuliza ni kwamba, Je? Halmashauri wote wa NCCR MAGEUZI walitumwa na Msajili wa vyama vya siasa kumuhujumu MBATIA.

Yaani Msajili wa vyama achague kumuhujumu Mbatia kupitia wana NCCR MAGEUZI ambao huko nyuma walitofautiana mitazamo na Mwenyekiti wao.

Bado nawaza madhara na uzito aliyonayo MBATIA kiasi hadi kuhujumiwa na Msajili.!!

Mnapogombana kwenye vyama vyenu njia nyepesi ni kutoa majibu ya hoja za pande zinazokinzana nanyi.

Kwa mujibu wa kanuni na sheria ya vyama vya siasa, Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa hualikwa kuhudhuria mikutano yote ya kikatiba inayoitishwa na vyama mbalimbali

Si kazi ya Msajili wa vyama vya siasa kubashiri kuwa katika mkutano alioalikwa na NCCR MAGEUZI Moja kati ya kitakachotokea ni MBATIA KUSAMISHWA UONGOZI

Ndio maana hata siku ZITTO anafukuzwa uanachama Ofisi ya msajili ilikuwepo.

Ndio maana hata siku CHADEMA inamkaanga Dkt. SLAA na kumpitisha LOWASSA kugombea Urais, Ofisi ya Msajili ilikuwepo

Ushamba wa kuisingizia ofisi ya Msajili na serikali kwa migogoro ya ndani ya vyama vya siasa umeshachuja. Haunogi Tena.
 
Back
Top Bottom