Donge nono kutolewa: Nimeibiwa

Donge nono kutolewa: Nimeibiwa

Pole sana daaah inauma sana ila mtazamo wa huyo aliyekwambia tafuta masela wa eneo husika nadhan linamantik
 
Pole sana lakini, Dah! mali zote hizo kuziwacha ndani ya gari na wewe kuondoka ni uzembe wa hali ya juu, hususan hapa Dar, inajulikana wazi kuwa kuna vibaka wa kwenye magari.



Hivi magufuli yupo wapi?
 
Huo ni zaidi ya msiba mkuu..
Ikishindikana kabisa kupata vitu basi tupitishie bakuli tuchangie..

Iwe funzo pia kwa wengine kama Hard disk ni ya back up basi ikae mahali salama sio kutembea nayo kila kona
 
Pole sana. Kama gari lako halina alarm, jaribu kuweka, inaweza saidia kukustua kama mtu akivunja.
 
Ajali haina kinga kaka, msaada tu jamaa apate vitu vyake, japo nadhani zile mil 3 hatazihitaji zirudi.
Hizo hazirudi mkuu mpaka dakika hii robo Zimeshakuwa kwenye mfumo wa safari lager au viloba
 
Nilishawahi kuibiwa bag lina laptop na external hard drive na mbaya zaidi sikufanya backup ya vitu vilivyo kwenye computer.
Siku nyingine nikawa naficha vitu kwenye buti au chini ya seat.

Two months ago walivunja kioo na kuondoka na laptop ya mshkj ambayo aliiweka chini ya seat. Nikaingia gharama za kuchonga kioo. Usiweke kwenye buti wala chini ya seat, beba mgongoni.
 
Kuwa makini siku hizi jamaa wana detectors nafikiri wanasearch hadi kwenye buti

Duh m hua naweka chini ya seat nikijua ni safe kumbe adi wanadetector solution hapa sijui n nini.
 
Duh m hua naweka chini ya seat nikijua ni safe kumbe adi wanadetector solution hapa sijui n nini.

Acha begi ofsn au nyumbani au beba mgongoni utembee nalo. Utaingia gharama ya kutafuta laptop mpya na ku fix kioo, na data muhimu zimepotea. Vinginevyo, kama eneo lina mlinzi, mshikishe hata buku 2, hatoenda mbali na gari lako.
 
Pole sana je ile laptop uliweza kuisajiri kwenye icloud kama ambavyo iphone na ipad ili kuweka ulinzi wa kutosha
 
Faiza ni kweli ila jamaa anasema alikuwa anaingia just kumcheki mshikaji waondoke it was within fraction of a second.

Huyo "jamaa" alikuwa hana simu? Halafu wizi wa Dar si wajinga, mmoja akiwa anavunja na mwengine anakufata ulipokwenda ili usiwastukize ghafla.
 
funga ip spy camera na intruder sensor, mwizi akivunja kioo inapiga alarm huku ikirecord kila kitu kinachoendelea na kutuma kwenye smart phone yako.
 
Mwambie anichek...hao wez nakuhakikishia watakuja na laptop kichwan wakikutafta wenyewe, nitafte kabla ya siku saba hazijaisha. Palipovunjwa usipatengeneze maana ndipo watakapovirudisha vitu kama walivyochukua. Asante
 
Mwambie anichek...hao wez nakuhakikishia watakuja na laptop kichwan wakikutafta wenyewe, nitafte kabla ya siku saba hazijaisha. Palipovunjwa usipatengeneze maana ndipo watakapovirudisha vitu kama walivyochukua. Asante

Weka namba
 
Mbona meseji kama hii imepostiwa na mdada fb sasa muhusika ni nani.mbona siwaelewi
 
Mbona meseji kama hii imepostiwa na mdada fb sasa muhusika ni nani.mbona siwaelewi

Kasema mumsaidie kupost kwenye whatsapp group mbalimbali ivo wengne wameona uzito wamepost facebook, ni sawa na wewe ukipost hili tangazo litaonekana kama ni lako.
 
Back
Top Bottom