Dotto Bulendu: Tumefika Hapa? Hakika Tumepoteza Mwelekeo kama Taifa

Kalyempari
Dotto Bulendu namfahamu vizur Sana na Ni ndugu yangu wa karibu Sana. lkn lazima nikili kwamba....
Tangu kusitishwa kakipindi kake Flani pale star TV na kauwezo kake ka kufikiri kameshuka Kama 37% ivi,yaani anacopy tu matukio pumba tupu ataki kuumizwa kichwa
 
Ameandika Mwandishi Dotto Bulendu

1.Amejeruhiwa na Risasi mchana kweupe,wenzake pamoja na Kiongozi wao mkuu wa mhimili wakaenda kumuona hospital ya Rufaa akiwa hajitambui,anavuja damu,haongei wala hajui chochote.

2.Alipelekwa Hospital Nairobi bila uficho,Rais mstaafu wa nchi hiyo,Makamu wa Rais wa nchi wakaenda Nairobi kumuona na kumpa pole.

3.Familia yake ikaandika barua ofisini kwake kuomba apatiwe haki yake ya matibabu,ofisi yake ikajibu kuwa haiwezi kubeba hizo gharama kwani utaratibu wake wa kwenda Nairobi Hospital eti haukufuatwa.

4.Akatangazwa kusitishiwa mshahara wake,akalalamika baadae akarudishiwa mshahara Kama ilivyo kawaida.

Akiwa kitandani anaupambania uhai wake,akatangazwa kuwa amefutwa ubunge kwa madai kuwa hajulikani alipo na hajajaza fomu za mali na madeni za watumishi kwa mujibu wa sheria,kuondoshwa kwenye ubunge kwa tuhuma hizi kutamuweka nje ya ulingo wa kuwania nafasi za uwakilishi za kisiasa mfano Ubunge na Urais kwa miaka mitano.

Haki ya msingi ya binadamu yeyote ni haki ya kuishi,ndiyo maana linapokuja suala la kupigania Uhai gari la kubeba wagonjwa halifungwi na sheria za barabarani maana tunalenga kuokoa uhai wa binadamu.

Mtu mwenye utu,anayeamini Mungu yupo,anayesali Kanisani ama msikitini au popote hawezi weka masharti kwenye suala la kuokoa uhai wa mtu.

Mtu mwenye utu,anayemuogopa Mungu hawezi fanya sherehe ya kufurahia bunadamu mwenzake kupita kwenye tishio la kupoteza uhai.

Mtu anayemuogopa Mungu hawezi shabikia tishio ana jaribio la binadamu mwenzake kuuawa,leo kama kuna mtu anamdhikahi mtu aliyenusulika kifo na kuwa sehemu ya mkakati wowote wa kumzidishia mateso binadamu yeyote aliyepo duniani kwa kusudi la Mungu akasome Mwanzo,Zaburi,injili,Ufunuo na Quran tukufu aone kama kuna sehemu inayosema tufurahie mateso ya wenzetu.

Kwa nini ufurahie mateso ya mwenzako?Maandiko matakatifu yanatuambia amri kuu kuliko zote ni Upendo,kweli tumefika mahali upendo siyo sehemu ya maisha na sasa tunaweza furahia mateso ya binadamu?

Sheria tulizotunga wenyewe zinasema Uhai ni moja ya msingi mkuu wa binadamu,Uhai hauna mbadala,ukitoka umetoka,leo kweli tunajenga jamii ya watu wanaoweka masharti makali dhidi ya binadamu anayepigania uhai wake?

Leo tumefika mahali binadamu wanapelekena kwenye vyombo vya sheria tena za binadamu kuvutana kwa hoja kuwa mgonjwa alikosea ama hakukosea kupambania uhai wake?

Leo tunajenga jamii inayokusubiri unasuke na kifo halafu ianzishe mjadala wa kama ulikosea ama kupatia kuupambania uhai wako?

Ni jamii hii hii inayosali kwa kusema...

"Eeeh mwenyezi Mungu Mtukufu ,
Muumba Mbingu na Dunia
Umeweka katika Dunia Serikali za wanadamu na Mabunge ya mataifa ili haki yako itendeke""

Kila nikisoma mistari hiyo, najiuliza ni haki gani tunaizungumzia? wakati haki ya kwanza ya binadamu yeyote ni uhai?leo tuna jamii isiyoguswa na uhai wa binadamu,ipo tayari kwenda kubishana kisheria eti binadamu aliyeupambania uhai wake kakosea na anastahili Adhabu?

Ni Mungu yupi tunayemtaja kila siku?ama kuna Mungu mwingine ambaye hatambui thamani ya uhai na ameweka mipaka ya namna ya kuupambania uhai?maana jumapili iliyopita nilipokwenda kusali,tukaambiwa Mungu wetu hapendi watu wanaojikweza na waliojaa viburi.

Mungu anatutaka tuwe wanyenyekevu,tusubiri kukwezwa na tusijikweze,tunajenga jamii ya watu wenye viburi,wasiostushwa na kuono mioyo ya watu inajazwa chuki.

Eeeh Mwenyezi Mungu utusaidie.
I love it
 
*Anaandika Dotto Bulendu wa DW-Sauti ya Ujerumani Na Star TV*

1.Amejeruhiwa na Risasi mchana kweupe,wenzake pamoja na Kiongozi wao mkuu wa mhimili wakaenda kumuona hospital ya Rufaa akiwa hajitambui,anavuja damu,haongei wala hajui chochote.

2.Alipelekwa Hospital Nairobi bila uficho,Rais mstaafu wa nchi hiyo,Makamu wa Rais wa nchi wakaenda Nairobi kumuona na kumpa pole.

3.Familia yake ikaandika barua ofisini kwake kuomba apatiwe haki yake ya matibabu,ofisi yake ikajibu kuwa haiwezi kubeba hizo gharama kwani utaratibu wake wa kwenda Nairobi Hospital eti haukufuatwa.

4.Akatangazwa kusitishiwa mshahara wake,akalalamika baadae akarudishiwa mshahara Kama ilivyo kawaida.

Akiwa kitandani anaupambania uhai wake,akatangazwa kuwa amefutwa ubunge kwa madai kuwa hajulikani alipo na hajajaza fomu za mali na madeni za watumishi kwa mujibu wa sheria,kuondoshwa kwenye ubunge kwa tuhuma hizi kutamuweka nje ya ulingo wa kuwania nafasi za uwakilishi za kisiasa mfano Ubunge na Urais kwa miaka mitano.

Haki ya msingi ya binadamu yeyote ni haki ya kuishi,ndiyo maana linapokuja suala la kupigania Uhai gari la kubeba wagonjwa halifungwi na sheria za barabarani maana tunalenga kuokoa uhai wa binadamu.

Mtu mwenye utu,anayeamini Mungu yupo,anayesali Kanisani ama msikitini au popote hawezi weka masharti kwenye suala la kuokoa uhai wa mtu.

Mtu mwenye utu,anayemuogopa Mungu hawezi fanya sherehe ya kufurahia bunadamu mwenzake kupita kwenye tishio la kupoteza uhai.

Mtu anayemuogopa Mungu hawezi shabikia tishio ana jaribio la binadamu mwenzake kuuawa,leo kama kuna mtu anamdhikahi mtu aliyenusulika kifo na kuwa sehemu ya mkakati wowote wa kumzidishia mateso binadamu yeyote aliyepo duniani kwa kusudi la Mungu akasome Mwanzo,Zaburi,injili,Ufunuo na Quran tukufu aone kama kuna sehemu inayosema tufurahie mateso ya wenzetu.

Kwa nini ufurahie mateso ya mwenzako?Maandiko matakatifu yanatuambia amri kuu kuliko zote ni Upendo,kweli tumefika mahali upendo siyo sehemu ya maisha na sasa tunaweza furahia mateso ya binadamu?

Sheria tulizotunga wenyewe zinasema Uhai ni moja ya msingi mkuu wa binadamu,Uhai hauna mbadala,ukitoka umetoka,leo kweli tunajenga jamii ya watu wanaoweka masharti makali dhidi ya binadamu anayepigania uhai wake?

Leo tumefika mahali binadamu wanapelekena kwenye vyombo vya sheria tena za binadamu kuvutana kwa hoja kuwa mgonjwa alikosea ama hakukosea kupambania uhai wake?

Leo tunajenga jamii inayokusubiri unasuke na kifo halafu ianzishe mjadala wa kama ulikosea ama kupatia kuupambania uhai wako?

Ni jamii hii hii inayosali kwa kusema...

"Eeeh mwenyezi Mungu Mtukufu ,
Muumba Mbingu na Dunia
Umeweka katika Dunia Serikali za wanadamu na Mabunge ya mataifa ili haki yako itendeke""

Kila nikisoma mistari hiyo,najiuliza ni haki gani tunaizungumzia?wakati haki ya kwanza ya binadamu yeyote ni uhai?leo tuna jamii isiyoguswa na uhai wa binadamu,ipo tayari kwenda kubishana kisheria eti binadamu aliyeupambania uhai wake kakosea na anastahili Adhabu?

Ni Mungu yupi tunayemtaja kila siku?ama kuna Mungu mwingine ambaye hatambui thamani ya uhai na ameweka mipaka ya namna ya kuupambania uhai?maana jumapili iliyopita nilipokwenda kusali,tukaambiwa Mungu wetu hapendi watu wanaojikweza na waliojaa viburi.

Mungu anatutaka tuwe wanyenyekevu,tusubiri kukwezwa na tusijikweze,tunajenga jamii ya watu wenye viburi,wasiostushwa na kuono mioyo ya watu inajazwa chuki.

*Eeeh Mwenyezi Mungu utusaidie.*

MY TAKE;
Tumefika hapa, hakika tumepoteza mwelekeo kama taifa lililokuwa na heshima ya utu uliotukuka na kuwa mabarazuli.
 
Tunatakiwa ku keremua ngonjera: Mtukufu rais wa awamu ya tano amethubutu kujenja standard gauge rail, kuangusha miti milioni moja ili kujenga stigilars George, kujenga vituo 65 vya afya, kutoa bora elimu bure.

Zidumu Giles za mwenyekiti wa chama💪🏾
 
Polisi,viongozi na watu mbalimbali waliuawa kwa kupigwa risasi pale Kibiti lakini hukuweza kulaani kwa kuandika makala kama hii Ila umeona TL ni more human than those who were killed by unidentified gun men.

My Take: We are all equal in eyes of GOD
 
Kwa hiyo hayo yanalipiwa kwa Tundu Lisu. Kosa moja halihalalishwi kwa kosa jingine. Kuweni na roho ya binadamu
Polisi,viongozi na watu mbalimbali waliuawa kwa kupigwa risasi pale Kibiti lakini hukuweza kulaani kwa kuandika makala kama hii Ila umeona TL ni more human than those who were killed by unidentified gun men.

My Take: We are all equal in eyes of GOD
Yo
 
Unajifanya hujui yaliyompata Azori Gwanda?
 
Polisi,viongozi na watu mbalimbali waliuawa kwa kupigwa risasi pale Kibiti lakini hukuweza kulaani kwa kuandika makala kama hii Ila umeona TL ni more human than those who were killed by unidentified gun men.

My Take: We are all equal in eyes of GOD

Mungu Jehovah aonae yaliyo sirini na ahukumu kwa haki. Kila aliehusika kwa namna yeyote kudhulumu haki ya mtu na akutane na ghadhabu ya Bwana na damu aliyoimwaga na iwe juu yake na VIZAZI vyake.
 
Back
Top Bottom