Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,024
- 1,612
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, leo Mei 25 imebariki Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na Sekretarieti yake yote kusimamishwa na kuwataka kutojihusisha na siasa ndani ya chama hicho hadi uamuzi huo utakapoamuliwa vinginevyo.
Mnamo Mei 21, Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi ilimsimamisha Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shughuli zozote za chama hadi mkutano mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma zinazowakabili.
Pia soma:
- NCCR Mageuzi yamsimamisha James Mbatia kufanya shughuli za Chama