Donge nono kutolewa: Nimeibiwa


Yeah upo sahihu sana. Wao wezi hatakuwa wametoka mbali. Akifanya kama ulivoshauri atapata vituvyote kasoro pesa tu


 

kwani mwizi akibadilisha OS siamna kitu? eSET inaondoka kabsa
 
kwani mwizi akibadilisha OS siamna kitu? eSET inaondoka kabsa

Baada ya installation unatakiwa ufungue account Eset, wizi unapofanyika unafungua account yako kwenye computer nyingine na kutoa taarifa za wizi wa laptop. Mwizi wako anapowasha laptop anapigwa picha kupitia webcom na picha utazikuta kwenye account yako, Kisha wanakutumia map itakayokuonyesha mtaa na nyumba ilipofichwa laptop yako.

Eset ilimkamatisha kijana fulani maeneo ya mikocheni aliyekuwa akipora wanafunzi laptop walikuwa kundi la vijana waliokuwa wanatumia gari dogo lenye vioo vyeusi. Kijana aliyeporwa laptop alichofanya ni kufungua account yake na kuriport wizi, ilichukua muda wa wiki moja kwani hawakuifungua mara moja, walipoiwasha webcom ikachukua picha zao pamoja na map ya eneo ilikofichwa, yule kijana baada ya kupata picha na map wakaondoka na vijana wenzao kuhakiki kama ramani waliyopewa ndipo penyewe, na walipofika eneo hilo waliuliza wenyeji kama wanamfahamu kijana mwenye gari dogo lenye rangi nyeusi na vioo vyeusi, walionyeshwa nyumba anayokaa, sawa sawa na map inavyoonyesha. Walitoa taarifa polisi na walipofika kwenye nyumba hiyo waliwakuta hao vijana, na nyumba ilipokanguliwa laptop yake ilipatikana pamoja na zingine nyingi sana zilizoibiwa.
 
Pole sana mkuu,hayo ndio maisha halisi ya watu wa Dar,tunaishi kwa mashaka sana,sijui kwa watu wenye mihela yao lakini kwa sisi wenye vipato vya kawaida tunao own vigari vyetu used vya kijapan maisha ni ya mashaka sana,imefikia wakati hua naona ni bora nipande daladala nakuwa na amani kuliko nikitoka na gari kwenda katikati ya jiji.
 
Aisee pole sana, shida hizo kazi za watu kama ndio picha za harusi kwa kweli lazima uchanginikiwe,jitahidi kupitia kwenye hawa wenye studio,na waliokuibia ni watu watakuwa wanakujua na wanajua kazi yako, pole ndugu.

Tukisikia tutakujulisha sababulazima hizi tabia za wizi zikomeshwe kwa nguvu zote.
 
kama kweli uko siriaz na vitu vyako nenda mtaa wa bunge ukivuka flats za nssf kwa mbele upande wa kulia kuna duka la mangi jana kuna mtu alikua anauza external naamini zitakua ni hizo, ukienda na polisi umeliwa!

Hawa ndio wafuga wezi hawa, si wakuchekewa.

Ndio hao hao akina Mbowe. Kwa pesa wamefanya mpaka aliyekuwa "shetani" kawa malaika aliyekuwa "malaika" kawa shetani.
 
Jamaa kajipatia capital ya kutosha ya kuanzisha b'ness ila kwa mwizi kila atakachoiba shetan wake anamnong'oneza kuwa hicho ulichoikwapua hakitoshi,baaas hadi pale 40 yake itakapofika.Pole sana mwathirika wa hili.
 
Siku nyingine hakikisha unatumia principles za backup mfano HDD and laptop havitakiwi Kuwa pamoja but ajali no ajali na pole sana
 
Acha begi ofsn au nyumbani au beba mgongoni utembee nalo. Utaingia gharama ya kutafuta laptop mpya na ku fix kioo, na data muhimu zimepotea. Vinginevyo, kama eneo lina mlinzi, mshikishe hata buku 2, hatoenda mbali na gari lako.

Mkuu ukibeba mgongoni nadhani kazi yao inakuwa rahisi zaidi
1.moja wanajua kwamba unamali

2.hawapati tabu ya kuanza kutafuta mzigo uko wapi.

3.watatumia nguvu nyingi kupora wanaweza hata kugharimu uhai wako
 
Ajali haina kinga kaka, msaada tu jamaa apate vitu vyake, japo nadhani zile mil 3 hatazihitaji zirudi.

Ajali INA KINGA! Wewe bado umepotoshwa na imani za kikale. Na kinga yake ilikuwa ni kutoacha vitu vya thamni kwenye gari! Ona umeenda ''shule ya gharama kubwa'' kujifunza somo dogo tu...
 
Hawa ndio wafuga wezi hawa, si wakuchekewa.

Ndio hao hao akina Mbowe. Kwa pesa wamefanya mpaka aliyekuwa "shetani" kawa malaika aliyekuwa "malaika" kawa shetani.
Wewe binti mtarajia kufurahishwa na marijali 70 peponi, ni nini tena hiki?
 
Jamani kumlaumu huyu au kumdhihaki haitasaidia kitu,kama mtu ana mbinu za kumsaidia apate vitu amsaidie kwa upande wangu nakushauri wasiliana na polisi wa maeneo hayo huwa wana contacts za wezi wote utavipata vitu vyako vyote but kwa kutoa kitu kidogo
 
Hivi siku hizi hakuna Waganga wa kienyeji wenye TV inayokuonesha mwizi wako?
 
Hapo kwenye blue bold kama sijaelewa au! yaani mtu ameshindwa kujilinda hadi anaibiwa halafu anaahidi kumlinda yeyote atakayefanikisha kuvipata vifaa vyake!
Atamlinda kwa maana ya kumpatia baashishi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…