Yanayoendelea bungeni, ni dhahili kwamba Watanzania tunadharauliwa na viongozi waandamizai wa serikali na wabunge wetu, hasa wa chama cha mapinduzi. Yani Mh. Mbowe pamoja na ujumbe na ushahidi mzito wa nyaraka aliouwasilisha juu ya Mh. Rais kuhusika moja kwa moja katika ukwapuaji pesa za escrow, pia kuthibitisha uwongo uliosemwa jana na waziri Muhongo juu ya mwanasheria wa TANESCO ndugu Ngwilima kwamba hakufukuzwa kazi bali aliaacha mwenyewe, mtu aliyekuwa mzalendo kwa kutoa ushauri usio na maslahi kwa wachache bali kwa taifa, kisha uzalendo wake kusababishia kufukuzwa kazi, bado watu, yaani wabunge wengi wa CCM hawashituki, wameendelea na utetezi wa hoja za kufundishwa ambazo hazihitaji elimu ili kujua kwamba wamefundishwa, hii ni dharau kubwa hasa kwa sababu sisi twaonekana ni wajinga sana na hakuna tuwezalo kufanya. Tuamke NDUGU, tumebakiza moja tu, halihitaji kuunganishwa na vyama vya siasa bali na utanzania unaopambana dhidi ya dhuluma hii. Tuingie BARABARANI TUU NA KUUKATAA UPUUZI HUU. Binafsi nawapongeza wabunge wote wateteao masrahi ya watanzania kwa utashi wao wote.