Nimejiridhisha kwamba, kelele zisizo haki, hazimzuii Paul Makonda kufika alikompangia Muumba!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,957
4,140
Kelele zingelikuwa ndio kizuizi cha mtu kufikia hatima Yake, watu wengi tungelikufa mapema.

Tukiorodhesha tuhuma hapa kumhusu Makonda, kitabu chenye kurasa elfu kinajaa.

Tukisikiliza clips za watu wasio haki wakipiga kelele zinazompinga Makonda, hakuna mwenye MB za kutosha kuzisukiliza zote.

Watu waliomtishia kumfikisha kwenye vyombo vya sheria lakini wakaishia kupanua madomo yao na wsitende chochote, ni maelfu kwa maelfu.

Wengine walienda mbali zaidi hata kufikia kumtishia uhai wake, lakini Paul Makonda, ndio kwanza Mungu anazidi kumnawirisha.

CCM ni chama kikubwa mno, kinawafahamu watu wake, makonda isingelikuwa rahisi kuaminiwa tena kwa tuhuma zile ziliimbwa na wapinzani wake kisiasa!

Na sasa wengenewe wengi, bado wangali wakipiga kelele juu ya Makonda!

Ni vyema kutambua sasa kuwa, Mungu akipanga jambo lake, hata dunia yote ikawa kinyume na huyo mtu, Mungu atalifanya.

Kelele za wasio haki, hazizuii kusudi la Mungu kumhusu mtu wake.

Niwashauri kama alivyowashauri Elia wale mabaali.

Ongezeni kelele mkazidi sana kuzipaza, labda shetani atawasikia!
 
Uko sahihi sana. Mungu ni wetu sote. Ni kama jua tu hutuangaza wote. Ukitaka kumuelewa Mungu utajikuta huna imani. Hitler,Gadafi,Mandela,Obama,Papa Francis na Mother Theresa wote hawa wana Mungu na wote aliwainua kwa nyakati tofauti. Nachotaka kusema ni kuwa,kuna watu wanacheza kidunia na kidunia wanaonekana anayewafanyia ni Mungu,kwasababu tu wanaoshinda makanisani wangelitamani kuwa kama Makonda ila haiwi. Hakuna mtihani mgumu kama kumuelewa Mungu na ukimpima kwa vyeo na mali,hutasali.
 
Kwa hiyo umeona Makonda kupewa kile cheo alichokuwa nacho Mjema au yule kijana Mzanzibar aliyekuwa anakwenda mapumziko Lamu ndio mafanikio yake?
Unajua makusudio ya Mungu wewe? Acha aendelee kufanya hiyo kazi ya u MC wa chama, kama alitenda yasemwayo utakuja ona matokeo yake muda ukifika.
 
Niko ubalizo wa Marekani hapa kuomba documents!!

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Kelele zingelikuwa ndio kizuizi cha mtu kufikia hatima Yake, watu wengi tungelikufa mapema

Ni vyema kutambua sasa kuwa, Mungu akipanga jambo lake, hata dunia yote ikawa kinyume na huyo mtu, Mungu atalifanya

Kelele za wasio haki, hazizuii kusudi la Mungu kumhusu mtu wake

Ongezeni kelele mkazidi sana kuzipaza, labda shetani atawasikia!
Naunga mkono hoja, huyu ni mpakwa mafuta wa Bwana, Bwana Ndie Anasimama nae
CCM inazidi kuimarika, kupendwa na kukubalika, hadi makapi ya ndani ya chama, yameanza kujichuja yenyewe!!, si mnaona!.

Na hapa ndio mwanzo tuu wa hizi amsha amsha!, kama ni mvua, hii ni rasha rasha tuu!, mvua halisi ni 2025!.

Ila pia kijana ni msikivu sana, alianza kwa moto sana, tukampooza Pongezi Paul Makonda kuifufua CCM kwa amsha amsha. Twende mdogomdogo ngoma ikivuma sana inakaribia kupasuka! sasa anakwenda vizuri!.

Na kwa vile humu umezuka mtindo ukimkubali mtu ukamsifia na kumpongeza, huchelewi kuitwa chawa!,
angalia huyu dogo sisi kaka zake, tumeanza nae wapi.

Mimi nilianza nae hapa Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Nikaja hapa Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Alipopitia misukosuko tukasimama nae kwanza kwa kutoa wito Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... kisha tukamshauri Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .
Kuna watu wenye roho za kwanini tukawaambia Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!
Na mwisho nikapendekeza Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...

P
 
Hii nayo ni moja wapo ya kelele zilezile
Hakuna kelele, wala nini! Sioni kama kuna sababu za msingi za yeye kutumia jina na cheti cha kitaaluma cha mtu mwingine.
Labda kama hiyo skendo yake ni ya uongo, basi ajitokeze hadharani na kutuambia ukweli ni upi.
 
Hakuna kelele, wala nini! Sioni kama kuna sababu za msingi za yeye kutumia jina na cheti cha kitaaluma cha mtu mwingine.

Labda kama hiyo skendo yake ni ya uongo, basi ajitokeze na kutuambia ukweli ni upi.
Umemalizia vema mkuu

Na kama umelijua hili, basi tulia, la hauwezi, thibitisha ufek wa jina lake!
 
Uko sahihi sana. Mungu ni wetu sote. Ni kama jua tu hutuangaza wote. Ukitaka kumuelewa Mungu utajikuta huna imani. Hitler,Gadafi,Mandela,Obama,Papa Francis na Mother Theresa wote hawa wana Mungu na wote aliwainua kwa nyakati tofauti. Nachotaka kusema ni kuwa,kuna watu wanacheza kidunia na kidunia wanaonekana anayewafanyia ni Mungu,kwasababu tu wanaoshinda makanisani wangelitamani kuwa kama Makonda ila haiwi. Hakuna mtihani mgumu kama kumuelewa Mungu na ukimpima kwa vyeo na mali,hutasali.
Hekima hii
 
Kwa hiyo umeona Makonda kupewa kile cheo alichokuwa nacho Mjema au yule kijana Mzanzibar aliyekuwa anakwenda mapumziko Lamu ndio mafanikio yake?
Unajua makusudio ya Mungu wewe? Acha aendelee kufanya hiyo kazi ya u MC wa chama, kama alitenda yasemwayo utakuja ona matokeo yake muda ukifika.
Muda upi?
 
Mungu akipanga jambo lake, hata dunia yote ikawa kinyume na huyo mtu, Mungu atalifanya
Huyo Mungu ndiye kamuinua Daudi huko CCM au mama Abdul ndiye kafanya hayo?

Ipo wazi kabisa kuwa CCM ni wakiukaji wakuu wa haki, ni wezi na wanyang'anyi, wanajimilikisha mali za umma na kuzifanya kuwa mali za chama chao.

Ni vyema unapotuma neno "Mungu" kusifia wao wezi na wanyang'anyi uwe unatofautisha ni Mungu yupi, tambua hata shetani ni mungu tena wa dunia hii (include 🇹🇿)
 
Kelele zingelikuwa ndio kizuizi cha mtu kufikia hatima Yake, watu wengi tungelikufa mapema

Tukiorodhesha tuhuma hapa kumhusu Makonda, kitabu chenye kurasa elfu kinajaa,

Tukisikiliza clips za watu wasio haki wakipiga kelele zinazompinga Makonda, hakuna mwenye MB za kutosha kuzisukiliza zote

Watu waliomtishia kumfikisha kwenye vyombo vya sheria lakini wakaishia kupanua madomo yao na wsitende chochote, ni maelfu kwa maelfu

Wengine walienda mbali zaidi hata kufikia kumtishia uhai wake, lakini Paul Makonda, ndio kwanza Mungu anazidi kumnawirisha!

CCM ni chama kikubwa mno, kinawafahamu watu wake, makonda isingelikuwa rahisi kuaminiwa tena kwa tuhuma zile ziliimbwa na wapinzani wake kisiasa!

Na sasa wengenewe wengi, bado wangali wakipiga kelele juu ya Makonda!

Ni vyema kutambua sasa kuwa, Mungu akipanga jambo lake, hata dunia yote ikawa kinyume na huyo mtu, Mungu atalifanya

Kelele za wasio haki, hazizuii kusudi la Mungu kumhusu mtu wake

Niwashauri kama alivyowashauri Elia wale mabaali,

Ongezeni kelele mkazidi sana kuzipaza, labda shetani atawasikia!

Huyu Mungu mngemjua vyema msingekuwa mnamzihaki namna hii, hachelewi kumpa mtu haki yake. Hata kama ni kuwa kiongozi wa Malaika.
 
Huyo Mungu ndiye kamuinua Daudi huko CCM au mama Abdul ndiye kafanya hayo?

Ipo wazi kabisa kuwa CCM ni wakiukaji wakuu wa haki, ni wezi na wanyang'anyi, wanajimilikisha mali za umma na kuzifanya kuwa mali za chama chao.

Ni vyema unapotuma neno "Mungu" kusifia wao wezi na wanyang'anyi uwe unatofautisha ni Mungu yupi, tambua hata shetani ni mungu tena wa dunia hii (include 🇹🇿)
Uko sahihi mkuu!

Ila sasa, maombi yako na kelele zako zimezuia nini kwa makonda kuendelea kuwepo hapo alipo
 
Uko sahihi mkuu!

Ila sasa, maombi yako na kelele zako zimezuia nini kwa makonda kuendelea kuwepo hapo alipo
Hata Nduli Idi Amini hatukuthubutu kumzuia alipovamia nchi yetu, na tulipopigana naye tulipoteza watu wetu wengi sana, na mbaya zaidi tulianguka kiuchumi hadi wa leo japo Nduli alishatoweka😂

Kelele kuhusu Makonda ni jambo la muda tu, kumbuka, kila jambo na wakati wake...

Kuna wakati wa kuishi bila kitambi.

Kuna wakati wa kuishi na kitambi.

Kuna wakati wa kuwekwa huru.

Kuna wakati wa kuwekwa kuzuizini

Kuna wakati wa kutukana watu na kuna wakati wa kutukanwa na watu nk

Mwisho wa yote kuna wakati wa kurudi mavumbini na hapo ndio huwa mwisho wa makelele yote.

Daudi na CCM wana mwisho wake, ukitambua hilo utaachana na uchambuzi wa vihoja kufagilia wahuni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom